Unampenda lakini hakupendi

Hii kitu imenisaidia sana. Unakuta mtu sio kwamba anatisha sana au vipi lakini basi unajisikia kuwa connected nae sana. Ukimwona unatamani umwangalie, unapenda alivyo, pozi zake,upole wake na anavyoongea n.k Sasa unapoamua kukiri hisia zako kwake na akajua unavyompenda, hayo mashauzi sasa! Mpaka vile vigezo vilivyokufanya uvutiwe nae mwanzoni, vinakuwa havina maana tena maana unaanza kumwona yuko tofauti na ulivyomchukulia.
Upande wa pili, Ukiachana na swala la kuvutiwa na tabia, hata akiwa mzuri sana, yale manyanyaso unayokutana nayo, yanakufanya umwone kama takataka ya jalalani kabisa. Maana ni kama ana enjoy kukufanyia vituko au hathamini ubinadamu ulionao, ukilalamika wenzie watamtetea kuwa anakupima aone tabia yako. Wengine watakwambia, huyo hakupendi ndio maana anakufanyia hayo. Cha ajabu hakwambii kuwa hakutaki ili uendelee na mambo yako, bali anaendelea kukuzinguazingua huku ukibakia bila ufahamu wa status yako ya kimahusiano. Sasa mtu kama huyo unamfuga wa nini?:
Kuna mwingine, unakuwa nae katika relationship baada ya kumfukuzia sana. Ukiangalia, alikusumbua mno, mkianza mahusiano unatarajia atabadilika na kushow some maturity,lakini inakuwa kinyume chake. Ni kama wewe ni baba na yeye ni mtoto wa mwisho. Utaonyeshwa deko, visa plus vituko kila anapojisikia. Ndio hayo ya kutokujibu sms, kutopokea simu na kutoeleweka anataka nini katika uhusiano maana huwezi kuelewa anataka muachane au uhusiano uendelee.
Sasa, unadumu vipi katika uhusiano na mtu wa hivyo? Huwa najitahidi kuwa mjinga ila mara zote nakwama kabisa aisee.
Wakati nikiwa bado mshamba wa mapenzi, kulikuwa na kabinti nilikapenda ambako kalikuwa kakiishi mtaa niliokuwa nikiishi.
Sio siri, yule binti alikuwa mzuri sana isipokuwa alitokea tu kwenye familia yenye maisha ya kawaida sana.
Basi, kwa akili zangu, nikawa napanga mengi sana juu ya yule binti kama uhusiano wa kudumu,ndoa n.k Nilipoona umefika muda mwafaka, nikaona nijitose. Nachojipendea mimi ni kuwa, sijawahi kushindwa kujieleza kwa mwanamke toka nikiwa bado mdogo sana kiumri na kuna wakati wazazi wangu walipokuwa wakizikamata barua zangu za mapenzi na wakiangalia umri wangu, walikuwa hawaamini kama naweza kuandika matured stuff kiasi kile.
Tukirudi kwenye stori. Nikamvaa dada na kutiririka yote bila kumficha na niliona kanielewa sana. Nikatarajia tu nitajibiwa moja kwa moja kuwa nimekubaliwa au sijakubaliwa hata kwa sms tu. Hilo sikuliona. Nikituma sms, inajibiwa kwa mkato tu. Siku akikuuliza yeye kwa text, uko wapi? Kinachofuata ni matatizo tu, mama mkubwa anaumwa, shangazi ameniambia nimfuate Arusha kuna hili na lile. Mara nina wageni, nitumie hela ya Taxi iwalete nyumbani.
Mpaka hapo sijui mimi ni nani kwake. Nikawa mpole sana na kumvuta kwa ukaribu na kwa kiasi fulani nilifanikiwa ila baadae nikagundua mwenzangu hayuko kimahaba zaidi na amewekeza zaidi katika misaada yaani ananifanya mimi kama side kick fulani hivi. Nikaamua kupunguza misaada. Hapo ndipo nilipouona moto. Ndio ikawa nikipiga simu sijui ndio haiangaliwi kabisa? Nikitext najibiwa baada ya siku mbili.
Nikaona huu ni ujinga na kuamua kukaa kimya pia, nikafuta namba zake. Kipindi hicho picha tunatumiana kwa email, na yenyewe nikaifuta. Alipoona changes, nikaona anaanza kujirudirudi,but it was too late. Nilishamtambua yeye ni mtu wa aima gani na sikuwa na hamu nae tena. Baadae Dada yake akaja kunieleza kwa kirefu kuwa alikuwa na mwanaume wake Oman, hakuzoea kudate na wabongo. Nikasema Pambafff, arudi huko basi!
 
Tuwekee hiyo link ya uzi huo
 
Thnx mkuu
 
Nipo kazini mkuu nitalifanyia kazi mkuu i promise
 
Hahaha
Nakumbukaga nyimbo mbili

Nalivua pendo wa mwasiti
Utanikumbuka wa vumilia

These songs, ni nzuri saana ukipata madhila kama haya
Sipati picha mnavyopelekwa pelekwa poleni asiee ukiona haelekei achana nae tatfa mwanamke mwingine tulivyojaa hivi
 
Ama nilipitiwa na ucngizi? Other time she said nilimpa sister cm aingie internet(a google)
 
Kosa kubwa sana hili vijana wa kiumeni na kikeni hufanya,mapenzi sio kama kusubiria mvua useme itanyesha tena unaweka ndoo za maji kutegeshea kukinga maji ya mvua..................
 
I better say to hell na hawa viumbe
 
kuanzia anza kutongoza mwanamke mwingne wa kukeep busy au labda ulikua haumpi hela mana sisi ukiwa mbahili utafanyiwa vituko mpk uondoke mwenywe
Hela natoa haswa na sio chini ya elfu 70000 kwa wiki hiyo ni yakumtoa kwenye vishawishi na hapo dada yangu she as not telling me if she needs some amount of money what if she tells me imagine of that? Nikaona hilo sio tatizo navyo chat hapa ss nilikuwa nampango nimfungulie kitega uchumi chochote ifikapo mwakani sio chini ya 5M ila ndio hivyo aleti ushirikiano wowote nami for sure mm binafsi si mwelewi adi ss naninatamani hawe future yangu na sio kupitapita japa mda unanirusu sanaa tu kula ujana ila naamini as Gentleman hupaswi kurukaruka km njiwa. Nikitaka kuvhat nae haitapita dak5 ameshatoa sababu ya kufanya kitu kingine ile chatting moment inapotezewa tu hivyo ooooooh, sipendagi kuchat na simu na au kutokatoka.
 
achana nae uyo kaka utakua chizi bure usipoangalia tafta mwanamke mwingne atakaekua na hisia na ww uyo hakufai
 
Kuna bro angu alisomesha demu toka msingi

Nikawa namchana huyo mtoto hakufai mwisho nikapotezea maana alikuwa hana akili angenichomesha kwa wakwe zake

Sikaja kumuoa haha haha ndoa hata miezi mitano haikufika Dogo full kumtishia visu akitaka tendo la ndoa

Siku moja kaja kunipigia simu nimshauri nini nikamwambia tuuuu ushauri nilishakupa kilichobaki subiri akuchome kisu ufe
 
[emoji28][emoji28][emoji28]
 
aaaaaaa mpotezee tafta pesa wanakuja wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…