Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,695
- 40,721
Fikiria unapata kijarida cha kurasa mbili au nne hivi cha Kiswahili ambacho ni cha bure kabisa. Ni kijarida cha habari na maoni kinachojaribu kuunganisha mambo yanayozungumzwa kwenye mitandao mbalimbali na mtu wa mitaani ambaye hana internet lakini anaweza kunufaika na mijadala hiyo. Kijarida ambacho ukianza kusoma huwezi kuweka chini na ukifika mwisho unataka kumpatia mwingine naye asome. Ni kijaridha chenye mvuto wa ajabu, chenye habari za kina, hoja zenye ushawishi na burudani ya kuangalia. Kijarida ambacho ni cha bure kabisa lakini ubora wa kinachopatikana ndani yake unashindana na magazeti makubwa.
Sasa wewe jichukulie ni mtu wa "kawaida" whatever that means, unayejua lugha ya Kiswahili, Kiingereza cha kuyupia maji, na mikononi mwako hauna zaidi ya dakika kumi na tano za kupoteza. Unapewa kijarida mkononi na rafiki yako, unategemea kitu gani kimo ndani ya kijarida hicho ambacho kitakufanya utafute siku nyingine na nyingine na nyingine?
Yaani kijarida ambacho unaweza kumwambia rafiki yako, jamaa au ndugu kuwa lazima akitafute. Na hakihusiani na mambo ya ngono lakini kinavutia kina baba na kina mama, wasomi na wasio wasomi, matajiri na maskini na wote wanaposoma wanajiambia moyoni "hiki ni kijarida chetu".
NINI UNATARAJIA KIWEMO NDANI YA KIJARIDA HICHO? Sasa msilete stori ndeeeefu.. toa wazo na mawazo yote yanapokelewa na hakuna wazo lolote baya, duni, dhaifu, au la kuchekesha au kuudhi!