Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Ningependa kiwe na habari za ujumla zinaizunguka jamii,kama siasa,burudani michezo, dini/imani na kadhalika.
Lakini ili kiwe na ushawishi na mvuto,
kiwe kinatoa habari ambazo hazipatikani katika media nyingine kwa maana kitoe behind-the-scene info zinazohusu matukio makubwa katika lugha nyepesi na inayoeleweka.
b. Kiwe na mjumuisho pia wa matukio mengine makubwa ulimwenguni lakini yenye "positive relevance" kwa Tanzania.
c. Kijarida hicho,kikiweza kuwa na vikaragosi,hata kwa uchache tu,pia itasaidia kutoa mvuto na kufikisha ujumbe kwa jamii.
Ningependa kizungumzie jinsi muda unaotumika kulalamika bila kufikia tamati ya kuwa na mkakati thabiti wa kubadili matatizo yanayowakabili wadanganyika unavyoweza kutumika vema na kubadili fikra na maisha yao.
Ningependa kiwe na habari za ujumla zinaizunguka jamii,kama siasa,burudani michezo, dini/imani na kadhalika.
Lakini ili kiwe na ushawishi na mvuto, kiwe kinatoa habari ambazo hazipatikani katika media nyingine, kwa maana kitoe behind-the-scene info zinazohusu matukio makubwa katika lugha nyepesi na inayoeleweka.
Kijarida hicho kinaweza kuwa na mjumuisho pia wa matukio mengine makubwa ulimwenguni lakini yenye "positive relevance" kwa Tanzania.
Pamoja na yaliyosemwa na waliotangulia ku post.. pia ningependa kiwe na " summary" ya mambo muhimu yanayoandikwa na magazeti ya kiingereza kama East Africa etc ili nami nisiyejua kiingereza nisipitwe;
Ningependa kiwe 'website based' kihabarishe kwa ufupi habari zilizojiri kutoka mitandao ya tanzania na ya watanzania walio nje, kwa nia ya kuhabarisha na sio ngono au udaku kwa vile vijarida vya udaku viko kila kona Tanzania, vilevile kuwe na kurasa mbili tatu maalumu kwa comments za wadau ambazo zitolewe direct toka kwenye forums kama hii ya JF nk,
Ukianza kusoma huwezi kuweka chini na ukifika mwisho unataka kumpatia mwingine naye asome.
Pamoja na yaliyosemwa na waliotangulia ku post.. pia ningependa kiwe na
1. " summary" ya mambo muhimu yanayoandikwa na magazeti ya kiingereza kama East Africa. (hiyo summary iwe kwa Kiingereza au Kiswahili?)
2. kiwe na matangazo ya fursa mbalimbali - kazi, biashara, n.k lakini siyo matangazo ya waganga wa kienyeji na dawa zao za mapenzi etc;
3. aidha font zake zisiwe ndogo sana; kiwe cha rangi pia itanivutia zaidi.
Ningependa liwe na sehemu ambayo kutakuwa na mazungumzo ya watu wa pande mbili,ya kwanza ni ile ya serikali ikieleza namna ilivyojipanga kumkomboa Mtanzania(hasa mwenye kipato cha chini)pia maelezo ya progress ya implementation ya hzo strategy.Kwa upande wa pili,Mtanzania wa chini apewe nafasi ya kueleza ni yapi anayaona kama mdau mlengwa wa strategy za serikali.Challenges,failures and areas of success from their point of view.Kwa hitimisho la hayo,awepo mtu huru&mtaalamu ambaye ataanalyze maoni ya pande zote mbili bila kuwa biased na ushauri wake kama itabidi.
1. Ningependa kiwe 'website based' kihabarishe kwa ufupi habari zilizojiri kutoka mitandao ya tanzania na ya watanzania walio nje,
2. Kuwe na kurasa mbili tatu maalumu kwa comments za wadau ambazo zitolewe direct toka kwenye forums kama hii ya JF nk,
Rev. Kishoka,
Huwezi kufanya mpango na kuchapisha vijarida vidogo vya kusambaza nchi nzima BURE, ili uwafikie walio wengi? Manake nadhani watu wengi vijijini huku hawanunui magazeti. Asante.
Kwa hicho kijarida chako Mzee Mwanakijiji. Unaweza kuzungumzia/kufuatilia utendaji wa vyombo vya serikali manake uzembe ni mwingi sana.
Kila toleo unawa-interview watu wa kawaida kabisa kona zote Tanzania nawatakueleza maoni yao. Ambayo unaweza kutumia kama msingi wa matoleo. Kasi na uhakika wa habari.