Unawezaje kumsamehe aliyekukosea?

Unawezaje kumsamehe aliyekukosea?

Illuminata Rodgers

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2015
Posts
2,845
Reaction score
2,030
Hello JF,

Katika maisha kila binadamu hukosea na aombapo huweza kusamehewa au kutokusamehewa, kwa wale mnaosamehe mnawezaje kufanya hivyo?

Sababu mimi mtu akinikosea kitu ambacho kikanitoa chozi basi huwa sisamehi yani huwa nashindwa kabisa kumsamehe, hata aombe msamaha vipi sisamehi then namchukia sana.

Mnaosamehe mnawezaje jamani kuwasamehe waliowakosea?
 
1479203539715.jpg
 
Hello jf,katika maisha kila binadamu hukosea na aombapo huweza kusamehewa au kutokusamehewa..kwa wale mnaosamehe mnawezaje kufanya hivo sababu mimi mtu akinikosea kitu ambacho kikanitoa chozi basi huwa sisamehe yani huwa nashindwa kabisa kumsamehe hata aombe msamaha vipi sisamehe then namchukia sana,mnaosamehe mnawezaje jaman kuwasamehe waliowakosea?


Tafakari uliowakosea na pengine hawakuju akama wewe ndiye uliyewatenda. Madhara gani uliyowasababishia japo kwa vitu unavyoweza kuviona ni vidogo lakini hujui kwao vilikuwa na thamani gani.

Unaweza kuona namna gnai watu uliowakosea na wakajua halafu hata hawakukuuliza badala yakewalikusamehe na maisha yakaendelea?

Pengine umewafitinisha watu kwa ujinga na kutokujua, umefanya hila kuchukua nafasi ama sifa y amtu mwingine , umezuia watu kwa namna moja ama nyingine wasifikie malengo yao. Unajisikiaje?

Ninajua ulizaliwa ukajikuta ukpo duniani na hukujua utazaliwa ama utaishi maisha haya. Vivyo vivyo siku yako ya kufa huijui na utakufa kifo cha aina gani hujui.

Hivyo kumbuka katika kiburi cha mwanadamum mafanikio na majivuno yake, yuk chini ya Mamlaka ya Mungu. Anayesema Mungu hayupo ni mpumbavu asiyejitambua. Ni swa na mtoto anayemkataa mzazi wake kwamba hakumzaa ama hakuwa na umuhimu katika kuzaliwa kwake. Huyo ni mpumbavu.

Mungu ameweka taratibu za kuishi. Lakin wanadamu wajinga wamekuw awakizihoji na kuzipinga. Bila kusahau kwamba Mungu ndiye anayewaweka duniani na hata ndiye aliyewaruhsusu kupata hayo maarifa wanayodhani sasa ni makubwa kuliko uweoz wa Mungu.

Kumbuka wewe mara ngapi umemkosea Mungu an awala hajaminya mapafu yako ana kufunga pua za mara moja kwa kuw ana uwezo huo?

Mungu amekusamehe kwa kutokumwamini na kumtambua.
Mungu amekusamehe kw a matendo yako yanayomchukiza kila kukicha.
Alikuw ana uwezo wa kuku expose kwa mambo yako ya hovyo na kisha kukukatilia mbali. Lakini hajafanya hivyo kwa kuw ani mwingi wa Rehema. Anasubiri pengine ipo siku utabadilika kwa kuwa yeye hapendi kifo cha mtu mwovu.

Kwa kutafakari hayo, jiweke mahala pa huyo unayemwapia kakuksoea.

Ukiweza nenda kazungumze naye. Mtumie mtu akaongee naye uombe awakutanishe mmnalize tofauti zenu. Akileta ujinga, wewe achana naye lakini muwe mbela ya shahidi mwaminifu asije akaendelea kukuumiza.

Bila shaka naye atajifunza kitu katika maisha yake na kitamfaa kama si yo leo ni kesho.

Kwa kuzungumza utakuta mnajenga urafiki na maelewano mapya ambayo pia yataongeza siku zako za kuishi. Hasira hufupisha maisha yetu.
 
Ukitaka kusamehe watu wachukulie kama ni watoto wadogo bila kuwaangalia usoni lakini usiwadharau. Pia watu hawakukosei kwa bahati mbaya bila wewe kuwa sababu.
 
Hello jf,katika maisha kila binadamu hukosea na aombapo huweza kusamehewa au kutokusamehewa..kwa wale mnaosamehe mnawezaje kufanya hivo sababu mimi mtu akinikosea kitu ambacho kikanitoa chozi basi huwa sisamehe yani huwa nashindwa kabisa kumsamehe hata aombe msamaha vipi sisamehe then namchukia sana,mnaosamehe mnawezaje jaman kuwasamehe waliowakosea?
Unaona madhara ya kutosamehe sasa - Nilichokutana nacho jana sina hamu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom