Ungekuwa unapata hela kila DAWASA na TANESCO wanapoomba radhi kwa kukukosesha huduma, ungekuwa na milioni ngapi saivi?

Ungekuwa unapata hela kila DAWASA na TANESCO wanapoomba radhi kwa kukukosesha huduma, ungekuwa na milioni ngapi saivi?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
710
Reaction score
1,610
Wakuu,

Nadhani saivi ningekuwa na mjengo wangu wa maana huku Mbezi Beach, pamoja na ndinga kaliiiiiii.

Jamani, hakuna taasisi/shirika la kiserikali linakera kama DAWASA Wizara ya Maji na TANESCO 😫😫😫, yaani mtu ungekuwa na mamlaka unazifutilia zote mbali kila kitu kinaanza upya kwa kuwa na watu wenye weledi, na kuwa na mifumo ambayo wakizingua tu unakula kichwa, hakuna protection ya Rais. Huu uchawa wa kiduanzi ndio unatuletea hizi huduma za kipuuzi.

Tatizo la presha kuwa ndogo kuliko kawaida na maji kukatika ndio imekuwa kawaida yetu sasa, kwanini mnatufanyia hivi? Na sisi kama kenge tupo tu.

Unamkosesha mtu huduma mwezi, unaishia tu kumpa samahani, hii KUNRADHI inasaidia nini DAWASA, TANESCO? Inafidia mtu alichopoteza?

Wenzetu unamkosesha huduma unatakiwa kumfidia, hata kama ni kwa masaa machache, ila kwakuwa wanaongoza kenge na nyani basi wanafanya tu mnavyotaka.

Kwa TANESCO kuna zile zinautwa tire sijui phaze, ambako kulingana na matumizi yako unaweza kuhamishwa toka kwa yule wa aliyekuwa ya 5 ambaye akinunua umeme wa elf 10 anapata units 75 - matumizi madogo na ikizidi hapo unaondolewa huko ambako kwa elf 10 unakuwa unapata unit 28.

Hivi mnajua kama huduma ya kurudisha watu kwenye matumizi madogo hata kama mtu amekidhi vigezo kwa Dar imesitishwa? Wanaorudishwa ni hao wa mikoa mengine tu?

Yaani wewe tuseme ulikuwa na friji, au jiko la umeme ambalo lilikuwa linafanya matumizi yako kuwa makubwa lakini friji/jiko la umeme limeharibika, au maisha yamebadilika umerudi kwenye ubachelor wa chumba kimoja, hutumii tena vitu hivyo na matumizi yameshuka, ama kwa sababu nyingine mbalimbali matumizi yako yameshuka, kwa miezi mitatu (kwa vigezo vilivyowekwa na TANESCO), wewe mkazi wa Dar HUTARUDISHWA KWA WENYE MATUMIZI MADOGO, utaendelea kupata units 28 hivyo hivyo kwa elfu kumi!

Kama si wizi ni huu TANESCO? Yaani nikosa vigezo nitolewa,lakini nikiwa navyo mkatae kunirudisha kwakuwa nipo Dar? Kwasababu ukiwa Dar kuna ruzuku unapewa inayopunguza makali ya maisha?

Turudi kwenye mada, ungekuwa unalipwa kila mara unapoombwa radhi na DAWASA, TANESCO ungekua na kibunda cha sh ngapi?

Kwa huu mwaka tu pekee ningekuwa na si chini ya milioni 10🥲🥲, nilikuwa sielewi kwanini sijawa milionea bado, kumbe ni DAWASA na TANESCO ndio wananikwamisha😒😒
 
Back
Top Bottom