Uncle ameozwa kwa mdada wa kazi: Anataka nimshauri

Yakuza

Senior Member
May 22, 2011
114
43
Ndugu WanaJF

Uncle amekuwa anatafuna mdada wa kazi kwa jirani, mara wenye nyumba wanapokuwa hawapo huku mdada mwingine wa kazi akishuhudia vitendo vile. Kweli za mwizi ni 39, ya 40 sasa imewadia. Wenye nyumba wakasafiri kwa muda wa wiki moja, uncle akaendeleza kamchezo kake bila kuhofia mdada mwingine wa kazi. Kipindi hiki, akaamua kumtafunia mdada wa watu nyumbani anakofanya kazi. Kibaya, akawa anamtafunia kitandani kwa watoto wao wa kike, ambao wamesafiri nao.

Wenye nyumba waliporudi, yule mdada mwingine akaamua kusema yote kwa wazazi. Wazazi wakawaita baadhi ya wazee na majirani. Wakamuita na uncle pia. Uncle na yule mdada wa kazi wakawekwa kiti moto kweli kweli. Uncle na mdada ikabidi wakiri kuwa wamekuwa wakitafunana kwenye chumba wa watoto na wakati mwingine sebureni.

Wazee, majirani na wazazi wakaamua uncle amuoe yule mdada wa kazi, na mdada wa kazi akiridhia chapchap! Uncle hakuwa na ujanja, akaandikishwa barua ya makubaliano akatia sahihi na yule mdada akasaini pia, na mashahidi wote. Mdada wa kazi akapaki mizigo yake na kuongozana na uncle hadi nyumbani kwa uncle. Uncle anasoma chuo kikuu na bado anaishi na wazazi wake. Bahati, wazazi wa uncle wamesafiri ila wanarudi wiki ijayo. Uncle amemuoa yule mdada hii ni siku ya tano!

Wazazi wameishaambiwa juu ya mkasa huu, ila wako kimyaaaa. Uncle amechanganyikiwa...sana sana! Sasa anaomba nimpatie ushauri, ebu nipeni mawazo ili nimsaidie uncle...........
 
wacha uncle aendelee kula raha!!hakuna ushauri wa ziada zaidi ya kumsisitizia awe mwaminifu katika ndoa yake!!!
 
IHrKtX2DvWeC1W1IPgKIVDJOUhBIRQUEKEUAGnGIJcev5QGI7DCOLxLjGWJM0GQ9zwEgZyev8vJSv3vWb8ehMAAAAASUVORK5CYII=
lakini na wewe haka ka avatar kako hakampi shida huyo uncle wako kweli??una bahati uncle kaozeshwa!!!
 
Kwani Uncle alipo kua anafanya mapenzi na huyu mfanyakazi hakujua kama anafanya kosa au hakutaka kujua matokeo? mwambie uncle keshalikoroga alinywe tuu japo moto...
 
Kila kitu hutokea kwa sababu maalum, uncle wako alipangiwa huyo dada kama mke....kwa akili ya kawaida na usomi wake yawezekana akawa anaona hawezi kuwa na house girl....Binafsi, namshauri atafute nyumba/chumba wapange waendelee na maisha yao kama mke na mume....Zali la mentali kwa housegirl....Big Up girl!
 
Kila kitu hutokea kwa sababu maalum, uncle wako alipangiwa huyo dada kama mke....kwa akili ya kawaida na usomi wake yawezekana akawa anaona hawezi kuwa na house girl....Binafsi, namshauri atafute nyumba/chumba wapange waendelee na maisha yao kama mke na mume....Zali la mentali kwa housegirl....Big Up girl!

Michelle

Umesema kweli. Kwa vyovyote wazazi wake watamtaka aondoke pale nyumbani, hivyo uncle atafute chumba aendelee na maisha. Yote maisha!
 
pole kwa uncle cz najua huyo mke hawez kuwa mtamu tena kama alivyokuwa housegirl cha muhim awe anamvizia tena wazazi wake wasipokuwepo atapata utamu uleule wa mwanzo
 
Uncle anapanga kumfukuza kwa nguvu huyo mdada wa kazi (mke wake), wakati aliisha jicommit kwa maandishi. Hivi kisheria inawezekana? Mdada wa kazi au wazazi wa kule alikokuwa mwanzo wanaweza kumshitaki popote?


Uncle bwana......., yamemfika shingoni......Wala sitanii hii ni kweli imetokea juzi juzi....na game linaendelea....Huu mwaka 2012 inaonesha utakuwa na vituko na maajabu! Ukiachana na misiba ya marafiki zetu na pengine sisi pia!
 
uncle anapanga kumfukuza kwa nguvu huyo mdada wa kazi (mke wake), wakati aliisha jicommit kwa maandishi. Hivi kisheria inawezekana? Mdada wa kazi au wazazi wa kule alikokuwa mwanzo wanaweza kumshitaki popote?


Uncle bwana......., yamemfika shingoni......wala sitanii hii ni kweli imetokea juzi juzi....na game linaendelea....huu mwaka 2012 inaonesha utakuwa na vituko na maajabu! Ukiachana na misiba ya marafiki zetu na pengine sisi pia!

uncle wako anapaswa kuwajibika!
 
Wamemkomesha, na bado mziki ndio unaanza. Subutu yake amfukuze! Sizitaki mbichi hizi? Wakati anazirukia hakuziona mbichi. Adabu hana wala heshima. Ghrrrrrrrr!
 
mwambie uncle nampa hongera sana ila ajitahidi tu kum2nza mkewe huyo maana amempata bila hata mahali,ameiba weeeeeeeeee sasa wamempa bure ndo anataka kumfukuza?analo hilooooooooooo!
 
Anapanga kuwatumia wazazi wake wamkatae huyo mdada kisha atumie kigezo hicho kumtimulia mbali........

Hivi, akifanya hivyo ni uungwana kweli? Mdada wa watu anaweza kuwa tayari ana mimba au ukimwi au vyote viwili. Lakini pia, kamsababishia kupoteza kazi yake na anaweza kumpelekea kurudi kijijini........akiwa tayari ameharibikiwa!!!!

Sheria inasemaje kwa mtu kama uncle? Mimi kama mdada kitendo hichi kinaniuma japo ni uncle!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom