Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 141,980
- 285,477
maneno matupu hayavunji mfupa .Binafsi ukiniuliza swali hilo nitakujibu kuwa sababu kubwa ni mfumo wa Stakabadhi Ghalani ambao umetuathiri sana wakulima wa Korosho, Serikali ya CCM imekuwa haina msaada kwa wakulima wa korosho wakati wa maandalizi ya zao hilo, lakini jambo la ajabu ni kuwa serikali hiyo hiyo imekuwa ikiibuka na kuwakopa wakulima tena kwa Mabavu kwa kutumia mfumo wanaoita stakabadhi gahalani.
Baada ya kuchoshwa na hali hiyo wakulima wa Korosho waliamua kuanzisha umoja wao UWAKOTA ili waweze kuingia wenyewe mnadani lakini serikali ya CCM tena kwa kumtumia katibu wao Mwenezi Ndg Nape Mnauye waliahidi kupambana kuhakikisha umoja huo haufanyi kazi hususani baada ya kugundua kuwa unatoboa siri za bei halisi ya Korosho, hii ni dhuluma kubwa sana.
Nasema tena na tena DAIMA NITAICHUKIA CCM. Hebu nieleze wewe kwanini unaichukia CCM
![]()