Umejieleza vizuri sana,
Swali linakuja, unataka mtoto wako awe na confidence ipi?
Kama mnaongea vizuri, mnacheza vizuri, anafanya vizuri darasani unataka awe vipi tena zaidi? Maana ndio lengo la uzi wako,
Labda nikueleze kitu kimoja my dear friend, sikujui wala hunijui, ulichonacho moyoni wewe ndio unajua,
Trauma hujitokeza hata kwa abuse ya dakika 1, wewe unaona week mbili ni ndogo lakini trust me kwa mtoto haiwezi futika maisha yake yote (bitter truth),
Haukua kwenye maisha ghafla umejitokeza na kuanza kumpiga kwa week mbili mtoto wa miaka minne memory hua haifutiki,
Japo umeremba sanaa lakini ukweli unao ndio maana umekuja hapa kuomba ushauri wa kumfanya mtoto awe na CONFIDENCE, umesahau huko juu ulisema unaweza ukamuangalia akakuuliza "mbona unaniangalia nimefanya nini?" Ukamalizia "full kujishtukia, ananikeera"
Mtafute child psychologist near you, mpeleke mtoto akapate tiba mapema,
Kama wewe mzazi umeshaona kuna tatizo basi jua tatizo lipo.