Unawezaje kumaliza uraibu (addiction) wako mara moja

Nov 2, 2023
60
50
Nyakati hizi tumekuwa tunaishi kwenye mateso kuliko furaha. Tumekuwa watumwa wa tabia zetu wenyewe tusizo zipenda. Na kupelekea maisha yamekuwa ya kujutia, mkanganyiko wa kimawazo na kujinyausha akili zetu bila kujua kwa "stress" . Kwaufupi ni kama tunaishi jehanam, amani na furaha ni kitendawili kwetu.

Kuishi kwenye uraibu "addiction" ni maisha yenye matesa sana. Uraibu mara nyingi unakuja pale ambapo unakuwa unajihisi mdhaifu, kuchanganyikiwa kimawazo ile hali ya kutaka kudhibiti hisia zinazo kubugudhi kwa kupata ahueni kutoka kwenye kitu flani ili ujihisi kutua mzigo wakihisia au kama kujisahaulisha maumivu na hicho kitu kuchukua nafasi kubwa katika maisha yako na kushindwa kujisaidia mwenyewe kwenye kutoka kwenye utumwa huo.

Na kitu kikubwa kibaya kwenye uraibu utakufanya ushindwe kulielewa tatizo ulilo nalo kwa undani kwakuwa unalikimbia kwa njia tofauti. Ukijiona tu unauraibu flani ujue ni njia ya kukimbia ukweli wako wa ndani kwa hivyo hutoweza kulitatua kamwe hilo tatizo linalo kusumbua.

Kwanini tunakuwa waraibu?

Sababu kubwa inayotufanya tunaingia kwenye mtego huu ni kutafuta faraja na usalama wetu kwa kuogopa kukabiliana na hisia zetu na matatizo yetu kama yalivyo na maumivu yake. Tumekuwa waoga na maisha yetu wenyewe kwa kutojitambua thamani yetu na uwezo wetu tulionao wa kukabiliana na maisha yetu na tunaishia kungangania kwenye vitu vitupe thamani ya maisha na huu ni ujinga mkubwa.

Ukitaka kumaliza uraibu kwa kudhibiti hutoweza, ni utakuwa una ubadilisha majina tu na utabaki ukikuzunguka kwa njia tofauti kwakuwa umeupa umuhimu unaupa maisha chini ya kapeti na utakumalizia nishati yako ya kimwili na kukunyima uhuru kamili wa kiakili.

Kitu cha muhimu na unatakiwa ukielewe kwanza, ni lazima uwe tayari kupokea hisia zote bila kuchagua. Na uweze kufahamu mwili wako unakupa ishara gani na uzielewe. Bila hivyo utaishia kuwa muathirika wa ishara za mwili wako na kutaka kuzikimbia badala ya kuzielewa. Ufahamu huu tunaokosa unapelekea tunaishia kuwa waathirika wa vitu tunavyo vifikiria zaidi kuliko vitu halisi vinavyo tokea.

Njia pekee yakuweza kumaliza uraibu wako ni kutabiliana na matatizo yetu kama yalivyo kwa kuyaelewa uhalisia wake bila kuanza kujitengenezea kuathirika kimawazo kutako kufanya ushindwe kuangalia tatizo halisi na kuanza kutafuta njia ya kujitoa kwenye tatizo. Na ukiweza kuweka umakini wako wote kwenye tatizo bali utaweza kuli maliza kwenye mizizi yake mara moja.

Kwa kuweza kutuliza akili zetu na umakini wetu ukaishia kwenye kulielewa tatizo zaidi ya kulitengenezea juu bustani ya kupumzikia basi hatutofikia kuwa na uraibu wowote kwenye maisha na tutaishi tukiwa timamu kwa kufurahia kila kitu kwenye maisha yetu.

Nb: Uraibu ni matokea tu kama majani ya mti, ukiweza kujua mbegu gani iliyo pelekea kuwa na mti huo basi ndio mwisho wake na si kusumbuka kukata matawi utatumia nguvu nyingi lakini hakutokusaidia kitu.
 
Back
Top Bottom