Unamtext mtu message ndefu yeye anakujibu "K"

Unamtext mtu message ndefu yeye anakujibu "K"

Ni kama nisivyopenda maneno 'lol' mara limao sjui 'lmao' kuonesha kwamba mtu kafurahia au msg imemchekesha!
 
hao limbukeni tu, haina haja ya kupindisha maneno.
Mtu anaandika y ukiuliza unamaana gani ,yes au nini anakujibu ana maana why.
Inakubid uanze kuitafakari message kama upo kwenye mtihani vile na hapo unapoteza muda maana upo busy muda wote.
 
Kweli mkuu, ni kama kadharau flani hivi...

Sio ni kama dharau, ni dharau period. Haiwezekani mi njipinde kutoa maelezo yanaohitaji mrejesho afu mtu anajibu..., K
Huwa naangalia nabaki kucheka tu, tamthlia zimeharibu sana baadhi ya watazamaji wake.


Sent from my iPhone using JamiiForums app.
 
Aise kuna watu wa ajabu sana hii karne ya 21!


Lets say ulikua bafuni unaoga, ulivyotoka ukakuta missed call kama 4 hivi kutoka kwa mshkaji wako, ulipotaka kumpigia ukakuta huna salio ikabidi umtext.


"Oya kaka pole nilikua washroom nimekuta missed call zako vp kwema?" kama una airtime pls call me again", sasa maneno yote haya ni KB (Kilobytes) nyingi tu!


Jitu linakujibu "K", sasa maana ya "K" ni kenge, kongosho, kunguru, kinyeba au? acheni ukisasa wa ajabu bwana! hata kama "K" ni kifupi cha "ok", yet, uandishi wa namna hii haufai ukizingatia kwamba msg niliyokutumia inahitaji maelezo ya ziada!

Aisee nilifikiri peke yangu ndo sipendi mtu aniandikie message kwa vifupisho vya ajabu ni sawa sawa na wanaoweka 'x' badala 's' wananichefua
 
Eti mwingne anakuandikia P ,badala ya poa,.nikajiulza hyo p ni popo,punga au pumbu?
 
mikazó;8708028 said:
Eti mwingne anakuandikia P ,badala ya poa,.nikajiulza hyo p ni popo,punga au pumbu?

Hahahahaha mkuu umenichekesha sana!
 
Nikijaribu kuwasoma huwa nahisi hivi kama nimejibiwa hivyo
K - Not interested
OK - Slightly interested
Okay - Interested
 
Back
Top Bottom