“Harufu Mbaya ya Upigaji Mradi wa Kufua Umeme wa Bwawa la Nyerere”

Apr 24, 2011
29
542
Ujenzi bwawa la Nyerere (JNHPP-MW2115) unagharimu Sh6.5 trilioni. CAG alipokwenda kukagua alikuta ujenzi umechelewa kwa 46.5%. Ujenzi ulitakiwa kukamilika June 2022, hadi sasa ujenzi upo 67%. Mkandarasi kalipwa (69.5%) fedha yake yote (Sh4.3 trilioni). Kuna mzozo wa Serikali na mkandarasi.

Mkandarasi anataka kuongezewa miaka mingine miwili na gharama na ujenzi wa JNHPP anasema utakamilika 2024. Mkandarasi anasema watengenezaji wa mitambo walijitoa, umeme pale site hautoshi, na njia ya kupeleka vifaa site ni mbaya, haipitiki. Mradi wa Sh6.5 trilioni una mazonge?

Serikali na mkandarasi wameunda Bodi ya Uamuzi wa Migogoro (DAB - Dispute adjudication Board) kupata suluhu ya mgogoro wao. Hili linaacha maswali. Serikali na mkandarasi hawakuwa na mkataba? Mradi ulitakiwa kukamilika June 2022 na mkandarasi hajakamilisha, mkataba unasema nini?

Mkandarasi wa mradi ni Arab Contractors na Elsewedy Electric kutoka Misri na msimamizi wa mradi ni TANESCO chini ya wizara ya Nishati. Mhandisi mkazi wa mradi kutoka TANESCO, ana uwezo wa kumkataa kiongozi wa wakandarasi. Kwanini hilo TANESCO hawajalifanya kama siyo wanufaika?

Mpango kazi wa mkandarasi (ambaye amelipwa Sh4.3 trilioni, ambayo ni 69.5% ya fedha ya mahitaji ya malipo kwa mkandarasi) ambao ameuwasilisha unaeleza sababu hizo na anaomba miaka miwili na nyongeza ya gharama. Serikali inasema imekubali kumuongeza mwaka mmoja. Kwanini? Hapa kuna harufu mbaya ya upigaji na rushwa.

Kwanini nasema kuna harufu ya upigaji na rushwa? Serikali badala ya kumlipa mkandarasi Sh4.3 trilioni (65.9% ya fedha za mahitaji ya mradi), serikali wamemlipa mkandarasi Sh4.43 trilioni. Wamemlipa ziada Sh113 bilioni. Sababu walizotoa, eti ni mabadiliko ya fedha za kigeni. Loh!

Sh113 bilioni ni vyumba vingapi vya madarasa? Nyumba ngapi za walimu? Vituo vingapi vya afya? Zahanati ngapi? Vifaa tiba na dawa kiasi gani? Serikali inakwenda kumlipa mkandarasi kama ziada wakitoa sababu za mabadiliko ya ubadilishaji viwango vya fedha za kigeni. Huu ni UJAMBAZI.

Tutumie hesabu za serikali kupitia TAMISEMI. Ujenzi wa kituo kimoja cha afya unagharimu Sh500 milioni. Hivyo katika Sh113 bilioni (fedha za walipa kodi) tunaweza kupata vituo 226 vya afya Tanzania. Halmashauri ya Mji wa Tarime, kata zote 8 hakuna Kituo cha afya. Hakuna.

Kama ujenzi wa chumba kimoja cha darasa unagharimu Sh10 milioni, Sh. 113,196,370,381 zingeliweza kujenga vyumba 11,319 vya madarasa. Lakini fedha hii amelipwa mkandarasi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere kwa kutumia maji ya Mto Rufiji (JNHPP), kwa sababu za hovyo tu.

113,196,370,381.06 analipwa mkandarasi kama ziada? Hapa walikaa chini wataalam wa sheria wa wizara ya Nishati na baba wa mikataba, Palamagamba Kabudi, wakapitisha kwamba ukitaka kumlipa mkandarasi, unapoteza mabilioni ya fedha kutokana na viwango vya kubadilisha fedha za kigeni?

Waziri wa Nishati, January Makamba, unaweza kujitokeza hadharani mbele ya umma, ukatueleza, ni kwanini mkandarasi Arab Contractors na Elsewedy Electric kutoka Misri wamelipwa ziada ya Sh113 bilioni kwa 65.9% tu ya ujenzi wa JNHPP? Je, atalipwa kiasi gani cha ziada katika 100%?

Bunge dhaifu la CCM limeshindwa kubaini mambo haya, limeshindwa kuunda kamati maalum kuchunguza upigaji huu na rushwa hizi katika Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere kwa kutumia maji ya Mto Rufiji (JNHPP). Hizi ni fedha zetu watanzania. Ni jasho letu. Mnaziita tozo na kodi.

July 5, 2021 TANESCO kupitia kwa Mhandishi wao, Mwanji Mhaka, walisema hadi kufikia Juni 2022 Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere kwa kutumia maji ya Mto Rufiji (JNHPP), bwawa lake litakuwa na mita za ujazo Bilioni 32.3 ili kuanza kuzalisha umeme. Hii leo ni November 2022.

Mradi mkubwa wa Sh6.5 trilioni uliotakiwa kukamilika June 2022 haujakamilika hadi November 2022 (na unaweza usikamilike) na bunge lipo kimya tu? Pamoja na kutokamilika, bado zimeanza porojo za upigaji, mkandarasi aongezewe muda na fedha. Hizi ni fedha za nani mnacheza nazo hivi?

Medard Kalemani akiwa waziri wa Nishati, mwaka 2021 alilieleza bunge kwamba, mkandarasi amelipwa Sh2.04 trilioni (100% ya mahitaji ya malipo yanayotakiwa kulipwa kwa mkandarasi). Hivyo alilipwa kwa wakati. Kwanini mradi haujakamilika June 2022 kama ilivyopangwa? Nani muongo?

Ndugu zetu CCM, hivi mmeingia madarakani kuwasaidia wananchi au mmeingia kwa malengo mengine? Wenzetu mnayo nchi nyingine tofauti na Tanzania ndiyo maana mnayafanya haya? Kwanini mnashindwa kuwa na huruma na Tanzania ambayo watu wake ni maskini na umaskini mmeuleta ninyi?

#MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila
 
Mradi mkubwa wa Sh6.5 trilioni uliotakiwa kukamilika June 2022 haujakamilika hadi November 2022 (na unaweza usikamilike) na bunge lipo kimya tu? Pamoja na kutokamilika, bado zimeanza porojo za upigaji, mkandarasi aongezewe muda na fedha. Hizi ni fedha za nani mnacheza nazo hivi?
Kuna mjumbe wa Kamati ya Bunge kwenye hilo eneo anatajwa huku

 
Back
Top Bottom