Unaweza kutofautisha Ukimya na Jeuri?

Unaweza kutofautisha Ukimya na Jeuri?

Unaweza kutofautisha ukimya na ujeuri?

Kuna msemo unasema Silence is golden

Ni kweli, lakini not every silence is wisdom

Kuna watu wanaonekana ni wakimya, na kweli wanaweza kuwa wakimya kwa asili yao

Ila wakati mwingine sio ukimya tu, bali nyuma ya huo ukimya kuna jeuri, kiburi au dharau

Kwa mfano, huwezi ukasalimiwa halafu ukaamua kukaa kimya, au ukaulizwa jambo ukawa unamtazama mtu bila kujibu, halafu useme eti wewe ni mkimya

Kwa mtazamo wangu huo sio ukimya wa kawaida, huo ni silent disrespect

Kila kitu kina faida na hasara zake

Ukimya una faida nyingi unaweza kukuepusha na ugomvi, maneno yasiyo ya lazima na makosa mengi

Lakini hapa naongelea ukimya
kupita kiasi, sio ukimya wa busara

Too much silence wakati mwingine inaweza kukugharimu

Unaweza kukosa fursa za kazi, biashara, urafiki au hata mahusiano mazuri

Watu wanaweza kukuona una jeuri, una kiburi au unawadharau, ilhali wewe unaamini ni tabia yako tu ya kuwa mkimya

Mimi naamini kuna tofauti kubwa kati ya being quiet na being rude

Mtu anaweza kuwa mkimya lakini bado akawa na heshima

Anaweza kuitikia salamu, kujibu anapoulizwa na kuwasiliana inapobidi
Na hata kushiriki mijadala mbali mbali na kutoa hoja

Heshima haihitaji maneno mengi
Hii ni kweli kabisa


Kwako mdau🫴
Swali la Mjadala👇

Unawezaje kutofautisha ukimya wa busara na ukimya unaoficha jeuri au dharau?

Au kwako yote ni kitu kimoja?

Ni Zipi faida hasa za kua mkimya sanaa?

Ni zipi hasara za kua mkimya sana?

Una furahia ukiwa karibu na mtu mkimya sana au unakua bored?
Mimi ninavyo vyote 😅😛
 
Correct na nimejifunza not to prove myself to anyone

Jamii ya kitanzania na Africa kwa ujumla watu wapo low minded na hii imechangiwa ba vitu kama dini, mila potofu, na umaskini

Wengi hawajui hasa kwa nini wapo humu duniani, so unavyo leta perspective mpya wanaanza kuona umewazidi subconsciously lazima watakuchukia tu because people hate what they don't understand.
Absolute right . sio kila kitu kibaya kutoka kwa wazungu lakini hili la kila mtu a mind his business ni kitu bora sana
 
Back
Top Bottom