Napendekeza kuwepo na kipengele cha Video kwenye mtihani wa sekondari

sanalii

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,434
5,095
Nimefikiria kua kwenye mtihani wa kidato cha nne na/au cha sita kuwe na kipengele cha video ambacho wanafunzi watajibia maswali.

Kila mwaka NECTA inachagua au inaandaa video yenye angalau saa moja ( one hour length video) ambayo wanafunzi wataangalia na kisha watajibia swali / maswali ambalo litakua sehemu ya kuchagua.

Swali hili linawekwa kweny masomo ya lugha, kunaweza kua na video mbili, moja ya kingereza na nyingine ya kiswahili, zenye content tofauti.

Faida.
1. Kupima listening and observing skills ya wanafunzi
2. ⁠Itawasaidia wanafunzi ambao hupendelea zaidi audio visual kama njia ya kujifunza
3. ⁠kuwapa na kuweza kuwapima wanafunzi katika maarifa ya kisasa zaidi ( current issue ) kwakua video itakua inabadilika kila mwaka.

4. Itakua more competent based , haina Tahakiki wala kukariri majina ya wahusika

kwamfano mwaka 2024 video yao inakua documentary ya construction of Nyerere hydroelectric power dam.
May be 2025 video inakua “The covid 19”

Yani content inakua inabadilika kila mwaka.
Tofauti na vitabu vilivyochaguliwa ambavyo havibadiliki siku zote, ingawa dhamira zao zadumu lakini ni ngumu ku cover current issues, hiyo tunasema ni moja ya udhaifu wa fasisi andishi.

Kuhusu changamoto
naamini kua sekondari nyingi zipo maeneo ambayo si ndani ndani sana, kama shule haina TV, yaweka kua mwalimu ana laptop,

Pia video hiyo iwe uploaded Youtube so wanafunzi wanaangalia hata kwenye simu za wazazi ndugu na jamaa.

Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom