Imaniyanguitaniponyatu
Member
- Aug 23, 2021
- 54
- 87
Bei ya mahindi nchini Tanzania inaogofya sana hadi kufikia 100000-130000 kwa gunia la kilo 100 kwa baadhi ya mikoa ya nchi hii.
Kupanda kwa bei ya mahindi imepelekea wananchi wa kawaida kununua unga wa kupikia ugali kati ya 1400-2000 kwa kilo moja, hali ya upatikanaji wa chakula hicho inazidi kuwa ngumu na bei hii ni katika muda ambao wakulima wanajitahidi kuuza mazao yao wapate pesa ya kujikimu.
Maswali ya kujiuliza bei itakuwaje itakapofika miezi ya mwishoni ya mwaka huu.?
Hali hii imekuwa ikilalamikiwa na mamilioni ya Watanzania kuwa serikali imesababisha ongezeko la bei za vyakula nchini na lawama zote akitupiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, wengine walienda mbali zaidi wakisema maisha ya bara yanakuwa magumu wakati Zanzibar maisha ni mepesi ya kwamba Zanzibar wanapata bidhaa hizo kwa bei nafuu mno.
Kwingineko katika nchi ya Kenya wenyewe mambo yameenda ndivyo sivyo ambapo sasa wanatumia zaidi ya 105 Kshs kununua kilo moja ya unga wa mahindi ambazo ni sawa na 2050 za kitanzania, Taarifa kamili kuhusu kupanda bei ya bidhaa hii huko Kenya na sababu zake pengine zitakuwa ndio zile zile kama za Tanzania tu pengine, Serikali ya Kenya nayo pengine imesababisha kupanda bei kwa bidhaa hiyo.
TUTAJARIBU KUFANYA MIZANI LIDOGO KARIBIA NCHI ZOTE ZA AFRIKA MASHARIKI.