Ndugu WanaJF
Uncle amekuwa anatafuna mdada wa kazi kwa jirani, mara wenye nyumba wanapokuwa hawapo huku mdada mwingine wa kazi akishuhudia vitendo vile. Kweli za mwizi ni 39, ya 40 sasa imewadia. Wenye nyumba wakasafiri kwa muda wa wiki moja, uncle akaendeleza kamchezo kake bila kuhofia mdada mwingine wa kazi. Kipindi hiki, akaamua kumtafunia mdada wa watu nyumbani anakofanya kazi. Kibaya, akawa anamtafunia kitandani kwa watoto wao wa kike, ambao wamesafiri nao.
Wenye nyumba waliporudi, yule mdada mwingine akaamua kusema yote kwa wazazi. Wazazi wakawaita baadhi ya wazee na majirani. Wakamuita na uncle pia. Uncle na yule mdada wa kazi wakawekwa kiti moto kweli kweli. Uncle na mdada ikabidi wakiri kuwa wamekuwa wakitafunana kwenye chumba wa watoto na wakati mwingine sebureni.
Wazee, majirani na wazazi wakaamua uncle amuoe yule mdada wa kazi, na mdada wa kazi akiridhia chapchap! Uncle hakuwa na ujanja, akaandikishwa barua ya makubaliano akatia sahihi na yule mdada akasaini pia, na mashahidi wote. Mdada wa kazi akapaki mizigo yake na kuongozana na uncle hadi nyumbani kwa uncle. Uncle anasoma chuo kikuu na bado anaishi na wazazi wake. Bahati, wazazi wa uncle wamesafiri ila wanarudi wiki ijayo. Uncle amemuoa yule mdada hii ni siku ya tano!
Wazazi wameishaambiwa juu ya mkasa huu, ila wako kimyaaaa. Uncle amechanganyikiwa...sana sana! Sasa anaomba nimpatie ushauri, ebu nipeni mawazo ili nimsaidie uncle...........