Sehemu ya akili inayojiendesha yenyewe usiyopaswa kuidhibiti

Nov 2, 2023
60
50
Akili ni kiungo muhimu sana kwa kiumbe chochote. Vitu vyote tunavyotenda kwa kusema kwa hiari na bila kujua (moyo kudunda, kupumua na mengi tusiyoyajua) kwenye kuishi kwetu akili ina husika kwa asilimia zote.

Kwa jinsi tunavyoishi tulivyozoea kwenye mifumo yetu kutumia nguvu na kudhibiti imekuwa kipaombele kwa kufikiri ndio njia yakuweza kufanikisha kitu. Tunapoteza nishati nyingi sana kwakufanya vitu kwa kulazimisha viende tunavyohisi ndio sahihi kwa kutimiza tamaa na faraja zetu bila kujua kuna ushawishi gani mkubwa nyuma yetu unaopelekea hivyo.

Na haya yote yanatokea kwenye akili isiyojitambua misingi yake. Tumevipa vipaombele vitu vingi ila ujinga wa kutojitambua wenyewe unatutesa sana. Tunaenda shule, kwenye dini kutaka usalama na suluhisho la jinsi tulivyo tuweze kuwa sawa (kuishi kwa furaha na amani yote) na hilo haliwezi kutimia mpaka wewe mwenyewe uweze kulitimiza kwa kujichimba na kujitambua mwenyewe.

Tuanze na kujiuliza swali dogo, kwanini mawazo yetu tunayaona kama ni kitu kinatuletea na sisi tunapokea na muda mwingine hatuyataki lakini bado yanakuja. Na ugomvi mkubwa wa mtu ni yeye na mawazo yake ndio humchanganya na kumpa shida kubwa mwenyewe. Je, uwili huu unatoka wapi ndani ya mtu mmoja na ni wakweli?.

Tuna ufahamu kwenye akili zetu unaotufanya tuone kwenye sumaku yetu ya akilini tunayoitafsiri kama nafsi au umimi wetu, kuishi kwako kote na mifumo yako yote imehifadhiwa hapo na kukufanya kuhisi ndio wewe huyo kwa taarifa zilizopo. Ila kwa hakika huyu si wewe ni taarifa tu za jinsi ulivyo ishi zime hifadhiwa hapo na fumbo kubwa linalo tuchanganya ni kwakuwa taarifa hizo zinajiendesha kwa kutupa ishara ya tulivyo tenda na tunavyoweza kubadilika kutenda muda huu na ujao kwa jinsi tulivyo hifadhi taarifa.

Tatizo letu kubwa ni ufahamu wetu kutokuwa huru kwenye hii sumaku ya ishara inayojiendesha yenyewe yenye taarifa za tulivyoishi na kujiona ndio sisi na kutaka kuidhibiti kwa nguvu zote. Hapana, jambo la maana kufanya ni kuelewa kuwa ufahamu kwenye akili zetu hauwezi kufanya lolote lile kudhihiti hii sehemu yetu inayojiendesha akili mwetu na unapaswa uwe na ufahamu navyo tu nakuelewa vilivyopo ndani ya sumaku yako ya taafifa.

Na hii ni maana kubwa ya kujitambua inayompa mabadiliko makubwa binadamu kwa kuwa na ufahamu ulio huru na maudhui ya akilini mwake mwenyewe. Ukisha weza kuelewa mawazo yako yote ni ishara za taarifa tu ulizo nazo na hauhiski kuathirika nazo basi utakuwa mtu bora sana na hatari kwa uwezo uliokuwa nao wakujitambua.

Nb: Ila ukiwa mjinga na kutaka kuanza kupingana na mawazo yako kwakutojua yanajienda yenyewe na si tatizo ndio mfumo wake basi utaishia maisha yasiyo na furaha na amani muda wote kwakujitafsiri sivyo tu. Wewe si sumaku ya kuhifadhi taarifa geuza ufahamu wako na uone wewe ni kila kitu na ni ulimwengu wote bila kikomo.
 
Back
Top Bottom