Unga Unawamaliza Wasanii wa Bongo Flava

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18

3495466.jpg

Albert Mangwea ‘Ngwair’,
Muziki wa kizazi kipya Bongo Flava uko hatarini kutokana na kwamba mastaa wake wengi ambao wamewahi kutamba katika fani hiyo wanaanza kupotea mmoja mmoja baada ya kupata pesa na kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.Unga unaimeng’enya Bongo Flava
Mambo hayapo ok, Bongo Flava inazidi kumeng’enywa na nguvu kazi yake inapungua. Hapa ni gumzo kuwa vijana wengi wapo kwenye skendo ya kutumia dawa za kulevya.

Kuna maswali magumu; Kwanini baadhi ya wasanii wana-shine kidogo, wanakubalika kitaa na kiasi fulani maisha yao kuwa bora lakini ghafla tu madogo wanaonekana kitaa wamechoka na afya zimekuwa dhaifu.

Madai ya msingi ni matumizi ya dawa za kulevya a.k.a unga, kwamba madogo wengi wakishakubalika kitaa kwa njia moja au nyingine hujiingiza kwenye matumizi ya unga, wanabwia na wengine wanajidunga kabisa.

Its dangerous! The only gent on kundi marehemu la Wakilisha, Langa Kileo anaweza kuwa mfano hai, baada ya kukiri kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa iliyopita kuwa alikuwa anabwia unga lakini sasa amestop. Langa alisema kuwa alikuwa mbwiaji mzuri wa Cocktail kabla ya hivi karibuni kuugua typhoid, hivyo kukosa access ya kupata unga.

Alisema, alianza kama utani lakini baadaye alizidiwa na akawa hawezi kuacha, ingawa sasa hivi anamshukuru Mungu kwamba yamepita. Katika hilo, Langa alieleza kwamba angalau sasa anajisikia nafuu na afya imeanza kurejea. Hiyo ni kauli ya Langa kupitia session ya Crazy Friday, lakini ukweli ni kuwa madogo kibao wapo kwenye skendo ya kubwia.

Albert Mangwea ‘Ngwair’, Heri Samir ‘Blu’ Mark II B a.k.a Simba ni kati ya majina ambayo yanatajwa kwenye orodha ya wanaodaiwa kubwia unga. Hayo ni majina yanayotajwa lakini nyuma ya pazia ni wengi na hii inasababisha kizazi kipya kisiwe na afya standard. Madogo wanasimama vizuri lakini baadaye wanakuwa dhoofu l’hali. Hii ni hatari na sisi kama wadau tunalaani vikali matumizi ya dawa za kulevya.

Source: abdallahmrisho.blogspot.com
 
Unategemea nini kwa watu waliolewa sifa na kujiona wako sayari mpya!...Not proffessional, no responsibilities, no machinery to observe laws...nothing....completely nothing...fyuuuuup!
 
acha wamalizike mi sioni wana faida gani kwa nchi hii na kizazi kijacho.kwanza wanatuharibia tu watoto
 
Ndio maana akiperform wimbo 1 hoi kbsa, hat wa 2 hakumbuki lyrics tena.
 
Mi siwashangai hawa vijana sababu maisha yao ni yakuiga,muziki wanaofanya ni wakuiga,sasa chaajabu nini wakiiga kula nyunga kitu kilichoanza kwa wanao waiga?
 
Bado mko negative sana nao, madawa ya kulevya ni tatizo kubwa sio kwa bongo flava hata vijana wengine uhsusani walio mijini. Rehabilitation centers zinahitajika zaidi kutibu tatizo kuliko kuwashambulia waathirika huku hatua nyingine zikichukuliwa kupambana na matumizi ya madawa.

Kuiga tu sidhani kama ndio chanzo cha matatizo bali vijana wengi wameunga unga sana maisha yao na frustration kibao ndio wanajikuta wako huko, mapromota na distributers achilia mbali wachuuzi wa kanda wamekuwa wakinufaika na jasho lao na hakuna yeyote aliyesimama na kuwatetea zaidi ya kugonga copy.
 
Nadhani swali la muhimu hapa ni " je tutawasaidia je wasanii wa kitanzania kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya" ?..! Tukiwaongelea wasanii tu katika hili si sahihi na haitosaidia kwani si tatizo kwa wasanii peke yao ,hatuwezi jua huenda hata watoto wetu waweza kujiingiza ktk matumizi hayo ya madawa ya kulevya..! Waswahili husema..Mwenzio akinyolewa wewe tia maji...!

 
............................Mwenzio akinyolewa wewe tia maji...!


Waache wafu wazike wafu wao!
.
.
.
 
Banza Jiwe!

Matonya vipi? nilisikia alikamatwa china,kama ni ukweli hatutamuona tena kule wananyonga tu
 
Langa,mangwair,banza,daz baba,diouf,blue,tid,nice,bushoke,dully,ray c,20% orodha ni ndefu ila wapo ambao si rahisi kuwagundua akiwemo nelly kamwelu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom