Unataka kuagiza gari??... pitia hapa kwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unataka kuagiza gari??... pitia hapa kwanza

Discussion in 'Matangazo madogo' started by dullymo, Oct 6, 2009.

 1. d

  dullymo Senior Member

  #1
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 21, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hello JF bros n sisz!
  watu wengi wamekuwa wakitaka kuagiza magari kwa njia ya mtandao. ni njia rahisi na inayosave muda na gharama nyingine kama nauli nk na unapata gari kwa bei poa. mimi ni miongoni mwa wanaoleta magari kwa njia hiyo na nigependa niwape points muhimu ambazo zitawasaidia wale wanaotaka kuleta magari kwa njia hiyo.

  WAKATI WA KUNUNUA
  1. makampuni mengi siku hizi yanaweka picha za magari lakini magari hayo hayapo katika stock yao.
  2. unaweza kulipia gari kisha ukaambiwa gari hilo limenunuliwa na mtu mwingine kwa hiyo wanakuletea gari linalofanana na lile. wanaweza wakakupa kwa bei ile ile, au kwa bei ndogo na wakakurudishia chenji au wakakwambia uongeze pesa zingine.
  3. unaweza ukatuma pesa na huyo ulomtumia akaingia mitini. yaani ukaibiwa usipate chochote na hata ukimfuatilia unaweza kupoteza muda tu. mfano katika trdcarview kuna makampuni yamewekwa kwenye blacklist kwa makosa tofauti.


  GARI KWENYE MELI.
  4. unaweza ukanunua gari vizuri na meli ikaingia ila documents zikachelewa kufika then hapo unatakiwa ujiandae na storage kubwa.
  5. meli inaweza kupata chochote wakati ipo kwneye maji so ni vyema iwapo utalipia na insurance yaani CIF na sio CNF.
  6. sometimes meli inawahi kuingia kuliko ilivyotarajiwa na hii ni mbaya iwapo utakuwa hufuatilii movements za meli bandarini.
  7. gari inaweza kucheleweshwa kutuma hata kwa zaidi ya mwezi mzima gari haijatoka japan.

  GARI IKISHAFIKA BANDARINI
  7. baadhi wameletewa gari zina sctratch na dent tofauti na walizoziona kwneye picha ambazo zimekuwa edited.
  8. kuna washenzi wana tabia ya kuchomoa vitu muhimu ndani ya gari kama vile power windows, cd players, cd changers, screens nk.
  9. gari inaweza kuchunwa au kukwanguliwa wakati ipo bandarini na huna wa kumlaumu.

  KULIPIA USHURU TRA
  10. mtandao wa TRA haupo stable kabisa na hiyo ndio sababu kubwa wanayoitumia siku hizi katika kuchelewesha kutoa documents za kulipia ushuru. yaani kukupa assesment.
  11. TRA hawakupi ushuru kulingana na invoice yako uliyonunulia badala yake wanakupangia ushuru kwa bei wanayotaka wao. mfano umenunua gari kwa CIF $2500 wao wanaweza kukupigia ushuru wa bei ya USD 3500
  13. registration ya gari huwa inachukua kati ya wiki 1 mpaka mwezi mzima otherwise utoe kidogodogo.

  MUHIMU
  - wakati unaagiza gari usisahau kuwaambi wakufanyie JAAI inspection ambayo inacost kama usd 200- 350. usipofanya huku watakuja kukufanyia kwa zaidi ya 700,000 na kukuongezea storage charge bure.
  - ukiambiwa kwa mfano gari hilo linacost ml5 kuanzia kulinunua mpaka kulisajili ni vizuri ukajindaa na ml6 au zaidi maana baadhi ya vitu havina guarantee mfano ushuru wataokupa tra, storage charge, agent fees, shipping line agent fees nk.
  - ni vizuri ulete gari isiyozidi miaka 10 na isiyozidi CC 2000 (exept magari ya mizigo na mabasi) maana haina kodi ya uchakavu na excess duty.

  - unapolitoa gari lako bandarini hakikisha umeandikisha vibao vinavyoonyesha chasis namba, umekatia insurance angalau ya wiki 1, ina triangle na fire extinguisher ili kukwepa usumbufu wa askari barabarani nk.

  wadau kama nimesahau kitu ni vizuri kuongezea mimi ni binadamu.
  nategema hii itakuwa useful kwa wale wanaotaka kuanza kuimport magari.
   
 2. m

  mendezz2009 Member

  #2
  Oct 6, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe sio mchoyo wa ujuzi
   
 3. F

  Fisadi.Jones Senior Member

  #3
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante Dullymo kwa maelezo yaliyojitosheleza.

  Kwa sala la vitu kuchomolewa bandarini, kuna mtu anayefanya kazi kwa C&F agent flani aliniambia kwamba una haki ya kuwadai bandari. Jamaa anadai usi-sign kuipokea gari kabla ya kuifanyia uchunguzi na kuahakikisha kila likichoko kwenye BOL kipo. Kama vitu vimeandikwa kwenye BOL, kwa mfano radio, na ukakuta imenyofolewa, una haki ya kuwadai bandari. Na watakulipa. Je, hii ina ukweli gani?

  Kwa suala la ushuru wa TRA, mbona kuna wengine kama kina Next Level wanadai wanatumia CIF yako unless kuna dalili za wewe kutaka kudanganya? Na hiyo bei wanayoitaka wao inaamuliwa vipi? Je, wana table za bei kwa kila aina ya gari? Kama sio, basi wao wanazitoa wapi hizo bei?

  Na kama TRA wanapanga bei randomly kiasi hicho, inamaana watu wawili mnaweza kuagiza gari mbili zinazofanana kabisa halafu mkapangiwa bei tofauti? Kama ndio hivi, sasa huu sio uhuni tunaotakiwa tuutolee macho badala ya kukubali kwamba ndio utaratibu sahihi? Je, nikiagiza starlet CIF $3,000 wakiniambia ni $30,000 kwa sababu tu sura yangu mbaya inabidi nikubali tu imekula kwangu?

  Ukweli hasa wa hii dhana ya TRA kujipangia bei uko wapi? Maana wengine wanasema hawafanyi hivyo wengine wanasema wanafanya? Na kama wanafanya hivyo, je, hii sio aina fulani ya ufisadi na wizi? Na, mbona watu (hasa madalali) wanalichukulia kama kitu cha kawaida?
   
 4. F

  Fisadi.Jones Senior Member

  #4
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Halafu mzee Dullymo unadhani hii site iko accurate?

  http://www.gariyangu.com/

  Nimeuliza kwenye thread nyingine lakini sikupewa jibu.

  Asante mkubwa.
   
 5. d

  dullymo Senior Member

  #5
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 21, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hiyo BOL umemaanisha Bill OF lading? kama ni hiyo huwa hawaandiki options za gari zaidi ya chasisi no na mwaka tu. hata ukisema ubishane bandarini kwa kuibiwa dvd player ya laki 1 lakini ikasababisha ujiongezee storage huoni utakuwa unapoteza muda bure bila ya kupata chochote.
  pia inawezekana kabisa kwa watu wawili kuleta gari sawasawa ila mkalipia ushuru tofauti. hayo yalinikuta mie mwenyewe nilinunua toyota raum 2 zote za mwaka 2000 ila moja walinipiga ushuru 1.7ml na nyingine walinipiga 2.2ml.
   
 6. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Hii imetulia mkuu. Nadhani ungeongezea mchakato wa ku calculate makato yote ya TRA - kama Dumping Fee, Import Duty, Exercise Duty, VAT etc. Hope Itakuwa reference nzuri hapa JF.

  Pia, tungetengeneza listing ya online sites zote ambazo can be considered SAFE kutokana na uzoefu wa watu tofauti.

  Hayo ndio maoni yangu mkuu.
   
 7. F

  Fisadi.Jones Senior Member

  #7
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
 8. d

  dullymo Senior Member

  #8
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 21, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
 9. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
   
 10. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2009
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Mkuu asante kwa hili. Hapa penye nyukundu mimi mbona sijaelewa. Maana nilileta gari toka UK sikuambiwa hili au ni kwa ajili ya magari yanayoagizwa toka Japan?
   
 11. F

  Fisadi.Jones Senior Member

  #11
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
  Last edited: Oct 6, 2009
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Asante sana mheshimiwa nikipata mshiko wa kununua gari nitayafanyia kazi mie
   
 13. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Dullymo,
  ebu tusaidie kuhusu tradecarview Maana hawa watu wanauza magari kwa bei poa sana na kuna makampuni mengi saana, sasa hayo ambayo wameyawekea lable kwamba ni ya kitapeli ni yapi???????????? Msaada kaka.
   
 14. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  We come back on this.....nikotight kidogo na ''mabox'' ya bongo!
   
 15. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Waheshimiwa,

  Kwa sehemu nakubaliana na maelezo ya kuagiza gari kwa njia ya mtandao kuwa ni gharama nafuu lakini kuna hasara zake. Waswahili wanasema rahisi ghali!!

  Nilipata uzoefu mwaka 2005 baada ya kuagiza gari toka Japan kwa kupitia agent mmoja hapo Dar kwa makubaliano kwamba gari langu nitalipata baada ya mwezi mmoja kwa gharama ya 2,500 USD wenyewe wanaita CIF(Cost Including Freight).

  Aina ya gari niliyotaka ilikuwa ni Mark II Baloon mettalic Blue, Manual Transmission,Petrol Engine,4 doors, PW na iwe ni 4 cylinders. Baada ya jamaa kumlipa ile pesa ilichukua miezi 2 mpaka gari hiyo kufika Bandari ya Dsm. Kama hiyo haitoshi tulivoenda kuikagua ile gari kwa ajili ya Clearence ilikuwa haina vigezo karibu vote nilivyotaka!

  Kweli ilikuwa ni Baloon metallic Blue safi inawaka. Lakini ikawa ni Automatic Transmission, Diesel engine na kibaya zaidi ikawa ni 6 cylinders. Kidogo nishawishike kuikubali lakini nikaona itanisumbua baadaye.Pale pale Agent nikamwambia hiyo haikuwa gari niliyokuwa nimeagiza. Na kwa vile nilikuwa nimesubiri kwa miezi 2 nikamwambia sina muda wa kuendelea kusubiri gari tena bora arudishe hela yangu nitafute gari sehemu nyingine.

  Unajua aliniambiaje? Nisubiri mpaka gari hiyo ipate mnunuzi ndipo arudishe hela yangu! Aliniambia nimpe 1 week ya kufanya logistics za kuindoa bandarini na kutafuta soko. Believe me it took me another 1 month ya kusubiri mpaka nikaamua kuwatumia polisi ili kumshinikiza jamaa aweze ku-refund pesa yangu. Hata hivyo jamaa alikubali mbele ya polisi na akaanza kunilipa kidogo kidogo mara leo milioni 1, kesho laki 5, mara laki 3 mpaka nikawa bored stiff.Hiyo nayo ilichukua kama mwezi na zaidi. Kwa hiyo jumla ya muda wote ikawa kama miezi 4 na zaidi.

  Uamuzi niliochukua baada ya hapo ilikuwa kwenda kwenye show room za Bongo nikachagua gari niliyotaka nikalipa hela yangu na kuondoka na mashine. Niliona kuagiza gari toka Japan au Arabuni ni upuuzi na kupoteza muda.

  Conclusion yangu ni kuwa,be careful na hawa watu wanaojifanya ni agents wa kuagiza magari au kukuletea gari baada ya kui-pick kwenye mtandao mara nyingi ni matapeli na wababaishaji. Kuna jamaa zangu wengi wamewahi kulizwa kwa mtindo huu wa kumtumia mtu akuletee gari. Kuna rafiki yangu aliletewa gari ikiwa ina chemsha kama unapika maharagwe na kwenye mtandao ilikuwa inaonekana bomba na bandari ilipofika ni exactly kama ilivokuwa inaonekana kweny mtandao,lakini inachemsha!!

  Kwa hiyo jamaani be careful. Kama una hela yako ni afadhali ukanunue gari yako kwenye show room zetu za Bongo unaweza kupata gari nzuri tu na ukaepuka usumbufu na gharama za kipuuzi zisizo za lazima.

  Wakatabahu,

  makoye.
   
 16. M

  Mfikilwa JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 363
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  magari toka uk yanatakiwa yawe na MOT iliyo valid.
   
 17. M

  Mfikilwa JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 363
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  inaniuzi sana hiyo ya kuuplift sijui, yani wee acha tu.
   
 18. M

  Mfikilwa JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 363
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kwenye mtandao wa tradecarview bonyeza kisanduku cha help hapo utaona neno la black list bonyeza utayaona hayo makampuni.
   
 19. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2009
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Asante wachangiaji Wote Raha ipo hapa kwangu Niliagiza Gari 3 aina ya Mitsibishi Grandis Cheriot 2 za 99 iliobaki 98 ajabu zile za 99 nimelipa Mil3.2 kwa kila moja ila ya 98 niliandikiwa ktk accesmnt ya kulipa 2.6 Hivi hawa jamaa wanafuata vigezo gani? Sielewi
   
 20. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inaelekea wewe si mtaalam sasa katika ili CIF sio COST INCLUDING FREIGHT bali ni COST INSURANCE FREIGHT- umenipata nipo katika fani hii zaidi ya miaka 12.
   
Loading...