Kuhusu malipo ya kodi ya gari yako inayokuja, yawezekana ni kweli utafuata ukweli na haki utapoagiza gari yako, lakini bado unachosema hakijajikamilisha maana TRA hawajahakikisha. Hivi TRA ifanyeje kwa wale wanaocollude na suppliers kuiba kodi? Kwa mfano kuna wanunuaji wanamlipa muuzaji Japan bei ya kweli lakini wanakubaliana na muuzaji kuandika bei pungufu kwenye documents. Hata kama TRA wangekua na list ya bei ya magari yote hapo bado haisaidii, maana kuna lingine lilishawahi kupata ajali kubwa na lingine halikuwahi, ama moja limetumika zaidi ya lingine kwa kipindi kile kile. Hapo ndipo uplifting ya wataalam wa TRA inatakiwa lakini bado mlango wa mnunuaji wa kujieleza na kujitetea utakua wazi. Hata hivyo kikomo cha kufuatilia lazima ukibalance mwenyewe maana storage charge itaendelea kuongezeka na ikifikia limit time gari litapigwa mnaada ili kupunguza msongamano bandarini.
TRA ifanyeje?
Kwani TRA huwa wanafanya nini kwa makampuni na watu wanaokwepa kulipa kodi humu ndani ya nchi? Je, huwa wana-uplift randomly tu kodi za makumpuni na watu jinsi wanavyojiskia? Maana watu wanaotutisha humu ni wale wanaotupa picha kwamba TRA wana-uplift wakijiskia tu. Na wengine humu wanasema wana-uplift pale kunapokuwa na clear signs za kutaka kudanganya. Tumwamini yupi?
Yaani mimi mwenyewe nimepata gari ya bei rahisi, na ingawa kulikuwa na mwanya wa ku-burgain CIF nikaogopa nisije nikawapa kisingizio pale wakiamua ku-uplify halafu nikashindwa kuwasha moto vizuri, maana communication kati ya mimi na jamaa nikielelezo nitakachotumia. Hivi kweli unamaanisha watu waache kununua magari yenye bei nafuu? Saa nyingine anayeuza bei nafuu si kwa sababu limepata ajali. Inawezekana tu kwenye mnada siku hiyo mambo hayakwenda vizuri. Sasa je unamaanisha watanzania waepuke kununua magari rahisi? Mimi nilidhani tunasaidia kuokoa pesa zetu za kigeni pale tunapopata magari nafuu.
Sidhani kwamba ni sahihi kuwa-treat waagiza magari kama wezi vile. Na kumpata mtu aliyedanganya si kazi hivyo. Na mifano tumeshatolewa hapa jinsi gani wanaofoji wanadakwaga kirahisi tu. Nina mshakaji wangu mmoja yeye huwa anaagaazi sana akawa ananipa moyo kwamba ku-forge ni rahisi tu, huwa wanatengeneza invoices nyingine tu hapa hapa. Sasa hii inahitaji rocket science kugundua? Wewe unamfahamu hata mmoja anaye-colude na supplier? Na je, ku-colude huko kunafanyika kwenye magari tu?
Hebu fikiria, ukimpata mtu aliye-forge document unatakiwa u-uplift ama umpeleke polisi?
Mimi nadhani kuna watu wanafaidika na huu mfumo wa hovyo hovyo. Na nia yao kubwa kuifanya iwe painful kufuata njia halali ili ukienda huko kwenye mazabe wao watengeneze mingo. Sasa tunapokaa na kutetea huu upuuzi kama vile mwenye haki ni mkusanya kodi tu na mlipa kodi hana haki yoyote kwa sababu rafiki yake ana colude na ma-supplier, nadhani si sawa. Kila mmoja awajibishwe kwa matendo yake. Kama mimi sijadanganya, basi hunitendei haki kuniadhibu kwa kosa ambalo sijalifanya kwa sababu tu unahisi nimelifanya. Kinachonisikitisha ni pale ninavyoona bandugu mnaona hii ni sawa kabisa. Kwamba mtu anahisi umetenda kosa, hana kielelezo chochote, anakuadhibu na wewe unakubali tu.
Sasa mimi nasema, waki-uplift nitatafuta hiyo hela nitawalipa ili kuiondoa hapo bandarini nianze kuitumia. Halafu hiyo kesi yake itafika mpaka kwa mkuu wa TRA. Ikishindikana itaenda mahakamani, hata iishe baada ya miaka 100, nitakula nao sahani moja, kudadeki!!! Na watanilipa gharama zangu zote za usumbufu.
Nikienda pale bandarini ntakuwa na camera yangu, kila niayeongea naye nnampiga picha, maana ataweza kuwa shahidi wangu baadaye atake asitake. Na nimeshaagiza kinasa sauti kidogo cha kujificha, kitafika kabla ya gari.
Hivi sisi tunamatatizo gani? Kuna kampuni imekuuzia gari, invoices unazo, bank transfer unazo, kampuni ipo hapa hapa duniani hata wao TRA wanaweza ku-communicate nao ku-verify. Halafu TRA wanakwambia hujanunua kwa bei hiyo wewe unakubali tu? Na unajipa moyo kabisa kwamba ulilofanyiwa ni sawa kwa sababu kuna rafiki zako huwa wana-forge documents. Namna hii tutaendelea kuwa watumwa nchini kwetu mpaka mwisho wa dunia.
Kwa maelezo ambayo tumeshayapata hapa kutoka kwa waungwana wengine, nawapa TRA benefit of the doubt. Kwamba siku hizi wanaokumbana ku-uplift ni wale wanaojaribu ku-forge documents either kwa kushawishiwa na agents wao au kwa utashi wao wenyewe. Unaambiwa leta bank slip, unaleta yenye value zaidi ya CIF yako. Unaambiwa fungua email yako hapo tuangalie hayo maongezi yenu, unaanza kutetemeka. Halafu baadaye unawalaumu TRA.