Habari wana JF, Kadri siku zinavyozidi kwenda watu wenye uzito ulipitiliza wamekuwa wakiongezeka kwa kasi sana. Kwa Nchi za wenzetu wanauchukia sana unene kutoka na athari zake lakini cha kushangaza Tanzania ni Tofauti mtu anaponenepa hupewa sifa nyingi sana ikiwemo kuonekana maisha ameyapatia.
Kwa kifupi ukiwa na uzito mkubwa kupitiliza unakuwa kwenye Hatari zaidi kuliko mwenye uzito wa kawaida ya :-
1. Kupata kisukari
2. Kupata Magonjwa ya Moyo
3. Kupata shinikizo la damu -pressure
4. Kupata kansa mbali mbali
5. Kupata maumizi ya Muda mrefu ya Mgongo ,Magoti na visigino vinavyoweza kuambatana na Ganzi au la
6. Tafiti pia zinaonyesha wanawake wenye uzito mkubwa hupati shida kubeba ujauzito sababu ya kutobalance kwa hormone .
...na mengine mengi .
Hayo Magonjwa hapo Juu ni magonjwa ambayo siyo ya kuambukiza na Ndiyo magonjwa yanayoongoza kwa kuwa na gharama kubwa za matibabu hususani gharama kubwa za Dawa ,Je kwa hii kasi NHIF itatoboa ?
Kama una miaka chini ya 60 na hujui uko kundi lipi hebu chukua peni na karatasi fanya hesabu hii
BMI(Body Mass Index )=Uzito(kg)/(Urefu katika mita)^2
Yaani chukua uzito wako katika Kilogram gawa kwa kipeo cha pili cha urefu wako katika mita .Mfano ukiwa na kilo 60 na urefu wa sentimita 165 itakuwa hivi BMI =60/(1.65)^2 utapata 22.03.. .
Jibu utalopata angalia maelezo hapa
¡. 18.5-24.9 uzito wako unaendana na mwili .
¡¡.25-29.9 Uzito wako umezidi jitathmini
¡¡ .30 na kuendelea uzito wako ni mkubwa sana fanya jitihada uupunguze .
Tusisifiane wakati tunakaribisha shida siku kukutana na mtu ana pressure na magonjwa ya moyo katika umri wa miaka 30-40 ni imeongezeka sana Garama za haya magonjwa kila mwezi ni kubwa kasi ikiwa kubwa sana huu mfuko wa bima wa Taifa Utalemewa labda tukibadilika kuna Baadhi ya gharama zitapungua.