Unapoendesha nchi kijamaa, andaa tozo za kijamaa

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,885
Tuna miradi mikubwa ya kitaifa. Hii ikikamilika itasaidia wananchi wote kijamaa. Miradi kama SGR, bwawa la umeme, kiwanda cha dawa ni miradi ya kimkakati zaidi kuliko kujenga mashule vijijini. Hao wavijini waitwe kwenye harambe wafyatue matofali wajenge madarasa. Labda wachangiwe mabati, sementi etc

Hoja ya kuwa tozo kwenye miamala ya simu zitajenga hospitali na kununua madawa siyo sahahi kabisa.

Kwanza wako watu wengi wanatumia bima za afya, wanakatwa huko makazini hivyo hawaitaji kuchangia tena mfuko wa afya kununua dawa. Angesema zinaenda kujenga SGR au Bwawa la umeme hapo ningemwelewa sana.

Pili, kusema kuwa zitaenda kujenga mashule hili pia siyo sahihi maana kuna wazazi wengi wana watoto wao wanasoma private schools.

Pia wanaosomesha watoto private school wananyimwa mkopo wa HESLB. Sasa wachangie shule za kata ili iwe nini? Angesema zitaenda kujenga Bwawa la umeme na SGR, kiwanda cha dawa hapo ningemwelewa sana.

Kuendesha nchi ki-socialism unaitaji kutumia akili sana siyo kukurupuka.

Unapomwambia tajiri amchangie maskini you need to think twice.
 
Umeongea ukweli mtupu lakini tatzo serikali yenyewe inajiendesha kwa gharama kubwa na bado kuna mianya inayovuja ela, ndo maana wananchi tunakosa imani hata hio nyongeza itaenda kufanya kazi husika.
 
Jamaa wanatunyoosha kweli,halafu unaweza ona wananchi wanachanga hela ya kujenga kituo chá polisi
Nalog off
 
Back
Top Bottom