Unatumia unit ngapi za LUKU kwa siku?

Naomba kufahamu utaratibu wa kuwa na luku ya peke yangu katika fremu ya Biashara. Nina matumizi makubwa ya umeme ukilinganisha na fremu zingine. Natamani kufahamu hili ili kuondoa migogoro ya siku za mbeleni. Asante TANESCO
Kitu cha kwanza tafuta fundi atenganishe mifumo,namaanisha akutoe kwenye mfumo wa pamoja akutengenezee wa kwako peke yako,
hapo utahitaji kuingia gharama za kununua main switch yenye earth leakage circuit breaker,wire 10-16mm sq mita kadhaa kutegemea hiyo main switch yako itawekwa umbali gani toka kwenye mita. Earth rod na earth wire, na wire 1.5mm sq na 2.5mmsq kwa ajili ya kuextend waya zako endapo itatakiwa hivyo.
Baada ya hapo huyo fundi atakuchorea mchoro wa wiring aliyoifanya na kuithibitisha kwa muhuri wake wa usajili(contractor). Kisha utaenda Tanesco
utapeleka maombi utapewa fomu za kujaza,utazijaza,watakuja kukagua na kuchora michoro yao.
Baada ya hapo watakupa makadrio ya fedha unazotakiwa kulipia ili uunganishwe na nishati hiyo.
Nadhani kwa hapa utapata mwangaza. kinyume na hapo nitafute inbox.
 
Bila shaka wewe ni fundi umeme[emoji1][emoji1][emoji1]
 
This is too good to be true.
 
huu ni uwongo, unless kama ivyo vifaa haviwashwi mwezi mzima
friji peke yake jipya la around 50W inalamba unit 1 kila siku ( likiwa on 24 hrs )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…