Unashauriwa na Mkeo?...Utachanganyikiwa!!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,723
Mkuu Mwanajamvi...

Nimeona mara nyingi wanaume wakikaa pamoja utawasikia...Yule si anashauriwa na mkewe?..Ndo maana yuko kama amechanganyikiwa muda wote!

Ina maana wanawake wana ushauri mbaya sana?

Ni ushauri upi tuupokee na upi tuukatae toka kwa hawa raia?
 
Mi mke wangu ninavompenda huwa tunashauriana kila kitu cha muhimu kwa ajili ya maendeleo yetu

maneno ya vijiweni hayo mkuu PJ ukiyasikiliza utabomoa nyumba yako,

hasa wakati huu ambapo wanawake wengi wamesoma na wanajua maisha ni nini

mi nakataa ushauri wa wanaume wanaonishauri niukatae/dharau ushauri wa mke wangu..maana umetusaidia sana so far!

sorry kama kuna watu nimewakwaza!
 
mwanamke ni mshauri mzuri sana (mara nyingi) ingawa ukweli hukwepeki kuwa wakati mwingine mwanamke aweza kumshauri vibaya mumewe......

ila hii haifanyi basi kila mwanaume aombaye ushauri kwa mkewe anachanganyikiwa
hayo maneno ya kitaa tu kaka
 
Kaka PJ,
Ushauri wa wake zetu mara nyingi huwa ni mzuri na mimi huwa naufuata sana
lakini sometimes hawa viumbe huwa wanaweza wakakushauri kitu kama usipotafakari mara mbili mbili unaweza kukosana na ndugu, jamaa na rafiki zako.
Mfano kwa upande wangu linapokuja swala linalohusu upande wa ndugu zangu,
ushauri wa wife mara nyingi huwa sio MBAYA.
lakini mara nyingi ushauri wake huwa 'unajenga'.
 
mwanamke ni mshauri mzuri sana (mara nyingi) ingawa ukweli hukwepeki kuwa wakati mwingine mwanamke aweza kumshauri vibaya mumewe......

ila hii haifanyi basi kila mwanaume aombaye ushauri kwa mkewe anachanganyikiwa
hayo maneno ya kitaa tu kaka
Lakini nasikia mwanamke akiwa mshauri wako, bajeti kubwa ya fedha ya familia inakwenda kwenye ma'lipstic, chopstick, angel'face, lipshine, mediven na ma'chinese-sijui nini nin!:D:D
 
Kuhusu ushauri inategemea ntu na ntu.Awe mwanaume au mwanamke anaweza kuwa na ushauri mbaya au mzuri.Suala la ushauri mara nyingi pia huwa ni karama fulani kutoka kwa Mungu.Kuna watu wameumbwa na hekima na wengine ni aibu.
Cha msingi wewe mwenyewe uwe unachuja lipi jema au baya.Na as far as i know wanawake wengi wamepewa hekima hivyo ni watoa ushauri wazuri sana.
note that;
Behind every succesfull Man there is a Woman.
 
Nimesikitishwa sana na kauli nilizoanza kuzisikia sasa hivi kwamba ''JAMAA KASHIKWA NA MKE WAKE''!

wabongo bana,enewei
 
Lakini nasikia mwanamke akiwa mshauri wako, bajeti kubwa ya fedha ya familia inakwenda kwenye ma'lipstic, chopstick, angel'face, lipshine, mediven na ma'chinese-sijui nini nin!:D:D

huyo ni mke au mpita njia mwenye nia ya kukukomoa??

a woman who wants to have a family with you atakuwa makini sana na kila jambo linalohusiana na maisha yenu including finance.....
 
Kaka PJ,
Ushauri wa wake zetu mara nyingi huwa ni mzuri na mimi huwa naufuata sana
lakini sometimes hawa viumbe huwa wanaweza wakakushauri kitu kama usipotafakari mara mbili mbili unaweza kukosana na ndugu, jamaa na rafiki zako.
Mfano kwa upande wangu linapokuja swala linalohusu upande wa ndugu zangu,
ushauri wa wife mara nyingi huwa sio mzuri.
lakini mara nyingi ushauri wake huwa 'unajenga'.

Mkuu hapo kwenye red umeniacha kidogo.
Kwa ukweli ushauri wa mke si wa kupuuza but, lazima ujue wewe baba ndiye kichwa cha nyumba. Kichwa ndicho hufikiri. Hivyo ni lazima uanalyse ushauri kabla ya kuukubali moja kwa moja, vinginevyo unaweza ukachanganya mambo kama anavyoonyesha mkuu ndibalema hapo juu.
 
Na ukikuta wanaume wa aina hiyo wana matatizo maendeleo hayapo katika familia ni ndoto za alinacha ..wabinafisi wa mawazo ,wabaguzi kifikira ..
Msimamo wao Zero ...
kila siku wanapiga hatua moja nyuma badala ya kwenda mbele
 
Kuhusu ushauri inategemea ntu na ntu.Awe mwanaume au mwanamke anaweza kuwa na ushauri mbaya au mzuri.Suala la ushauri mara nyingi pia huwa ni karama fulani kutoka kwa Mungu.Kuna watu wameumbwa na hekima na wengine ni aibu.
Cha msingi wewe mwenyewe uwe unachuja lipi jema au baya.Na as far as i know wanawake wengi wamepewa hekima hivyo ni watoa ushauri wazuri sana.
note that;
Behind every succesfull Man there is a Woman.

and women will never be as successful as men because thet have no wives to advice them.........signature ya Nguli inahusu hapa
 
Nimesikitishwa sana na kauli nilizoanza kuzisikia sasa hivi kwamba ''JAMAA KASHIKWA NA MKE WAKE''!

wabongo bana,enewei
Yup broda!
Ukijaribu kuwa beneti na mywife, basi kauli ndo hizo hapo juu!
Kwa ufupi unaonekana huna mpango kwa watu wako wa karibu!..huh!
 
mwanamke ni mshauri mzuri sana (mara nyingi) ingawa ukweli hukwepeki kuwa wakati mwingine mwanamke aweza kumshauri vibaya mumewe......

ila hii haifanyi basi kila mwanaume aombaye ushauri kwa mkewe anachanganyikiwa
hayo maneno ya kitaa tu kaka

shem umenena......... muhimu uangalie ni ushauri gani ukubali na upi ukatae......... na sio kutoka kwa mkeo/mumeo tu bali kila anayetoa ushauri......... hakuna guarantee kuwa kama ni mume/mke basi ushauri wake siku zote utakuwa mzuri........... chekecha kila usauri na chukua ule wenye manufaa zaidi.............. muhimu ni ushirikishwaji........... hata kama ushauri wake hutaupenda laini usiache kumshirikisha ili awe informed unafikiria nini, unafanya nini na uko stage gani,.............

nmewahi kuona mwanmke akigombana na mumewe kwa sababu anamshauri mumewe wajenge na mume anasema hana hela ila mkewe haamini anafikiri mume anamalizia kwa wanawake na pombe.............. lakini ukweli ulikuwa mume hakuwa na hela ya kujenga.......... alikuwa akilalamika kwa mkewe anagombana naye kwa jambo lisilokuwepo na ingekuwa vyema wange tafakari naman ya kuongeza kipato cha familia ndio wajadili kujenga wakiwa na hela sio wagombane wakiwa hata ugali maharage ni shida nyumbani................ cha ajabu mke alikuwa hafichwi mshahara wa mumewe ila laiamini mume anapata mshahara mkubwa kuliko aliomuonyesha..........na yeye [ia alikuwa na kazi................... sasa mume alipoona ugonvi ule hautaisha leo wala kesho, akapiga stop mwanmake kujua mipango yake.......... hadi aliponunua kiwanja ndipo akampeleka akione na ndipo mkewe alipomuomba msamaha kwa kuwa alikuwa akimtkana kila siku wakati uwezo wake kifedha ulikuwa mdoko..............

so be careful............ si kila mtu anaweza kushauri.......... wengine wanaweza kuku-confyuzi kabisa................ na hata ukachanganyikiwa moja wa moja...............
 
Ndugu hayo maneno ya kweli hata mimi niliwahi kumsikia kaka yangu na wenzie nyumbani kwake akisema kitu hicho hicho, kwa pamoja walikuwa wanamwambia mwenzao kuwa siku hizi yuko kama kachanganyikiwa vile yaani life style aliyonayo ni ya kikekike kwasabau ya kushauriwa na mkewe mambo mengi. Lakini sasa cha ajabu mwenzao huyo ana gari, na nyumba moja anayoishi na mkewe, lakini kaka yangu na hao wenzake wengine wawili hawana nyumba kila mmoja kapanga tena mmoja namjua vizuri ni jirani yetu bado ni mtoto wamama, licha ya kumsema sema mwenzao. Jamani wakaka wote wa humu JF nawaombeni msiwe mnatusema sema hivyo sio vizuri, kuna wakati ushauri wetu una maana sana kuliko chochote! Muwage mnatusikiliza sio kutuponda!
 
Yup broda!
Ukijaribu kuwa beneti na mywife, basi kauli ndo hizo hapo juu!
Kwa ufupi unaonekana huna mpango kwa watu wako wa karibu!..huh!
my friend si kweli!uliza wapwaaz watakwambia!basi tu watu huwaga HAWAKOSI CHA KUONGEA
 
mkuu hapo kwenye red umeniacha kidogo.
Kwa ukweli ushauri wa mke si wa kupuuza but, lazima ujue wewe baba ndiye kichwa cha nyumba. Kichwa ndicho hufikiri. Hivyo ni lazima uanalyse ushauri kabla ya kuukubali moja kwa moja, vinginevyo unaweza ukachanganya mambo kama anavyoonyesha mkuu ndibalema hapo juu.

ilikuwa ni mistake. Nimesha'edit.
Sorry.
 
Bana Eeehh!! hata mwanaume mwenzio anaweza kukupa ushauri mbovu vile vile si lazima mwanamke. Muhimu wewe mwenyewe uwe na uwezo wa kupambanua zuri na baya hata kama utakuwa umeshauriwa na mkeo....
 
Nimesikitishwa sana na kauli nilizoanza kuzisikia sasa hivi kwamba ''JAMAA KASHIKWA NA MKE WAKE''!

wabongo bana,enewei
Yani unakubali kusikitishwa na simple minds? Si uwapotezeee tu? Raha jipe mwenyewe babu.Utakufa siku si zako!
"........Mwanaume atamuacha baba yake na mama yake na ataambatana na mkewe...."
As long as huyo mkeo ndiyo chaguo lako basi take it easy-dont mind
 
Nimesikitishwa sana na kauli nilizoanza kuzisikia sasa hivi kwamba ''JAMAA KASHIKWA NA MKE WAKE''!

wabongo bana,enewei

hao ni wanaume chipolopolo

manake mke mwenye kukushauri vizuri haiwezi kuchukuliwa kwamba eti ndo umewekwa kiganjani

kwanza ukitaka kujua utamu wa asali iweke kiganjani....

wale ambao wanakuwa hawana hekima ndo huwafanya waume zao ndondocha kwa njia za kishirikina, na wanaume wa hivyo kweli hawawezi kutoka au kufanya kitu

lakini wake zetu wanatushauri fresh, ikiwemo kukutana ma marafiki wengine ambapo tunapata pia ushauri mwingine kutoka pande zote mbili!
 
Back
Top Bottom