Ungemshaurije ingekuwa ni wewe

Theodora

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
802
570
Nawasabahi wote wanaMMU. Kuna wakati unadhani ya kwako mazito hadi usikie ya mwenzako aisee.

Rafiki yangu yuko kwenye mahusiano na jamaa na wana mtoto sasa eti kamtumia ujumbe wa sms jana 'kuna binti nimempa mimba.

Nimeshindwa kumshauri maana najua advise yangu ingekuwa negative.

Maana jamaa ninavyomfahamu uaminifu ni zero. Na mimi nilifanya maamuzi magumu kwenye maisha yangu muda sio mrefu kwenye mambo hayohayo ya uaminifu.

Je, ungemshauri vipi?
 
Hapo hakuna cha kuuliza anatakiwa tu kuachana naye na huyu Mhuni alee motto wake. Yaani wanaume huku ana mwanamke huku anataka yaan yanatamaa kama mapaka. Siyapendi mimi. Kwanini lakini. na hapo ukimuuliza atasema samahani ilikuwa shetani amenipitia huyo shetani kwa wanaume kila siku. Waende zao huko.
 
katumiwa sms tu!!! hebu afuatilie km its true maana ukute anamjaribu maana kuna vichaa wengine hutumia mbinu km hizo kuona reaction ya mwanamke, so awe na busara tu afuatilie akiujua ukweli ndio mengine yafuate, hawa viumbe jamani(wanaume) ni wa kuwaombea tu
 
Yaani hilo nalo anahitaji ushauri?

Kweli kuna watu ikija kwenye busara na hekima za kawaida tu ni ziro kabisa!
 
Mahusiano yao ni ya ''kuunga-unga''? Kwa watu makini wenye kupendana na waliolala kwenye HUBA, huyo shoga yako angesubiri kuonana ''LIVE'' na huyo shemeji yako waliongee kwa kina kama lipo, maana yawezekana huyo bwana kakutana na mtu akamwambia '' we handsome naomba tutafute mtoto''. Katuma hiyo sms kupima upepo.
Yote kwa yote maamuzi hufanyika baada ya kupata taarifa, taarifa sahihi husaidia kutoa maamuzi SAHIHI.
 
Hapo hakuna cha kuuliza anatakiwa tu kuachana naye na huyu Mhuni alee motto wake. Yaani wanaume huku ana mwanamke huku anataka yaan yanatamaa kama mapaka. Siyapendi mimi. Kwanini lakini. na hapo ukimuuliza atasema samahani ilikuwa shetani amenipitia huyo shetani kwa wanaume kila siku. Waende zao huko.

Punguza spidi kidogo,
C unajua? 'Can't live with, can't live without (without:bila kumkufuru Mungu)'
 
Waume walikuwa zamani, siku hizi wamebaki wanaume,,,I don't like them at all,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom