Unawezaje kutambua kuwa ni mchawi?

Unawezaje kutambua kuwa ni mchawi?

Daah, kwenye namba 6 najiona kabisa mimi kila kitu. Ila changamoto niliyo nayo saivi nimefulia mbaya, huwa natamani sana nisaidie wengine ila uwezo sasa ni shida. Nifanyeje wadau?🥲🥲
 
Hizi ni ngumu za kawaida kabisa kwa binadamu..

Binafsi kitu kibaya kikiwa kinajiandaa kunitokea uwaga naota vile vile kitakavyotokea siku mbili kabla yaani km hatari inatokea kesho kutwa,leo nAota na kesho naota hlf kesho kutwa inatokea kama nilivyoota...

Pili,naweza mjua mtu mbaya kwa mda mchache sana nitakAokuwa nae automatically

Naangalia video youtube hlf Najua kbs atasema maneno flani na kweli anayasema baadhi

Namuwaza mtu then ananipigia mda huo huo

Naangalia simu hlf mda huo huo inapigwa

Wachawi nawaota kwa sura zao halisi

Damu yangu inakataaga watu hlf badae nakujagundua hawana jema
 
Naomba na mimi nisaidie kwenye hiliii
1/kuna siku nimekaa baa moja pale zakheem mbele yangu amekaa jamaa moja mimii nikawa naona ndani ya shati kuna vitu vinamtembea kama nyoka,nikamkazia macho akasimama akenda chooni nikamuuliza jirani yake akasema haoni kurudi akaniita nikasimama nikaondoka
2/wiki kama mbili nimepita dukani kwa muha nikamkuta jamaa kama kama mipete flani siijui amekaa analitizama duka la muha sijui ilikuaje nywele zikasisimuka nikamkazia macho nikaona kitu kama panya yumo ndani ya shati lake kila ninapo mkazia macho yule kiumbe kama analazimisha kutoka jamaa anambana asitoke ni mimi na yeye ndio tulikuwa tunajua kinachoendelea maana watu walikuwa wanapita mwisho wa siku akasimama akaondoka
Nb: juzi imetokea hali kama hiyo pia jamaa nikamfuata nikamwambia acha unachokifanya hapa la sivo napiga kelele kukujazia watu akakimbia

Hii hali husababishwa na ninii hasa maana kila nae mwelezq hanielewii[emoji17]
 
Je, Inawezekana mtu mwingine (mtaalam) kukuibia/ kukuchukulia physic power zako kwa kutumia Nguvu zake, ukabakia jina kitu?
Msaada waalimu Mshana Jr Undava King Mr. Purpose
Achana na stori za kwenye muvi, nguvu hizi ni za asili na utegemea sana uwezo wa afya yako ya akili na katu haziamishiki unabaki kuwa nazo tu sema usipozitumia ipasavyo au unapoziathiri au kuzipotezea ubaki kama hazipo mpaka pale mazingira yanayosababisha nguvu hiyo kufanya kazi yatakaporejeshwa/kujirudi.
 
Naomba na mimi nisaidie kwenye hiliii
1/kuna siku nimekaa baa moja pale zakheem mbele yangu amekaa jamaa moja mimii nikawa naona ndani ya shati kuna vitu vinamtembea kama nyoka,nikamkazia macho akasimama akenda chooni nikamuuliza jirani yake akasema haoni kurudi akaniita nikasimama nikaondoka
2/wiki kama mbili nimepita dukani kwa muha nikamkuta jamaa kama kama mipete flani siijui amekaa analitizama duka la muha sijui ilikuaje nywele zikasisimuka nikamkazia macho nikaona kitu kama panya yumo ndani ya shati lake kila ninapo mkazia macho yule kiumbe kama analazimisha kutoka jamaa anambana asitoke ni mimi na yeye ndio tulikuwa tunajua kinachoendelea maana watu walikuwa wanapita mwisho wa siku akasimama akaondoka
Nb: juzi imetokea hali kama hiyo pia jamaa nikamfuata nikamwambia acha unachokifanya hapa la sivo napiga kelele kukujazia watu akakimbia

Hii hali husababishwa na ninii hasa maana kila nae mwelezq hanielewii[emoji17]
Kama ni kweli unachosema basi huna sababu yeyote ya kueleza watu hili wakuelewe kwa maana hawatakuelewa wala kukuamini cha zaidi ipo siku raia watakudhuru kwa kuamini wewe ndo mbaya wao/chizi na unaowaumbua nao pia wataitaji kwa namna yeyote ile wakudhuru.

Nguvu ulizo nazo zitumie kwa hekima kubwa na kwa utulivu hivyo zitumike kwa manufaa kusaidia waliopo hatarini kudhuriwa na watu wabaya pale tu penye ulazima na pasipo na ulazima piga kimya jali muda wako kwa maana wabaya ni wengi na katu dunia haiwezi badilika.
 
Hizi ni ngumu za kawaida kabisa kwa binadamu..

Binafsi kitu kibaya kikiwa kinajiandaa kunitokea uwaga naota vile vile kitakavyotokea siku mbili kabla yaani km hatari inatokea kesho kutwa,leo nAota na kesho naota hlf kesho kutwa inatokea kama nilivyoota...

Pili,naweza mjua mtu mbaya kwa mda mchache sana nitakAokuwa nae automatically

Naangalia video youtube hlf Najua kbs atasema maneno flani na kweli anayasema baadhi

Namuwaza mtu then ananipigia mda huo huo

Naangalia simu hlf mda huo huo inapigwa

Wachawi nawaota kwa sura zao halisi

Damu yangu inakataaga watu hlf badae nakujagundua hawana jema
Viashirio moja wapo vya mwanzo kuwa unazo nguvu ambazo hazijaendelezwa/kufanyiwa kazi kuleta matokeo halisi.
 
Hizo zoote unalizozitaja nimeshaziangalia muda sana mkuu lord of the rings nimecheki hadi spin-off yake inaitwa "the hobbit" kikubwa ile muvi ina concept tofauti sana ya uchawi mtunzi wa norvel zake late mr j.j.tolkien alijaribu kuchukua baadhi ya concept kwenye abramaic religions hasa christianity japo alipinga hili ila inaonekana dhahiri kwenye kitabu na movie .

Any tukiachana na hayo , nilichokuwa namaanisha ni kuwa hakuna mtu anazaliwa na nguvu za kichawi mkuu hayo mambo yalikuwa zamani enzi za mitume maana wao ndo walipewa maajabu na Mwenyezi mungu ili kuweza kuwaaminisha wale wasioamini kwa maneno.

Refer musa maajabu aliyofanya ,refer yusufu alivyokuwa anatabiri ndoto perfectly refer suleiman ukisoma babylonian talmud na pia quran imemuelezea jinis alivyoweza kutawala majini na upepo pia viumbe wengi tu hii ni kwa uwezo wa mungu n.k

Sasa kwanini nimekataa kuwa hakuna anyezaliwa na haya uchawi ? Tukiangalia abrahmaic religion zote zinakubali kuwa kuna majini/mashetani/mapepo wachafu pamoja na malaika (malaika wana maajabu mengi waliyojaliwa na Wenyezi mungu )
Hawa viumbe wote wameumbwa na Mungu . na pia majini pia wana abilities tofauti walizopewa na mungu na walikuwepo duniani kabla ya adamu.

Sasa inakuwaje mtu anakuwa mchawi? Ni pale anapoweka mkataba na hawa majini kwamba atayatumikia kutokana na masharti yao kisha yenyewe yatamsaidia kwenye mambo mengi mno ya maajabu mfano ni majini wana uwezo wa kwenda umbali mrefu kwa kutumia muda mchache mnooo yaani anaweza kutoka Tanzania hadi urusi kwa sekunde au dakika n.k hii ndo jinsi walivyoumbwa .

Hapa ndipo tunapata waganga na wachawi woote wana mikataba na majini ili yawasaidie kwenye mambo yao na hao ambai unakuta wana hisia hizo alizotaja mtoa mada ujue wana majini ndani ya miili yao either kwa kujua au kwa kutokujua na ndo huwa yana mfanya ahisi hayo aliyoongelea mtoa mada.

Usibishe na wala kufikiri hao waliokuwa na nguvu hizo wakaitwa mitume au manabii hivi sasa hawazaliwi nakuhakikishia ni kweli kabisa kuwa nguvu hizo zipo na wenye nazo ni wengi pia japo wanaozitumia mpaka kufikia kiwango cha juu cha matumizi yake nakuacha alama katika kizazi hiki ni wachache mno. Mimi ni mmoja wao mwenye hizo nguvu na sijihusishi na ulichokiandika hapo juu.

Kwenye muvi unachokiangalia ni ubunifu tu na mautundu ya mtunzi kunogesha au kutia manjonjo stori iwe interesting kwa mtazamaji ila siyo kila kilichooneshwa katika filamu hizo ndiyo ukweli wa mambo juu ya psychic powers.
 
Enhee tukianza na wewe una power gani?
 
Achana na stori za kwenye muvi, nguvu hizi ni za asili na utegemea sana uwezo wa afya yako ya akili na katu haziamishiki unabaki kuwa nazo tu sema usipozitumia ipasavyo au unapoziathiri au kuzipotezea ubaki kama hazipo mpaka pale mazingira yanayosababisha nguvu hiyo kufanya kazi yatakaporejeshwa/kujirudi.
Asante Mkuu Undava King hekima yako inazidi kunifungua ufahamu. Mungu akubariki Sana[emoji120]
 
Jitambue ikiwa umezaliwa ukiwa na uwezo au nguvu za kichawi ndani yako ambazo unafree will nazo kutozitumia au kuzitumia kwa mazuri(chanya) au mabaya(hasi), kazi ni kwako;

1.Una imani thabiti juu ya kuwajibika juu ya matendo yako au unabeba kinachokukumba kama sehemu ya kukosea,kujiadhibu au kupatia kwako pasipo kulahumu au kutwisha misalaba wengine.

2.Unajisikia vizuri sana ukiwa katika mazingira ya asili au kuishi katika mazingira ya nyumbani ambayo yana uoto na mazingira matulivu ya asili.

3. Unaweza kuhisi au kukisia nguvu hasi au chanya toka kwa wengine (ni kama kipawa usichoweza kukielezea kwanini unafanya hivyo) Mara nyingi unajikuta ni mtu mwenye tahadhari sana.

4.Unaweza kuwa pia na uwezo wa kuponesha au kutibu wagonjwa kiasili,kushauri kitabibu pasipo kusomea au kwa kukadiria tiba na ikawa au pengine wapenda sana masuala ya kutafiti mitishamba n.k na unapofanya hivyo unafurahia kweli toka moyoni.

5. Unajisikia tofauti au unawaza tofauti na watu wa rika lako na mara nyingi ukuwia vigumu kuchangamana nao au upendi vikundi "hiki kitendo kimedumu kwa muda mrefu maishani mwako japo si mara zote" na unakuwa na hisia kuwa umekuwa hivyo tokea hata ujajitambua ni lini hasa ulianza kujitofautisha.

6.Una ukarimu usiyo wa kawaida, una moyo wa kusaidia au kujitoa japo mara kadhaa umetendwa au kufanyiwa ndivyo sivyo lakini unaendelea kujitoa kusaidia wengine au kuufungulia moyo wako dunia.

7. Unajihisi unamuunganiko imara na utukufu, idea ya Mungu kuwa ni kiumbe pekee katika fikra zako unaona ni vyema kama ikielezewa kuwa ni nguvu ijumuishayo hali ya kiume na kike kwa pamoja iendayo na kutoka pia kuzunguka kila kiumbe na kila kitu.

8. Unataka au unapenda mno kujifunza bila mipaka hasa mambo ya sirini au yasiyo marahisi kuchunguzika na unachotaka ni kujitambua au kujiweka huru kifkra.

9.Una hisia nzito ya huruma na kuheshimu wanyama na mazingira yao mara nyingi ujisikii vizuri ukiona uharibifu wowote wa mazingira au mauaji/ukatili kwa viumbe hai.

10. Unajikuta wakati mwingi ukifurahia kulitizama anga nakustaajabia nyota, jua, mwezi n.k na unahisi kuna muunganiko fulani usioelezeka baina yako na vitu hivyo, unajaribu kudadisi nakutaka kujua mengi kuhusu mizunguko,uwepo na nguvu zake.

11.Unajikuta mara kadhaa ukijaribu kuunda au kujaribu kufanya uchawi pasipo kukusudia au kung'amua.

12. Waamini kuwa miujiza ni nguvu za ukweli, ambazo zinaweza kutumiwa kwa mazuri au mabaya itategemea na namna mtendaji wa miujiza hiyo atakavyoamua kuitumia.

13.Unaamini katika nguvu za kiakili (psychic power),mfano:-
*Claivoryance(uwezo wa kupata jumbe mbalimbali kupitia akili pasipo kuambiwa)

*Cleiraudience(uwezo wa kusikia sauti mbalimbali kupitia akili)

*Clairsentience(uwezo wa kuweza kuhisi nakujua pasipo kuona au kuambiwa) pia kuamini katika uwepo wa;

*Aura reading(hisia inayomzunguka kiumbe au kitu katika muundo wa rangi)

*Psychometry(uwezo wa kugundua ukweli kuhusu tukio au mtu kupitia kugusa kitu chenye mahusiano nacho)

*Telekinesis"mjongeo" au psychokinesis "nafsi" (ni uwezo wa mtu kuathiri mfumo halisi(kifizikia) bila ya kutangamana na uhalisia wenyewe) Mfano kutumia fikra kusogeza au kuvuta kitu n.k

*Preternatural(kufanya jambo nje ya uwezo wa kawaida au asili)

*Supernatural(uwepo wa nguvu isiyoweza elezeka kisayansi au kwa sheria za uhalisia(laws of nature))

*Divination(kitendo cha kutafuta maarifa ya mambo au hatima ya baadae au kupitia nguvu za supernatural)
Hivi kuponyesha watu kutumia dawa za mitishamba ni uchawi?
 
Binafsi nina nguvu flani ndani yangu ambayo sijaijua ni nguvu gani. Kuna wakati naweza kukaa nikawaza kitu flani na sio kwamba nimelala nakuwa macho lakini nawaza, baada ya muda kupita kama wiki, mwezi au siku kadhaa kile kitu nilichokiwaza kinatokea vilevile. Juzi juzi tu hapa nimekaa hapa Ofisini kwetu nikasikia kama kitu kinaniambia nikee roho ya mauti ofisini kwetu, nikawahadithia wenzangu kwamba kuna sauti imeniambia hivi, wakasema tu inabidi ukemee na ukiangalia kumetokea misiba zaidi ya saba kwa mwaka huu mmoja ukiwa wa staff mwenzetu na mwingine wa watu wa karibu na staff wetu wakiwemo wadada wawili wa hapa ofisini kuharibikiwa mimba kubwa tu. Pia kuna wakati naota napambana na wachawi sana nakemea mpaka mume wangu ananiamsha anasema mbona unakemea kuna nini? namhadithia kilichotokea. Hata kama ni mtu nilimuwaza atakuja ataniambia kitu flani atakuja mtu yuleyule na nguo zilezile na ataniambia kitu kilekile, pia nikifanya biashara huwa inatoka sana ila si mzingatiaji nabanwa na kazi, nikimsaidia mtu kutoka moyoni haipiti siku mbili napata kama ni hela au safari ya kulipwa hela zaidi ya kile nilichotoa. Je hizi ndizo hizo nguvu unazoziongelea za asili au? Undava, Mshana JR nisaidieni tafadhali.
 
Mkuu naomba unisaidie hapa, Wiki moja iliyopita nimefiwa na mdogo wangu (anaenifata kuzaliwa), nakumbuka kama miezi miwili nyuma iliyopita siku moja nilimuota (kwenye ndoto) kuwa amefariki, nilipoamka nilishtuka lakini nilipomuangalia alikuwa ni mzima hana Dalili mbaya ya kuugua nikaipuuzia ndoto ile, kipindi hiki imetokea ameugua na kuzidiwa ghafla na kufariki ndio nimeikumbuka ile ndoto yangu niloiota.

Tukio lingine miaka mitano iliyopita nilimpoteza (nilifiwa) baba yangu mzazi, nakumbuka hivyo hivyo miezi michache kabla ya kifo chake nilimuota kua amefariki, nilipoamka nilikuwa na mawazo Sana juu ya ndoto hiyo, nakumbuka nilikwenda kumuangalia kama ni mzima au anaumwa nikamkuta ni mzima. Baadae alipougua na kufariki nikaikumbuka ile ndoto yangu.

Chaajabu/ kinachonishangaza nikuwa jinsi nilivyoliota tukio la msiba, nguo alizozivaa marehemu na mazingira ya tukio ndivyo inavyotokea japo kwa muda mrefu kidogo tangu nilipoota.

Nisaidie mkuu nitakua Nina nini? Kwanini niwe naota tu destiny za watu japo zinatokea kwa muda mrefu, na isiwe naota mambo yao mazuri n.k

Inafikiaga hatua linapotokea najistukia naogopa hata kuwasimulia watu kuwa niliwahi kuota kabla tukio zima lilivyotokea.
Msaada mkuu.

Tukio lingine kuna siku mchana nilikuwa nimejiegesha kwenye kochi sebuleni nikasinzia kutokana na uchovu wa usingizi niliokuwa nao, ghafla nikajikuta nipo kwenye sayari nyingine kabisa nje ya dunia, kwakweli ni ngumu sana kumuelezea mtu akanielewa experience ya mazingira niliyoyashuhudia nilipokuwa kwenye hali hiyo, nilijiona naelea hewani kama puto ila niliweza kwenda maeneo yoyote niliyotaka. Ghafla Kuna mtu aliingia ndani nakuniita kwa Nguvu ili niamke nikale chakula, nilijikuta nimerudi ghafla kwa spidi isiyoelezeka kama kufumba na kufumbua, ila baada ya kuamka nikajikuta kichwani maeneo ya utosini panauma kwa mbali sana (ni kama kimsisimko fulani hivi kilinipata).

Je, hiyo ni nini?

Msaada wakuu Mshana Jr Undava King Mr. Purpose
 
Una nguvu ya astral projection ndani yako, uwezo wa kutambua yajayo kabla hayajafika, pia roho yako ni moja kati ya roho chache zinazoweza kuisafiri dunia bila nguvu kubwa ya meditation....
Ukifanya sana meditation na kujitenga na maisha ya 'material world' unaweza kuwa mkali kuliko manabii wengi kwakuwa tayari una msingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu[emoji120]
Baada ya kujiunga humu Jf na kukutana na mada hizi za meditation nimekuwa nikijaribu jaribu mara kadhaa japo nashindwa kuzingatia mawazo yanahama hama sana,
Nilijaribu pia kusoma habari ya Mantra kwenye google nikaambiwa inasaidia Ku count down mawazo na kubakia na empty mind, ila bado sijajaribu, hasa wanaisifia ile ya "Om...."
Hivi Nikweli Mantra inasaidia Ku calm mind hasa kwa biginners ?
 
Mkuu naomba unisaidie hapa, Wiki moja iliyopita nimefiwa na mdogo wangu (anaenifata kuzaliwa), nakumbuka kama miezi miwili nyuma iliyopita siku moja nilimuota (kwenye ndoto) kuwa amefariki, nilipoamka nilishtuka lakini nilipomuangalia alikuwa ni mzima hana Dalili mbaya ya kuugua nikaipuuzia ndoto ile, kipindi hiki imetokea ameugua na kuzidiwa ghafla na kufariki ndio nimeikumbuka ile ndoto yangu niloiota.

Tukio lingine miaka mitano iliyopita nilimpoteza (nilifiwa) baba yangu mzazi, nakumbuka hivyo hivyo miezi michache kabla ya kifo chake nilimuota kua amefariki, nilipoamka nilikuwa na mawazo Sana juu ya ndoto hiyo, nakumbuka nilikwenda kumuangalia kama ni mzima au anaumwa nikamkuta ni mzima. Baadae alipougua na kufariki nikaikumbuka ile ndoto yangu.

Chaajabu/ kinachonishangaza nikuwa jinsi nilivyoliota tukio la msiba, nguo alizozivaa marehemu na mazingira ya tukio ndivyo inavyotokea japo kwa muda mrefu kidogo tangu nilipoota.

Nisaidie mkuu nitakua Nina nini? Kwanini niwe naota tu destiny za watu japo zinatokea kwa muda mrefu, na isiwe naota mambo yao mazuri n.k

Inafikiaga hatua linapotokea najistukia naogopa hata kuwasimulia watu kuwa niliwahi kuota kabla tukio zima lilivyotokea.
Msaada mkuu.

Tukio lingine kuna siku mchana nilikuwa nimejiegesha kwenye kochi sebuleni nikasinzia kutokana na uchovu wa usingizi niliokuwa nao, ghafla nikajikuta nipo kwenye sayari nyingine kabisa nje ya dunia, kwakweli ni ngumu sana kumuelezea mtu akanielewa experience ya mazingira niliyoyashuhudia nilipokuwa kwenye hali hiyo, nilijiona naelea hewani kama puto ila niliweza kwenda maeneo yoyote niliyotaka. Ghafla Kuna mtu aliingia ndani nakuniita kwa Nguvu ili niamke nikale chakula, nilijikuta nimerudi ghafla kwa spidi isiyoelezeka kama kufumba na kufumbua, ila baada ya kuamka nikajikuta kichwani maeneo ya utosini panauma kwa mbali sana (ni kama kimsisimko fulani hivi kilinipata).

Je, hiyo ni nini?

Msaada wakuu Mshana Jr Undava King Mr. Purpose
Una nguvu nzuri kweli
Fanya anayokushauri mshana ukafungue kanisa ujipatie kipato

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom