Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa

Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa

Nakubaliana na wewe kwamba ni kwa mtazamo wako!
Na si mtazamo tu bali hata na "IMANI" yako ndivyo ilivyo kwake!
Mimi naamini kazi ya ZZK huku CHADEMA,...
Swali ni je, kuna nini hadi CCM wafurahie kazi ya kuimarika kwa upinzani?!
Haya ni mapenzi ya PAKA kwa PANYA

CCM ndio ilitoa kibali cha kuanzishwa vyama vingi ili Demokrasia ishamiri.
 
Naunga Mkono hoja kwa asilimia Miamoja na nachangia zaidi kwamba kwa maoni yangu;

1.Wakati wa uundaji wa misingi waepuke kabisa utaratibu wa CCM wa wagombea kugeuka wafadhili wa CHAMA katika ngazi husika jambo linalo athiri uwezo wa wanachama kujitambua na kuelewa jukumu la ukombozi na uhusika wao kwa kila mmoja katika kukijenga CHAMA na kugeuka kuwa ombaomba,wapiga dili za kitapeli kwa kuwagonganisha wagombea

2.Kuwakataa katika hali zote watu wanaojitokeza kwa kuibuka kiujanjaujanja na kutaka kugombea nafasi za viongozi hasa baada ya kuona kwamba hawana nafasi ya kupitishwa kwenye vyama vyao sasa wanaamua kukimbili CHADEMA si kwasababu ya kupenda itikadi ya CHAMA bali tamaa za madaraka ,ukubwa na pesa jambo linaloathiri CHAMA na kuharibu mikakakti na taswira ya CHAMA katika Jamii ya Tanzania.

3.Kuhakikisha wagombea mbalimbali wanaandaliwa kwa utaratibu maalum wa kuwachunguza watangaza nia na kuona uthabiti wao na kujitoa kwao kwa chama Kabla na baada ya kutangaza nia pamoja na uadilifu wao kwa jamii.Wote watakao onekana kutafuta uongozi kiccm ccm wapigwe chini.

4.Kuhakikisha kwamba wanatoa nafasi shirikisha na mafunzo maalum kwa potential candidates WA CHAMA na kuhakikisha kwamba chama kina jijenga na kujumuisha Taswira ya wanajamii wote katika ngazi zote na siyo watu wa Rika moja tu kujiona kuwa bora,wachapakazi na wenye haki zaidi katika CHAMA.

5.Kuhakikisha kwamba kunakuwa na uratibu mzuri wa M4C katika Kanda na kuwa na mikakati endelevu ya Kichama inayotekelezeka kuelekea matukio yote muhimu ya Kitaifa ambayo chama kinaamini kuwa na Maslahi nayoa mf. Kura za Maoni kuhusu katiba Mpya,Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.

6.Kuimamarisha na kueneza elimu ya Uraia na Uzalendo kwa wananchi pamaoja na wananchama wote wa CDM.

7.Kuweka Mkakati maalum wa kuhakikisha wapenzi ,wanachama na marafiki wote wa Chama wanajiandikisha katika Dftari la kudumu la Mpiga kura na kutunza shahada yao na kuandaliwa uhamasishaji wa kujitokeza kupiga kura ususan kwa Kizazi kipya ambacho hakitaki hata kusikia Jina la CCM likitajwa.

Mkuu.

Mawazo yako tumeyachukua na hakika tayari kuna mengi ya msingi ambayo kwetu ni kama umekazia maarifa maana tumesha anza kuyafanyia kazi kwa hatua na kwa umakini wa hali ya juu.

Ubarikiwe mpaka upigwe na butwaa! Hadi kieleweke.
 
Molemo, mwaka 2012 ulipobandika thread hii, ulizungumza kinabii, na maadui wa CDM ndicho wanachopigania ili kuwatenganisha Dk Slaa na Mbowe, kumbe mikakati ya kumchafua na propaganda dhidi ya Dk Slaa, na hata wafadhili wa PM 7 na waungaji mkono wa Zitto kutoka Lumumba Team na CDM, na mitafaruku inayotokea sasa ni nia ovu ya kuisambaratisha CDM.

Mkuu Wimana umeongea kweli Tupu.

Mungu amekuwa mwema sana kwa Chadema na amewafunika kwa wema wake viongozi mashujaa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

Mungu kwa kumtumia Ben Saanane kundi haramu la PM 7 liliweza kugundulika ambalo lilikuwa na njama za kuwafitinisha viongozi hawa majabali!

Endeleeni kuomba na kufunga ili viongozi hawa walibdwe kama mboni ya Jicho.
 
Last edited by a moderator:
Shida yako ni kuwa mgumu wa kuelewa mtoa mada anasema "kulingana na utaratibu wa wanasiasa wengi wa Afrika mwenyekiti wa chama ndie rais wa nchi"
Unataka CDM iongozwe kwa kufuata katiba yake, au huo utaratibu wa wanasiasa wako wengi?!!
 
Acheni demokrasia ichukue mkondo wake

Demokrasia bila Nidhamu ni uhuni mtupu na Fujo.

Anayedhani anaweza kuleta uhuni Chadema kwa vigezo vya demokrasia aende akaendeshe shamba lake huko....
 
Unataka CDM iongozwe kwa kufuata katiba yake, au huo utaratibu wa wanasiasa wako wengi?!!

Wewe Magamba na Katiba ya Chadema wapi na wapi.

Unajifanya kuijua Katiba ya Chadema kuliko ya Magambani.Pole zako!
 
Demokrasia bila Nidhamu ni uhuni mtupu na Fujo.

Anayedhani anaweza kuleta uhuni Chadema kwa vigezo vya demokrasia aende akaendeshe shamba lake huko....
Aondoke awaachie shamba lenu, sio?!! Pole sana.
 
Wapeni uongozi wa milele kama huyu hapa:

images
 

Attachments

Mkuu mlemo: 2po pamoja haya mambo n moja ya changamoto kwa wana chdm,hapa chdm ilipo fika ni kwa mchango mkubwa wa hawa vionzi.ndiyo maana nasema kuna msukumo wa upande wa pili wanao upata hawa wana chdm wanao jifanya hawaon maendeo makubwa ya chama.
 
mkuu umemsahau zito kabwe .uhodali wake na upiganaji wake umeonekana toka mwanzo.

WanaJF,

Nimekuwa mfuatiliaji wa wanasiasa mashuhuri Tanzania,Afrika na duniani kwa ujumla.Nimekuwa nikipenda kufanyia uchunguzi wanasiasa hawa walipoanzia harakati zao na mafanikio yao binafsi na ya wananchi wao wanaowaongoza.Nitakuwa nikijadili wanasiasa mbalimbali kwa awamu na leo ningependa nianze kuwajadili wanasiasa mashuhuri Tanzania, Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

Kwanini nimewachanganya Pamoja?

Ni ukweli ulio dhahiri kwamba huwezi kuwatenganisha wanasiasa hawa wawili hasa unapojadili mafanikio ndani ya Chadema.Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Wilbroad Slaa ni Katibu mkuu wa Chadema Taifa.Viongozi hawa wawili wamekuwa mhimili mkuu wa siasa za Chadema. Kitu kikubwa walicho nacho viongozi hawa wawili ni Ushirikiano wao.

Kila mmoja ana utaratibu wake katika uongozi lakini ushirikiano wao katika kazi umeifanya Chadema iwe moja na imara kama ilivyo.Ni vigumu kumsikia yeyote kati yao akisema kitu tofauti na mwenzake.Ninaamini hata kama kuna lolote ambalo wanakuwa hawakubaliani wanalimaliza ndani kwa ndani na kamwe humsikii yeyote akiongea tofauti na mwenzake.

Huu ndio uongozi unaotakiwa na hakika ndio siri kubwa iliyofanya Chadema ifike hapa ilipo.Kitu kikubwa kilichowapa credit kubwa viongozi hawa wawili ni pale Mwenyekiti Freeman Mbowe alipoachia nafasi ya kugombea urais kwa Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.Kwa aina ya viongozi wa Afrika tulio nao ni vigumu sana kuona spirit ya aina hii.

Na endapo kama hili lingefanikiwa basi Tanzania kwa mara ya kwanza ingekuwa kama nchi za Ulaya na Marekani ambapo Rais wa nchi siyo mwenyekiti wa chama tawala.Lakini kingine kikubwa kinachowapa sifa wakuu hawa wawili ni wazi wanaongoza jopo la vijana mbalimbali wasomi na wenye nafasi mbalimbali za uongozi.

Tunajua kuongoza vijana ni kazi hasa tunaposema vijana bado damu inachemka,lakini vijana hawa wamefundwa na wanawatii viongozi wao mfano John Mnyika,Godbless Lema,Halima Mdee,Tundu Lissu,Ezekiah Wenje,John Heche,Zitto Kabwe na wengine wengi.


Mafanikio yao

Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamepata mafanikio makubwa katika uongozi wao ambayo hata tukiyataja hatuwezi kuyamaliza kwa leo.Lakini kwa uchache nitataja yale makuu.

1.Kuitoa Chadema kutoka Chama kidogo kabisa hadi kuwa Chama tishio na mbadala wa Chama Tawala
2.Kutoka wabunge 11 katika bunge lililopita hadi kufikia wabunge 48
3.Kuwa Chama kikuu Rasmi cha Upinzani nchini.
4.Kuwa Chama tulivu na kisicho na migogoro ya kipuuzi.
5.Kuwa msemaji na kimbilio la watanzania
6.Kuongoza operesheni mbalimbali nchini zilizoingiza maelfu ya wanachama na kufungua matawi kote nchini
7.Kukuza mapato ya Chadema kwa njia mbalimbali
8.Kujenga ngome yake kuu kwa wasomi hususani katika vyuo vikuu.
9.Kujenga demokrasia ndani ya chama
10.Kufuta kabisa ule usemi kwamba vyama vya upinzani ni vyama vya msimu.

Maadui wa Chadema wanatakaje?

Katika uchunguzi wangu nimegundua kitu kimoja.Kwamba wale wote wasioitakia mema Chadema wanaamini njia pekee ya kukimaliza chama hicho ni kuwatenganisha viongozi hao wawili.Mtu mmoja alinipa mfano jinsi ilivyokuwa rahisi kuisambaratisha NCCR kutokana na tofauti za viongozi wake wakuu.Imekuwa ni rahisi zaidi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko kuivuruga Chadema chini ya Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

Ni ukweli kwamba Freeman Mbowe mwanasiasa na mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa hapenyeki kirahisi.Kwanza maadui wengi wanapenda kutumia pesa kurubuni watu, sasa Freeman mtamnunua kwa bei gani? Hali kadhalika Dr Wilbroad Slaa msomi aliyebobea na kulingana na falsafa,hulka na itikadi yake amekuwa injini kuu ya chadema kwa nafasi yake ya Katibu mkuu ambapo ndiye mtendaji mkuu na msimamizi mkuu wa shughuli za siku kwa siku za chama.Sasa kwa hali hii na kwa vyovyote vile maadui wa chama hiki wasingependa umoja wa viongozi hawa wawili.


Changamoto zao.

Penye mafanikio hapakosi changamoto.Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya bado viongozi hawa wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kufungua matawi ya wanachama hadi kwenye mashina.Si vibaya wakatumia mfumo wa washindani wao wakuu CCM ambao wana utaraibu wa uongozi unaojulikana kama balozi wa nyumba kumi.

Njia hii imeisaidia sana CCM hasa nyakati za uchaguzi.Changamoto nyingine ni kuwa na ofisi kubwa na ya kisasa ya makao makuu inayoendana na hadhi ya chama hicho. Mwisho viongozi hawa wanatakiwa waandae program ya kuwapata wanachama wenye sifa na wanaofaa kugombea nafasi za serikali za mitaa,udiwani na ubunge.Chadema waachane na mfumo wa zima moto wa kupata wagombea.


Mwisho
Kama nilivyoeleza juu viongozi hawa wawili Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamekuwa ni nguzo kuu ya chama hiki.Hapa Chadema kilipofikia kipo kwenye hatua ya mwisho yenye uwezekano wa kukamata dola 2015 kwa njia ya kura. Ni wazi hapa ndipo panapohitajika uwajibikaji na ushirikiano wa hali ya juu.Ningelikuwa mwanachama wa Chadema ningehakikisha katika uchaguzi wa ndani wa chama majabali hawa wawili hawaguswi. Wabaki kama walivyo. Wakamilishe kazi waliyoianza ambayo ni kukamata dola.Kisha baada ya hapo historia itakuwa imeandikwa.

WanaJF Karibuni kwa mjadala!
 
zetu juhudi 2015 tuungane kwa pamoja nguvu na mshikamano kukamata nafasi mbalimbali
 
Nakubaliana na wewe kwamba ni kwa mtazamo wako!
Na si mtazamo tu bali hata na "IMANI" yako ndivyo ilivyo kwake!
Mimi naamini kazi ya ZZK huku CHADEMA,...
Swali ni je, kuna nini hadi CCM wafurahie kazi ya kuimarika kwa upinzani?!
Haya ni mapenzi ya PAKA kwa PANYA
mkuu umenena,kwan zitto n kiongoz chdm sasa magamba wana maslahi gan naye mpaka washabikie yale anayo yafanya? Ndiyo maana tunasema magamba hawakuzichanga vzuri karata zao kwenye hili.
 
Back
Top Bottom