Sitasahau,ni baada ya kumaliza kidato cha nne pale Azania miaka ishirini na mbili iliyopita mzee akaniambia sasa mwanangu umekua inabidi uende ukafanye biashara wakati unasubiri matokeo yako ya mtihani,na akanikabidhi kama milioni tatu za mtaji.Nikaelekea wilayani Mpanda ili kukusanya mbao na kusafirisha kupeleka Dar.Kufika huko nikafikia nyumbani kwa kaka yangu aliyekuwa na kabekitatu karembo kwelikweli,basi ile sijamaliza hata siku tatu nikashikwa na maleria kali kutokana na hali ya hewa nisiyoizoea,kaka yangu akamwambia binti kuwa hakikisha unamhudumia kaka yako mpaka apate nafuu,basi kaka yangu alikuwa anashangaa tu,mbona mgonjwa kadri siku zinavyoenda ndio hali yake inazidi kuwa mbaya au matibabu sio mazuri, kumbe muhudumiaji wangu alikuwa ameshagundua hazina na sasa hivi tunavyoongea uzao wa mchezo huo umeshatimiza miaka 21....