Unavaa saa mkono gani?

Nilikuwa navaa saa mkono wa kushoto nilibadilisha baada ya kuona wanawake wengi wanavaa mkono huo niliamua kuvaa mkono wa kulia mpaka sasa.

Sababu kubwa iliyonifanya nibadilike ni mpenzi wangu pia anavaa mkono wa kushoto na anaigeuza sehemu ya kuangalia mda inakuwa kiganjani, huangalia muda kila baada ya masaa kadhaa ya kazi kupita sasa jinsi anavyoangalia anavutia sana, niliona huu kumbe ni mkono wa kike nilivua saa yangu na kuivaa mkono wa kulia.

Ni mtazamo wangu tu, wenzangu sijui kwanini wanavaa mkono wa kulia au kushoto!

Mimi huwa huwa navaa mkono wa kulia,maana mkono wa kushotovndio huwa nautumia kuandikia na kazi za mikono pia.
 
Saa inavaliwa kutokana na mkono mtu anaotumia sana. Kama mtu anatumia mkono wa kulia (Right Handed) sana basi saa anavaa mkono wa kushoto. Na kama mtu anatumia mkono wa kushoto (Left Handed) sana basi saa anavaa mkono wa kulia.

Hii inatokana na hatari ya kuivunja, kuiharibu au kuichakaza saa yake.

#Sio Lazima Kufuata Principle Hii.
Japo umeweka angalizo kuwa sio lazima, lakini huu ndio ukweli wenyewe

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Mkono gani kuvaa saa inategemea na aina ya mkono mtu autumiao na wala si maamuz binafsi, japo wachache huamua tu wao binafsi. binafsi am left handed so navaa saa mkono wa kulia, na naona wengi wanaovaa sa kushoto ni wale ambao ni right handed!! ni hivyo tu yaani
 
Saa inavaliwa kutokana na mkono mtu anaotumia sana. Kama mtu anatumia mkono wa kulia (Right Handed) sana basi saa anavaa mkono wa kushoto. Na kama mtu anatumia mkono wa kushoto (Left Handed) sana basi saa anavaa mkono wa kulia.

Hii inatokana na hatari ya kuivunja, kuiharibu au kuichakaza saa yake.

#Sio Lazima Kufuata Principle Hii.
Nimependa huu ifafanuzi,lakini ngoja nichangie.

Kuna ambao huvaa saa za chuma na kulegeza mkanda yaani saa inapwerepweta anaigeuza atakavyo(binafsi sipendi)haitulii pahala pamoja

Na mara nyingi hizi ni saa za chuma.
Watu wa aina hii kuepuka usumbufu wavae mkono ambao hauna harakati nyingi.

Kuna ambao huvaa saa hizo hizo za chuma au zingine za mipira, lakini mikanda yake mipana mno kiasi kwamba hata kuandika haandiki vizuri.

Mtu kama ana harakati nyingi za kuandika andika basi kuepusha usumbufu pia bora avae katika mkono ambao hatumii kufanyia shughuli zake.

Alafu kuna ambao huvaa saa za chuma lakini zimekamata vizuri mkononi kiasi kwamba hata ufanye harakati za kunyanyua mkono bado saa iko pale pale hawa wanaweza kuvaa katika mkono wao wa kulia kwa sababu saa haimsumbui wala kumtia uzito.

Lakini zipo saa za aina nyingi sana ambazo kwa watu wanaopenda kuvaa mkono wa kulia zipo saa nyingi tu ambazo haziwezi kuwasumbua endapo watavaa kwa mkono huo.

Saa mikanda membamba,nyepesi,inakaa vizuri mkononi,imebana vizuri japo sio sana,hizi saa zipo nyingi sana.

Lakini pia kuangalia kazi ya mtu ni muhimu sana.

Mfano kuna watu wao kazi yao kubwa ni kuandika ofisini labda wanatumia mkono wa kulia,mtu huyu pengine akaacha kuvaa mkono wa kulia kwa kudhani harakati nyingi zitaharibu saa yake,huyu anajinyima tu kwa sababu neno harakati linamtisha wakati hakuna harakati hiyo ya kutisha.

Neno harakati liangaliwe tena kwamba ni harakati zipi.

Kuandika ni harakati,kuuza bidhaa ni harakati,kubeba zege harakati,ukonda harakati n.k

Binafsi kitu kingine huwa ninachotizama ni urahisi wangu wa kuangalia saa naupata ukiwa mkono gani.

Mkono wa kulia nimezowea kuvaa saa na kufanyia vitu vingi hivyo hata nikivaa saa ni rahisi kwangu kuangalia saa luliko mkono wa kushoto.
 
Saa inavaliwa kutokana na mkono mtu anaotumia sana. Kama mtu anatumia mkono wa kulia (Right Handed) sana basi saa anavaa mkono wa kushoto. Na kama mtu anatumia mkono wa kushoto (Left Handed) sana basi saa anavaa mkono wa kulia.

Hii inatokana na hatari ya kuivunja, kuiharibu au kuichakaza saa yake.

#Sio Lazima Kufuata Principle Hii.

hii ndio kanuni sahihi ya uvaaji saa na kwa kuongozea tu,saa zinatengenezwa kutokana na mkono unaoivaa.saa ya kuvaliwa na mtu wa mashoto(lefty) ambae ataivaa mkono wa kulia,ile knob yake ya kubadili majira huwa inawekwa tofauti na saa ya kuvaa mtu wa right.
 
Ila Sasa kuzipata hizi za sisi mashoto ndo ubahatishe
 
Navaa kushoto

Biologically, mkono wa kulia una activities nyingi hautaki uzito kitu kinachomzongazonga...pia kuna ukushoto fulani hivi kuvaa kulia.

Fashionable, mkono wa kushoto hana shunguli nyingi basi abaki na urembe wa saa na brasalet...hata movement yake si strong.

Safety, saa ikikaa mkono wa kulia una % kubwa ya kuharibika haraka activities za mkono na quickly movement.
Umejibu kitaaluma kabsa. Asante.
 
Back
Top Bottom