Naunga Mkono hoja kwa asilimia Miamoja na nachangia zaidi kwamba kwa maoni yangu;
1.Wakati wa uundaji wa misingi waepuke kabisa utaratibu wa CCM wa wagombea kugeuka wafadhili wa CHAMA katika ngazi husika jambo linalo athiri uwezo wa wanachama kujitambua na kuelewa jukumu la ukombozi na uhusika wao kwa kila mmoja katika kukijenga CHAMA na kugeuka kuwa ombaomba,wapiga dili za kitapeli kwa kuwagonganisha wagombea
2.Kuwakataa katika hali zote watu wanaojitokeza kwa kuibuka kiujanjaujanja na kutaka kugombea nafasi za viongozi hasa baada ya kuona kwamba hawana nafasi ya kupitishwa kwenye vyama vyao sasa wanaamua kukimbili CHADEMA si kwasababu ya kupenda itikadi ya CHAMA bali tamaa za madaraka ,ukubwa na pesa jambo linaloathiri CHAMA na kuharibu mikakakti na taswira ya CHAMA katika Jamii ya Tanzania.
3.Kuhakikisha wagombea mbalimbali wanaandaliwa kwa utaratibu maalum wa kuwachunguza watangaza nia na kuona uthabiti wao na kujitoa kwao kwa chama Kabla na baada ya kutangaza nia pamoja na uadilifu wao kwa jamii.Wote watakao onekana kutafuta uongozi kiccm ccm wapigwe chini.
4.Kuhakikisha kwamba wanatoa nafasi shirikisha na mafunzo maalum kwa potential candidates WA CHAMA na kuhakikisha kwamba chama kina jijenga na kujumuisha Taswira ya wanajamii wote katika ngazi zote na siyo watu wa Rika moja tu kujiona kuwa bora,wachapakazi na wenye haki zaidi katika CHAMA.
5.Kuhakikisha kwamba kunakuwa na uratibu mzuri wa M4C katika Kanda na kuwa na mikakati endelevu ya Kichama inayotekelezeka kuelekea matukio yote muhimu ya Kitaifa ambayo chama kinaamini kuwa na Maslahi nayoa mf. Kura za Maoni kuhusu katiba Mpya,Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.
6.Kuimamarisha na kueneza elimu ya Uraia na Uzalendo kwa wananchi pamaoja na wananchama wote wa CDM.
7.Kuweka Mkakati maalum wa kuhakikisha wapenzi ,wanachama na marafiki wote wa Chama wanajiandikisha katika Dftari la kudumu la Mpiga kura na kutunza shahada yao na kuandaliwa uhamasishaji wa kujitokeza kupiga kura ususan kwa Kizazi kipya ambacho hakitaki hata kusikia Jina la CCM likitajwa.