Ukweli ni kwamba document hii inabidi isainiwe na bandari pamoja na shipper. Sasa sidhani kuwa shipper anaweza kukubali kuwa kakabidhi gari haina radio wakati inayo. Mimi nilipewa hiyo inspection certificate yenye X kwenye radio/TV/DVD player na nilifuatilia kwa shipper hiyo radio (Gari ilikuwa CIF) mpaka akanitumia ingine ingawaje ilikuwa ya low quality.
Umegusa kunako! Na hiyo inazidi kuonyesha kwamba kuna vitu tunadhani tunavijua kumbe la, halafu tunakaa tunalalama tu.
Maana nilikuwa nashangaa iweje mtu wa TRA tu ndiye asign kwamba hakuna radio? Hiyo ingekuwa bonge ya loophole ambalo sidhani kwamba lingeweza kuwepo kwa miaka yote hiyo ... maana watu wangekuwa wanaibiwa hovyo zaidi bila kuwa na la kufanya.
Tokea nimeanza kufuatilia hili swala ninazidi kupata picha kwamba tatizo pengine ni watu tu kutokujua taratibu hasa, na haki zao mpaka pale wanapokabidhiwa mzigo. Na jinisi ninavyoendelea kukusanya taarifa ndio nazidi kugundua kwamba baadhi ya watu ambao saa nyingine ndio tunaamini wanajua vizuri hizi taratibu na wanaweza kutusaidia, ndio hawana clue kabisa.
Maagenti wengi hawajui kabisa kodi inakalculatiwa vipi na TRA. Kwa hiyo kwao bado ni muujiza tu. Kufanya jaribio lingine, jana tukampigia dalali mmoja na kumuuliza HRV yangu ya mwaka 2002 ambayo iko njiani inakuja itakatwa kodi kiasi gani akasema 3M mpaka 4M. Nikimuuliza unaipataje, anasema ni kwa uzoefu wake. Kama angekuwa ana clue, pengine angeniuliza CIF ni kiasi gani. Kwa hiyo vitu vinaenda kwa makisio tu. Baadaye unakuta kodi tofauti unawalalmikia TRA badala ya kumuuliza dalali wako.
Siku zote nilikuwa nashangaa iweje vitu vinyofolewe kutoka kwenye gari bandarini halafu kusiwe na utaratibu wowote wa kulalamika na kuwa companseted. Kila "agent" ninayemuuliza analiongelea kama ni swala la kawaida tu, na kwamba ikitokea kubali tu imekula kwako. Kumbe zipo taratibu, na wapo watu wanaofuatilia na kupata haki yao.
Bado kuna maswali mengi tu, na bahati mbaya wale unaodhani ndio wanafahamu na wanaweza kukusaidia hawana ufahamu wa kutosha, na ningetamani sana wangefuatilia kwa undani maana wao ndio wanaoagiza magari mara kwa mara. Mimi naagiza mara moja tu kwa matumizi yangu.
Gari yangu inakuja. Ingawa kodi nikubwa, nitalipa kihalali kabisa.
Sasa ngoja ifike hapa halafu mtu achomoe kitu pale bandarini, au TRA wajifanye wana uplift. Nasema hapatakalika pale na patachimbika ... Kudadeki! Hiyo kesi hata kama itaisha miaka 50 ijayo. Nimehakikisha vielelezo vyangu vyote nnavitunza vizuri.
Eti mtu anaambiwa gari yako si ya bei hiyo halafu anakubali tu kwa sababu TRA wameenda kuangalia gari hiyo hiyo wakakuta bei ni tofauti. Haulizi hata wameangalia wapi huko ambako ndio reference ya bei za magari duniani. Yaana nitawapeleka mpaka mahakama kuu wakaonyeshe hiyo reference ya bei za magari duniani iko wapi. Kudadeki!
Sisi ndio tatizo saa nyingine. Watu vihiyo kabisa wanatengeneza mitandao michafu ya kutunyonya, na si tunakaa na kuafiki kama madunya hivi. Hatujui kwamba TRA wakilipishwa zaidi kwa vifaa vinavyopotea pale ndio hivyo wao watalipa hilo swala umuhimu, sio mpaka JK akawaambie.