Unaoga mara ngapi kwa siku?

Kuoga ni tabia au mazoea hujengwa tangu utoto,waliokua wavivu wa kuoga utotoni hata wakiwa wakubwa hali huwa hivyo hivyo na kinyume chake husadifu ukubwani.

Je wewe unaoga mara ngapi kwa siku? au waoga kila ukichafuka?
Inategemea na kazi na maeneo uliopo kama Mbeya,Njombe,Kilimanjaro,Arusha ,nk,kuanzia mwezi huu hilo baridi unweza kupiga wiki ni mwendo wa passportsize!
 
Mbili tu inatosha, Asubh na jioni

Msimu Kama huu wa baridi Ni Mara moja tu.
 
Kuoga ni tabia au mazoea hujengwa tangu utoto, waliokua wavivu wa kuoga utotoni hata wakiwa wakubwa hali huwa hivyo hivyo na kinyume chake husadifu ukubwani.

Je, wewe unaoga mara ngapi kwa siku? Au waoga kila ukichafuka?

Mimi huwa siogi bali huwa nina nawa sehemu muhimu tu.
 
Umenichekesha sana.
Ila uko sahihi. Wakati nasoma primary tulikuwa na ticha kumbe alikuwa na mental health issues. Akatuambia ukitaka uwe na ngozi nzuri sana, usipate chunusi oga 3x a day. Na tulikuwa na lunch break ya kama 1.5 hrs. Nilianza kuoga lunch time, mpaka leo nikipata chance naoga mchana. Yaani kuoga inanipa raha fulani hivi hata haielezeki aisee.
Nilipokuwa mdogo nilikuwa mtata sana kuoga aisee, hii biashara ya kuoga oga ilikuwa ngumu sana kwangu, na popote nilipopata nafasi nilipiga ndefu na maza akijipindua naingia bafuni nafungulia maji weeeeeeeee nikiwa pembeni kisha najipaka maji natoka au pakitokea ugomvi au kasheshe yoyote na maza siogi! akinichapa namweleza wazi siogiii unajifanya kunichapa?

Ila mbona tangu nimekuwa mkubwa aisee naoga vibaya sana, sina tatizo kabisa na kuoga hata mara 3 kwa siku sioni shida

Nakupinga mkuu kuwa ukiwa mvivu wa kuoga utotoni itaendelea hadi ukubwani

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Aisee mi kuoga maxmum ni mara moja tu kwa siku baasii. Siku nikioga mara mbili daah inakuaga siku ya kipekee sana na ni mara chache mno imetokea maishani mwangu na hazifiki hata kumi.

Nikiwa sehemu yenye baridi ndio kabisaa hata 1 week inakata afu fresh tu.
Nikiwa advance nilikua nasoma shule ya uko nyanda za juu kusini, ebana kuna baridi la kufa mtu, kuoga ilikua ni kwa mbinde saaana, kuna mwamba hadi term inaisha kaoga mala 2 tu.
 
Back
Top Bottom