.............mie hutumia papers nyingi sana ! kwanza napanga papers ktk shimo, kisha sehemu ya kukalia, halafu naendelea. However naenjoy sana cha kuchuchumaa !
though sio njia ya kujikinga na bacteria infections sasa utaweza kufanya mlolongo wote huo wa kupanga karatasi iwapo hujabanwa na haja kwa ukali hasa uharo sijui kama unaweza weka hata karatasi moja looh!
usaatarbu wa hivi vyoo wanauweza wadhungu wenyewe coz mtumiaji akimaliza anasafisha na kumruhusu mtumiaji mwingine akute mazingira safi, kwa bongo imeshindikana japo utakuta baadhi ya kumbi na hoteli wameajiri mtu wa kukaa chooni ukitoka tuu anaingia kusafisha kabla mwingine hajaingia coz utakuta mwingine anakanyaga na miguu pale pa kukalia.
Kuna wengine hawana aibu hasa vya maofisini waweza pishana na mtu katoka mlango wa choo mtanashati ananukia ukiingia na kukuta jinsi alivyokiacha choo looh haja yako yote inarudi ndani.
Vyoo vya kukaa mkiwa watumiaji ni wastaarabu vinafaa hata kwenye public shida kila mtu anakuwa na kinyaa na akimaliza koz kakikuta kichafu anaacha kichafu.
KITUKO: kunawannandoa fulani baada ya kuoana walifunga mlango wa choo cha master na kuacha kukitumia kwa sababu ya kutegeana kukisafisha, ilikuwa hivi, mke akiingia anasafisha kabla ya kutumia na baada ya kutumia. Mume akiingia anatumia na kukiacha kichafu bila hata kuflash ilhali maji yapo. Hali hii iliendelea na mke akalalamika kwamba basi hata kuflash nyee yako ili mie niwe nasafisha tuu usafi mwingine mume wala hakurekebishika. Ikafika mahali mke nae akazira kusafisha wakawa wanatumia nyee juu ya nyee hadi ikafika mahali huwezi hata kuingia kuoga ikabidi wakifunge na watumie cha public amabcho anasafisha housegirl.
So usafi wa vyoo vya kukaa ni ustaarabu wa mtumiaji na usafi, wote mkiwa hivi hata kama ni nyumba nzima ya watu 10 kila ukiingia chooni waweza lala au kusinzia huku wadondosha nyee looh