Unavaa saa mkono gani?

Tripitaka

Member
Nov 30, 2019
75
150
Mimi navaa kushoto, lakin baada ya kuvaa sana saa mkono wa kushoto sasa hiv mkono una kama alama hiv, yaani ile sehem ya mkono imekua white tofauti na sehem nyingine ya ngozi.

Hii inakaaje wakuu inaweza kuniletea shida yeyote kiafya ?
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
8,912
2,000
Mimi navaa kushoto, lakin baada ya kuvaa sana saa mkono wa kushoto sasa hiv mkono una kama alama hiv, yaani ile sehem ya mkono imekua white tofauti na sehem nyingine ya ngozi.

Hii inakaaje wakuu inaweza kuniletea shida yeyote kiafya ?
Usibane sana mkanda wa saa.
kuhusu madhara ya kiafya tungoje wajuvi waje hapa tupate faida.
 

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,190
2,000
Saa inavaliwa kutokana na mkono mtu anaotumia sana. Kama mtu anatumia mkono wa kulia (Right Handed) sana basi saa anavaa mkono wa kushoto. Na kama mtu anatumia mkono wa kushoto (Left Handed) sana basi saa anavaa mkono wa kulia.

Hii inatokana na hatari ya kuivunja, kuiharibu au kuichakaza saa yake.

#Sio Lazima Kufuata Principle Hii.
Hii nimeipenda imewai kunitokea.
 

Joanah

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
15,873
2,000
Navaa kushoto
Huwa naiweka kama anavyoiweka mpenzi wako...ni rahisi zaidi kuangalia muda kwa namna hiyo

Kipindi nasoma,ule muda tunafanya mitihani nikiigeuza kuelekea upande wa kiganja nakuwa naenda vizuri sana na muda
 

Nature

Senior Member
Nov 5, 2014
131
1,000
Nilikuwa navaa saa mkono wa kushoto nilibadilisha baada ya kuona wanawake wengi wanavaa mkono huo niliamua kuvaa mkono wa kulia mpaka sasa.

Sababu kubwa iliyonifanya nibadilike ni mpenzi wangu pia anavaa mkono wa kushoto na anaigeuza sehemu ya kuangalia mda inakuwa kiganjani, huangalia muda kila baada ya masaa kadhaa ya kazi kupita sasa jinsi anavyoangalia anavutia sana, niliona huu kumbe ni mkono wa kike nilivua saa yangu na kuivaa mkono wa kulia.

Ni mtazamo wangu tu, wenzangu sijui kwanini wanavaa mkono wa kulia au kushoto!
Ilikuwa ni uoga wako tuu

Suala la kuvaa au kutokuvaa saa mkono wakushoto halikuondolei au kukushushia hadhi yako kama mwanamume
Heshima na unadhifu wako kama mwanamume unaanzia kwanza kwenye akili yako
Wanaume wote maarufu ninaowafahamu wanavaa saa mkono wa kushoto ..na haijawaondolea sifa ya kuwa wanaume wenye heshima
Mfano

Magufuli,
Biden
Obama
Ronaldo
Majaliwa
Kikwete
Lewandowski
Lebron James

Na wengine weengi ,

Na pia watu wengi wanatumia mkono wa kulia kwa mambo mengi mfano unapokula chakula....kama ni saa ya mkanda wa chuma basi ni kash kash zisizo maana

unaweza kuta mtu ni fundi carpenter kwa hiyo mkono waa kulia kuanzia asubuhi hadi jioni ni nenda rudi ,Panda shuka..kwa hiyo ni rahisi saa kuharibika....

Kazi nyingi ngumu zinafanyika kwa mkono wa kulia, japokuwa siyo wote wanatumia mkono wa kulia kwa hiyo uwezekano wa Saa kuharibika ikivaliwa mkono wa kulia ni mkubwa zaidi

Hoja ya kusema kwamba unaacha kifanya jambo kwa sababu tu eti mwanamke au msichana anafanya hivyo hivyo ni ushamba

Kwa hiyo wanaume waache kucheza na kushabikia mpira wa miguu kwa sababau eti siku hizi kuna wanawake nao wanacheza mpira wa miguu kama wanaume?

Sent from my TA-1032 using JamiiForums mobile app
 

oscar classic

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
462
1,000
Mimi navaa kulia sababu ya king kiba anavaa kulia,

Alafu kulia ni mkono wa kuume thusy namimi navaa saa kwenye mkono wa kiume
 

cocastic

JF-Expert Member
Nov 30, 2019
16,981
2,000
Navaa mkono wa kulia, ila SAA inakua upande wa kiganja hivyo huwa rahis kwangu kutazama muda.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom