Unaweza kutueleza ni kwanini unaichukia CCM?

Unaweza kutueleza ni kwanini unaichukia CCM?

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,292
Reaction score
6,773
Binafsi ukiniuliza swali hilo nitakujibu kuwa sababu kubwa ni mfumo wa Stakabadhi Ghalani ambao umetuathiri sana wakulima wa Korosho, Serikali ya CCM imekuwa haina msaada kwa wakulima wa korosho wakati wa maandalizi ya zao hilo, lakini jambo la ajabu ni kuwa serikali hiyo hiyo imekuwa ikiibuka na kuwakopa wakulima tena kwa Mabavu kwa kutumia mfumo wanaoita stakabadhi gahalani.

Baada ya kuchoshwa na hali hiyo wakulima wa Korosho waliamua kuanzisha umoja wao UWAKOTA ili waweze kuingia wenyewe mnadani lakini serikali ya CCM tena kwa kumtumia katibu wao Mwenezi Ndg Nape Mnauye waliahidi kupambana kuhakikisha umoja huo haufanyi kazi hususani baada ya kugundua kuwa unatoboa siri za bei halisi ya Korosho, hii ni dhuluma kubwa sana.

Nasema tena na tena DAIMA NITAICHUKIA CCM. Hebu nieleze wewe kwanini unaichukia CCM

attachment.php

 
wafanyakazi kugawana mshahara nusu na nusu na serikali eti kodi wakati wawekezaji na wafanyabiashara wanalipa asilimia ndogo tu
 
ccm aina tofauti na tajiri anaye watukania mama zetu mtaa mzima then bdae anatukaribisha chakula nyumbani kwake kwa binadamu wa kweli na mwenye ufahamu hato kwenda ila kwa mtu mwenye ufahamu mb 8 atakuwa wa kwanza getini kwa tajiri kumbuka ya kwamba duniani kuna binadamu na watu mimi ni binadamu ndo maana nimechagua kuto kwenda je wewe ni nan? mtu au binadamu
 
Kuua kabisa huduma za afya na elimu nchini haifai tena ccm inaongoza kihuni
 
Kule znz'bar waliua watu wasio na hatia, wanaitawala zanzbar kimabav na kisaikologia kwa kivuli cha utukufu wa muungano,
 
Kila tukijitutumua wanatudidimiza, eti zimwwi likujualo...
 
  • Thanks
Reactions: bht
Kuna mtu mmoja alienda kuchukua Fomu ya kugombea Uraisi akakwama kwenye Lifti
Dah... Jamaa aliilaani kweli CCM.

Mimi naichukia kwa sababu ya Rangi yake, na ukitaka kuijua rangi ya CCM
sio kijani wala Njano itazame wakati wa Kura za maoni za Uraisi, Ubunge na Udiwani
hapo utaijua CCM.
 
mm ni yale matusi yao kwa wananchi yanayofanywa na nape na vijana wenzake bila kuchukuliwa hatua au tamko ndicho kinachonifanya niichukie ccm mfno kuna wakati akiwa kanda ya ziwa alidai atawashikisha ukuta wasioitaka ccm ....
 
Back
Top Bottom