Unawezaje kutambua kuwa ni mchawi?

Unawezaje kutambua kuwa ni mchawi?

Asante mkuu[emoji120]
Baada ya kujiunga humu Jf na kukutana na mada hizi za meditation nimekuwa nikijaribu jaribu mara kadhaa japo nashindwa kuzingatia mawazo yanahama hama sana,
Nilijaribu pia kusoma habari ya Mantra kwenye google nikaambiwa inasaidia Ku count down mawazo na kubakia na empty mind, ila bado sijajaribu, hasa wanaisifia ile ya "Om...."
Hivi Nikweli Mantra inasaidia Ku calm mind hasa kwa biginners ?
Sawa kabisa .. Na mawazo kuhamahama ni hatua ya awali ukiendelea uta master kumonitor na kuyadhibiti
Mantras ni muhimu sana kwenye spiritual awakening

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una nguvu nzuri kweli
Fanya anayokushauri mshana ukafungue kanisa ujipatie kipato

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
Mkuu bintishomvi nashukuru kwa mchango wako wa fikra, lakini bahati mbaya Mimi sina wazo la kuanzia kanisa hata nikifanikiwa kumaster hizo nguvu, Lengo na kiu yangu kubwa ni kujitambua/ kupata Ufahamu
wa Ulimwengu
 
sio uchawi lakini huo ndugu,
Nguvu alizonazo kila mtu wala sio uchawi huo
Its free power everyone have, ungefundisha tu namna kila mtu anavyoweza kuzitumia
your devil and god dwell within yourself, niwewe kuamua kuwa mwema au mbaya
 
Jitambue ikiwa umezaliwa ukiwa na uwezo au nguvu za kichawi ndani yako ambazo unafree will nazo kutozitumia au kuzitumia kwa mazuri(chanya) au mabaya(hasi), kazi ni kwako;

1.Una imani thabiti juu ya kuwajibika juu ya matendo yako au unabeba kinachokukumba kama sehemu ya kukosea,kujiadhibu au kupatia kwako pasipo kulahumu au kutwisha misalaba wengine.

2.Unajisikia vizuri sana ukiwa katika mazingira ya asili au kuishi katika mazingira ya nyumbani ambayo yana uoto na mazingira matulivu ya asili.

3. Unaweza kuhisi au kukisia nguvu hasi au chanya toka kwa wengine (ni kama kipawa usichoweza kukielezea kwanini unafanya hivyo) Mara nyingi unajikuta ni mtu mwenye tahadhari sana.

4.Unaweza kuwa pia na uwezo wa kuponesha au kutibu wagonjwa kiasili,kushauri kitabibu pasipo kusomea au kwa kukadiria tiba na ikawa au pengine wapenda sana masuala ya kutafiti mitishamba n.k na unapofanya hivyo unafurahia kweli toka moyoni.

5. Unajisikia tofauti au unawaza tofauti na watu wa rika lako na mara nyingi ukuwia vigumu kuchangamana nao au upendi vikundi "hiki kitendo kimedumu kwa muda mrefu maishani mwako japo si mara zote" na unakuwa na hisia kuwa umekuwa hivyo tokea hata ujajitambua ni lini hasa ulianza kujitofautisha.

6.Una ukarimu usiyo wa kawaida, una moyo wa kusaidia au kujitoa japo mara kadhaa umetendwa au kufanyiwa ndivyo sivyo lakini unaendelea kujitoa kusaidia wengine au kuufungulia moyo wako dunia.

7. Unajihisi unamuunganiko imara na utukufu, idea ya Mungu kuwa ni kiumbe pekee katika fikra zako unaona ni vyema kama ikielezewa kuwa ni nguvu ijumuishayo hali ya kiume na kike kwa pamoja iendayo na kutoka pia kuzunguka kila kiumbe na kila kitu.

8. Unataka au unapenda mno kujifunza bila mipaka hasa mambo ya sirini au yasiyo marahisi kuchunguzika na unachotaka ni kujitambua au kujiweka huru kifkra.

9.Una hisia nzito ya huruma na kuheshimu wanyama na mazingira yao mara nyingi ujisikii vizuri ukiona uharibifu wowote wa mazingira au mauaji/ukatili kwa viumbe hai.

10. Unajikuta wakati mwingi ukifurahia kulitizama anga nakustaajabia nyota, jua, mwezi n.k na unahisi kuna muunganiko fulani usioelezeka baina yako na vitu hivyo, unajaribu kudadisi nakutaka kujua mengi kuhusu mizunguko,uwepo na nguvu zake.

11.Unajikuta mara kadhaa ukijaribu kuunda au kujaribu kufanya uchawi pasipo kukusudia au kung'amua.

12. Waamini kuwa miujiza ni nguvu za ukweli, ambazo zinaweza kutumiwa kwa mazuri au mabaya itategemea na namna mtendaji wa miujiza hiyo atakavyoamua kuitumia.

13.Unaamini katika nguvu za kiakili (psychic power),mfano:-
*Claivoryance(uwezo wa kupata jumbe mbalimbali kupitia akili pasipo kuambiwa)

*Cleiraudience(uwezo wa kusikia sauti mbalimbali kupitia akili)

*Clairsentience(uwezo wa kuweza kuhisi nakujua pasipo kuona au kuambiwa) pia kuamini katika uwepo wa;

*Aura reading(hisia inayomzunguka kiumbe au kitu katika muundo wa rangi)

*Psychometry(uwezo wa kugundua ukweli kuhusu tukio au mtu kupitia kugusa kitu chenye mahusiano nacho)

*Telekinesis"mjongeo" au psychokinesis "nafsi" (ni uwezo wa mtu kuathiri mfumo halisi(kifizikia) bila ya kutangamana na uhalisia wenyewe) Mfano kutumia fikra kusogeza au kuvuta kitu n.k

*Preternatural(kufanya jambo nje ya uwezo wa kawaida au asili)

*Supernatural(uwepo wa nguvu isiyoweza elezeka kisayansi au kwa sheria za uhalisia(laws of nature))

*Divination(kitendo cha kutafuta maarifa ya mambo au hatima ya baadae au kupitia nguvu za supernatural)
Je baada ya kujitambua kua ni mchawi vipi ntaweza kuutumia
 
Natamani hii Mada iendelee nizidi kujifunza. Kuna nguvu fulani ninayo huwa nashindwa kuielezea kinaga ubaga. Naweza Pata wazo au jambo yaani linakuja ghafla, kama ni kitu kibaya nikakikemea huwa hakitokei, ila nikipuuza huwa kinatokea. Jambo hili huwa linabitatiza Sana kwa kweli. NA pia kama ni jambo jema niliafiki huwa napata. Nisipoafiki huwa sipati.

Msaada fatadhali
ni kweli ata mm mungu kanipa uwezo wa kucomand ubongo kwa kumsababishi a mtu apate mabaya au mazur na naweza kuipanga future yangu na ikaja vile nataka ibelieve kila mtu analokarama ilo na ukitaka kulifungua basi jaribu sana kucheza na ubongo wako ndo wenye siri yko
 
Roho ikifungwa kamwe haiwezi kufanya makubwa...

Nipo kifungoni nimelitambua hili 2015. Nahangaika kujitoa humu kwa msaada wa wataalamu wa mambo ya kiroho. Sipo mbali na geti la gereza hili. Utumwa na kuishi kama roboti sasa unaenda kutamatika
.
 
Napenda kujitambua niwe na hiyo inayoitwa free will...

Napenda kusoma historia za kale nafurahi kuzisikia, napenda sana kusoma habari za roho kuujua ulimwengu wa roho.
 
Achana na stori za kwenye muvi, nguvu hizi ni za asili na utegemea sana uwezo wa afya yako ya akili na katu haziamishiki unabaki kuwa nazo tu sema usipozitumia ipasavyo au unapoziathiri au kuzipotezea ubaki kama hazipo mpaka pale mazingira yanayosababisha nguvu hiyo kufanya kazi yatakaporejeshwa/kujirudi.
Safi
Sahihi kabisa
 
Badala kuwavuta watu upotevuni ungeweza kuanzisha mada kama; Je unapenda kuurithi uzima wa milele
 
Ndio mimi ni mchawi kwa asilimia 100
Mkuu, nitawez aje kumaliza Nguvu ya uchawi iliyo wekwa na mchawi kwenye mwili wangu, nasema hivi Kuna dingi mmoja alikua mchawi Sasa kunasiku nitofautiana Naye akaniambia kitakacho kupata huta sahau maishani mwako zilipita siku3 nkapata ajali Sasa chakushangaza nakua kama napata nafuu gafla ilenguvu ya kupona inapotea ni miaka Sasa imepita
 
Mkuu, nitawez aje kumaliza Nguvu ya uchawi iliyo wekwa na mchawi kwenye mwili wangu, nasema hivi Kuna dingi mmoja alikua mchawi Sasa kunasiku nitofautiana Naye akaniambia kitakacho kupata huta sahau maishani mwako zilipita siku3 nkapata ajali Sasa chakushangaza nakua kama napata nafuu gafla ilenguvu ya kupona inapotea ni miaka Sasa imepita
Mmh nipe muda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom