Unatumia formula gani kulisha nguruwe wako ?

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,327
5,273
Wakuu salaam Sana,
Huku jf huwa hatunyimani maujanja ya maisha Ni jukwaa Lina Wana POA Sana!

Nimeigia kwenye ufugaji wa nguruwe na nimeanza na wawili tu moja dume na mwingine jike ila uzao tofauti.na Wana umri miezi 5 hivi.
Naombe mnielekeze mbinu nzuri na rahasi yaa ya gharama nafuu jinsi ya kuandaa chakula Chao.

Natanguliza shukran
 
Toka lini nguruwe akalishwa chakula???---- Nguruwe ni Scavenger na rafiki yake ni Fisi, katika ndege Scavengers ni Tai, Mwewe na jamii zake na Kunguru, sasa wewe umeona mtu gani anayefuga hao ndege kwa ajili ya kitoweo???!!--- iweje wewe ufuge nguruwe??, basi fuga Fisi pia.
 
Are you serious ????
 
Duu mkuu mi hua nawalisha mchanganyiko wa pumba za mahindi na mchele.

Pia chakula chao kikuu hua nawapa maganda ya viazi mbatata, nayokusanya kutoka kwa wachoma chips mitaani, but hua nayapika ili kuua baadhi ya vidudu vinavyoweza sababisha wakapata magonjwa nyemelezi...

Usafi pia ni jambo lamuhimu hakikisha kila siku unasafisha pot zao za kulia na banda zao kiujumla.

Nawasilisha.
 
Nasikia nguruwe ni mnyama mwenye alimentary canal inayofanana na ya binadamu. Kwa hiyo vyakula vya binadamu anaweza pia kupewa nguruwe.
 
Leo sikukuu yenu ya eid tulia hivyo hivyo
 
Duu mkuu mi hua nawalisha mchanganyiko wa pumba za mahindi na mchele.

Pia chakula chao kikuu hua nawapa maganda ya viazi mbatata, nayokusanya kutoka kwa wachoma chips mitaani, but hua nayapika ili kuua baadhi ya vidudu vinavyoweza sababisha wakapata magonjwa nyemelezi...

Usafi pia ni jambo lamuhimu hakikisha kila siku unasafisha pot zao za kulia na banda zao kiujumla.

Nawasilisha.
Nashukuru mkuu japo hujaniambia mchanganyiko wa pumba unawapa kiasi gani?
 
Kuna mdau kuniambia nichukue kiroba kimoja Cha kilo 50 Cha grower wanazopewa kuku Kisha nichanyanye either na gunia 2 la pumba ya mchele au la mahindi alafu Kila siku niwape Kila mmoja kilo moja asbh kilo moja jioni

Ila naona hili chakula Ni Cha ghali mno kwangu
 
Toka lini nguruwe akalishwa chakula???---- Nguruwe ni Scavenger na rafiki yake ni Fisi, katika ndege Scavengers ni Tai, Mwewe na jamii zake na Kunguru, sasa wewe umeona mtu gani anayefuga hao ndege kwa ajili ya kitoweo???!!--- iweje wewe ufuge nguruwe??, basi fuga Fisi pia.
ni kweli, nguruwe ukichelewesha chakula, na yeye amezaa vitoto ananyonyesha, utamkuta anatafuta kitoto chake cha pili au cha tatu. akitoka nje, hao watoto wako wanatambaa (watoto wa binadamu) akijichanganya huwa anaweza kumla.
 
Nasikia nguruwe ni mnyama mwenye alimentary canal inayofanana na ya binadamu. Kwa hiyo vyakula vya binadamu anaweza pia kupewa nguruwe.
Ni kweli ila exception nasikia ni mbili
1. Papai
2 . Kitunguu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom