Unawezaje kumaliza woga na wasiwasi wako na ufungue mipaka ya akili yako?

Nov 2, 2023
60
50
Kila kiumbe kimeumbwa na woga wa asili kama ishara ya hatari ili kuongeza umakini kisidhurike. Woga ni mfumo wa muhimu wa mwili wakujilinda na kitu chochote kinachoweza kuwa hatarishi kwako. Haimanishi moja kwa moja ukiogopa wewe ni mdhaifu, hata simba ana woga pia.

Lakini woga tunaoenda kuongelea hapa na unaotutesa kwenye maisha yetu si wa asili bali ni wakifikra, kimawazo tunao utengeneza wenyewe katika akili zetu. Na mara nyingi huja kwa kutotaka kukutana na uhalisia ulio tofauti na ulivyojijengea akili mwako. Tunaishi zaidi kwenye mawazo kuliko uhalisia wa maisha. Tumeumia sana na yaliyopita na tunahofu sana kuja kutokea wakati ujao na tunasahau wakati uliopo kwakuwa tupo ndani ya giza la hofu.

Mzizi mkubwa wa hofu zetu ni mawazo yetu wenyewe. Uwoga na wasi wasi huanza pale tu tunapoanza kuweka mawazo ya kutaka kujitoa ubinafsi wetu katika tukio halisi linalotusibu kwakuhofia usalama wetu kwa jinsi tulivyo jiwekea akilini mwetu. Akili imeshindwa kujua nini kinaenda kutokea kwetu kwa fikra tu za kimawazo.

Akili zetu zinachukua kumbukumbu zetu nakujua sehemu salama kwetu tulizozipitia ila ukikutana na hali tofauti na usalama ambayo hujaelewa basi hofu itanza na woga kwakutaka kujilinda na hicho kwakuwa hujaweza kutambua mipaka yako na kutodhurika nayo kwa kuweza kuishi bila kuhitaji usalama wa kiakili kwenye mawazo yako kukuzuia kuweza kuvuka mipaka yako kwa akili ilivyo jiwekea.

Na madhara ya ukishakuwa na woga basi hata kitokacho nnje kimatendo hakitokuwa uwezo wako wote bali kujilinda au kuukimbia woga huo na si kuumaliza ndani yako. Woga huondoa ufanisi wako. Inafikia tunadhurika kuogopa kuwa jinsi tulivyobarikiwa vipawa vyetu kwakua tunaona kama visipo tupa fedha haraka situtaonekana tunafanya ujinga au hatuto onekana wa thamani. Kwahivyo inatubidi tutafute kitu kinachotupa fedha halaka na kusahau vipawa vyetu vya ndani vyamuhimu kwenye maisha yetu kwa woga tu.

Woga umetusumbua muda mrefu sana na kutufanya tushindwe kufurahi na maisha yetu. Tumeshaona woga wetu mkubwa ni zao letu la akili. Tijiulize ni kweli ishara za mawazo yetu ni kitu chakutuogopesha ama ni sisi ufahamu wetu mdogo wa kuelewa mawailianoya akili yetu wenyewe kwa kuchanganya ishara na uhalisia ni upi na kuathirika nao kwa kuweka unafsi kati. Nakupingana na woga wako kutaka kupambana nao ni kama una mwagia moto mafuta, ni wewe unapigana na mawazo yako mwenyewe bila kujua. Na ukitaka kujificha kwa kutafuta usalama ili kukwepa hofu itabaki ina kusubiri kwakuwa hujaiondoa bado.

Tumeanzisha mbinu za kuweza kupambana na woga wetu lakini hazitoweza kutusaidia. Tunahitaji suluhisho litamaliza kabisa woga wetu wote kwa pamoja na si kipangana na woga mmoja kwa mmoja hutoweza kumaliza akili haina mwisho wa kufikiri. Kitu gani sasa kinaweza kufungua hili fumbo na kuweza kupata uhuru kwenye akili zetu na kuishi bila bugudha ya woga.

Ukiweza kuangalia kwa makini mawazo yetu ya woga kama ishara sio tatizo ila kushidwa kuwa na maelewano mazuri ya kutambua akili yetu inayofanya kazi kwa kujitegemea (nafsi) inatengeneza usalama wa kimawazo wakujilinda. Ukiweza kuwa na umakini wa ufahamu kuweza kuona jinsi akili yako inavyoweza kujitengenezea usalama bila kutaka kudhibiti chochote kile kuelewa ni ishara na si uhalisia. Kwa kuweza kuona hili wewe mwenyewe ndani yako utaweza kuona utofauti kati tukio halisi linalotokea mbele yako na tukio unalo litengeneza kwenye mawazo yako na woga wa kimawazo huwa ndio mwisho wake.

Kuishi kwa kuwa salama muda wote kunatufanya tushindwe kuingia ndani ya hofu zetu kujiweka huru nazo. Na lamuhimu kuelewa sana ni msaada pekee ni ule tu unaojisaidia mwenyewe kwa kuelewa ukweli tu. Bila kuhusisha mtu yeyote kukwambia chochote. Wewe mwenyewe unatakiwa uwe mwangaza wa maisha yakoxna si mtu mwingine yeyote kwa elimu yake au imani yake yoyote na huu ndio ukweli utaokuweka huru kwenye kila kitu.

Nb: Iwapo tutaishi kijinga kwa kufikiri kila kitu cha kwenye mawazo yetu kinatuhusu basi tutakikuza na kitatuadhiri zaidi na zadi. Tuelewe mipaka ya mawazo yetu na uhalisia wa maisha na tutaweza kuishi kwa furaha muda wote.
 
Back
Top Bottom