Unatumia unit ngapi za LUKU kwa siku?

Binafsi sina uwezo wa kutumia AC kwa sababu wengi niliongea nao wanaomiliki AC wanasema umeme wa 10,000 (28+units)kwa siku hautoshi, especially kama unatumia nonstop.

Umeshawahi kuishi nyumba yenye AC na kununua umeme wake? Labda unaweza kuwa na practical experience.
Yaani umeme wangu wa wiki nzima hautoshi kuwasha AC siku moja! Hapo sipawezi nitaiweka kama pambo
 
Unatumia yuniti ngapi za LUKU kwa siku?

Wajemeni, siku hizi naona kama mita ya umeme inakimbia. Hivi kwa wastani yuniti ngapi za LUKU hutumika kwa nyumba ya kawaida tu?
Microwave,,Ceiling fan, freezer, pressure cooker, rice cooker,washing machine, deki,= 3.4 KWHR/day
 
Ila kwa BTU 9000 si itakula umeme mchache pia?
Usije ukajikoroga ukanunua AC yenye BTU 9000 hii ni ndogo sana imelenga vyumba vidogo kama chooni mara nyingi ni ukubwa wa vyumba vya mita za mraba 6 ( yaani mita 2 kwa mita 3 na urefu wa ukuta mpaka "ceiling board" mita 3).

Kwa wastani AC standard kwa vyumbani unapaswa angalau uweke yenye BTU 12000 kwa chumba chenye ukubwa wa mita za mraba 9 mpaka 10 kwa matokeo mazuri. Hii kwa wastani hutumia umeme wa units 4 mpaka 7 kwa masaa 8. Hapa nimeweka kwa AC pekee sijamuisha na vifaa vingine ulivyonavyo.

Samsung mara nyingi zipo effective ukilinganisha na kampuni zingine kwa aina ya AC zinazouzwa bara la Afrika. Nimegundua kuna makampuni mengine yanaonyesha AC ina uwezo wa BTU 12000 ila uhalisia unakuwa ni BTU 9000.
 
Kwamba ni wahuni wahuni wanaforge digits?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom