Unamiliki nini katika Umri huu?

Unamiliki nini katika Umri huu?

Kuku
Baiskeli
Tv
Sofa moja
Chumba cha kupanga
Laptop
Printer
Watoto 6
Mke 1
Wazazi wenzangu 2


"corona ipo tuchukue tahadhari"
 
29,vyote ulivyotaja and more nadhan faida ya kuingia ndoan mapema mwenzi mzuri anakufunga speed governor
 
Teh teh we jamaa sio ahaaaaaaa
Nina miaka 23.

Namiliki grupu la whatsapp la PachuPachu, Msingi Kiuno, na ZaUchiZoteHapa.

Nina sabwufa limeharibika sehemu ya flash na pini ya waya imekatikia kwenye tundu.

Nasikia nilikabidhiwa viwanja kijijini kwetu ila sijawahi hata kuviona na kwenda kijijini sitaki.

Nina wanawake wanne wa kudumu na watatu ni occasional.

Sina chumba wala nyumba nalala kwa rafiki yangu Dilongele.

Nina elimu kidogo ya form six.

Pia nina nyege.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WEWE MWENYE NYUMBA TAYAR HONGERA

Mimi nina gari 1 ya kutembelea kwa sasa ila kuna jingine natarajia kununua nyumba haijakamilika bado, nimepanga nyumba nzima nalipa kodi mwenyewe laki 3 kwa mwezi nina simu 5 samsung galaxy s8 plus,nina iphone 7, vitochi viwili vya batani vya tecno, na nokia na pia nina tecno cammon Cx
FRIJI NINAYO LG, TV NINAZO MBILI SINGSUNG INCH 25 FLAT CHUMBANI, Sebuleni nimeweka StarX, dish nina azam na dstv, Vitanda vitatu 6×6 , 5×6 zipo mbili nina saloon 2, sebuleni nina sofa jikoni nina jiko la gas, na kubwa la kerosene, nina mpango pia wa kufungua duka la nguo za kiume za kimodeling zinazoenda na wakati
Yaani ndo hichi nilichojaaliwa na mungu mpaka sasa
Namiliki Jahazi la uvuvi wake watatu nyumba moja Mbweni Njia panda ya ulaya pia namiliki busha lenye kilo 13 na bendera ya TANU pia na Ungo wa kurukia usiku na shamba la minaziView attachment 1410571

Sent using Jamii Forums mobile app
me ni tajiri kumbe nina watoto watatu
nina viwanja vitatu Moshi Lushoto na Mkuranga nina fanya biashara ya pooltable, samaki na pikipiki(bodaboda)

kwa siku naingiza si chini ya 50

Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka 58
Mke mmoja watoto wa ndoa 6
Watoto wa pembeni 5 niliwachukuaga ninao home - jumla ya watoto 11
Nina kiwanja...tofali zipo site mwaka wa pili sasa ila kupandisha mambo yamegoma
Nimepanga nyumba nzima...Tandare kwa Mtogole
Sijawahi kumiliki gari...ila nina pikipiki wa ajili ya safari zangu na familia
Nina kibarua Tshs 540,000 kwa mwezi
Watoto 3 wasichana wamezalia home....wapo
Watoto wengine 3 wa kiume, mmoja Dj kwenye bar, Mwingine bodaboda na mwingine yupo home tu hata sijui shughuli zake
Shemeji zangu wawili kaka za wife nipo nao, mmoja dereva wa daladala, mwingine bajaji wana wake zao..wote tunao home
Wadogo wa wife wasichana wamemaliza la saba mwaka jana, ninao home pia - mmoja anajifunza cherehani na mwingine anafanya kazi ya kibanda cha Tigo / Mpesa -
Nina wadogo zangu wawili wa mwisho, wote wanasoma VETA changombe - ufundi magari.
Watoto wengine bado wapo shule......kayumba sina uwezo wa kuwapeleka FM Academia.
Kila ikifika jioni tunakutana wote - tunafanya donee ili tuweze kuwa ha hela ya kuhemea siku inayofuata, kulipa umeme na maji.

Cha moto nakipata !!! na Corona hii kukaa home kichwa kinaumaa!!
we mwamba kiboko una roho nzuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
22 years old namiliki hp laptop pressario CQ56,kitanda na godoro 5*6 jiko la gesi mtungi wa kg 29.5 taifa gesi, simu smart 4g, sabufa kubwa sea peano,kabati la nguo, music,movies libraly and stationaries, samsung full hd flatscreen with 32 inches, big and muscular body special for cute girls
 
Mimi mwamume umri 35,Namiliki wake wawili watoto wanne,vitanda 5 na godoro zake Sina nyumba sina gari sina kiwanja,sina kazi,sina pesa Natunzwa tu na wake zangu.Kwa sasa hivi natafuta mke wa tatu awe na miaka 30 anayejiweza.
Hahaaa
 
Nina 30, namiliki nyumba mbili moja ipo kibaha kwa mathias, nyingne ipo morogoro nane nane, nina gari nne (ranger nyeusi, harrier, noah , na spacio), sina mke, sina mtoto, sasa hvi najenga ghorofa moja kimara, nina mashamba ekari 22, nina biashara yangu kubwa tu ambayo inasogeza siku, ni machine za kusaga za kukoboa, nina viwanja viwili. Katika elimu nina degree moja, na sasa hv ninatarajia kusoma masters kwaajili ya sifa tu, si unajua sisi wahaya. Ni hayo tu.
Hahaaa
 
Dash....Nina 78yrs...jobless...jinzi 2...tisheti 4 ...madem 6 wa JF...niwataje?...naishi kwa shemeji ..
 
Umri wangu ni miaka 40..
Namiliki baiskeli moja aina ya swala,
Kichwa cha cherehani cha singer,
Stuli 3 na ngoma kubwa za ngozi,,
Kitanda cha kasuku 4/6,
Godoro na mito 2 ya Sufi..
Maua ya plastic 3,
Feni moja Philips,,
Radio aina ya Sanyo,
Pasi ya mkaa,,
Jiko la stove,
Taa ya kandili,,
Kabati la vyombo ,,droo zake zipo juu pembeni lina nyavu..
Kombe kubwa la bati,,
Ndoo 3 za bati,,
Kandambili za mgogo pair 1..
 
Nina miaka 23 mwakani hapo mwezi february natimiza 24....Ni kijana mtanashati (Me) ambaye kiasi kikubwa cha fedha za kujipa huo umaridadi nategemea kwenye kubet,sina kazi,sina demu ,sina mke,sina maisha nayasikia tu kwa wenzangu kikubwa namiliki smartphone used (Tecno Pouvoir 2),saa ya shillingi elfu 3,nguo kibao sijui thamani yake inafikia shillingi ngapi,pia namiliki vitabu na mapamphlets ambayo niliyanunua mwenyewe kwa pesa zangu za kubet kipindi nasoma .....Now nasubiri tu matokeo ya kidato cha sita angalau niongeze kumiliki cheti kingine ukiachana na hivi ninavyomiliki (cheti cha kuzaliwa na cha form four)


Juzi kati nilikuwa namiliki elfu 5 tigopesa nimewalipa RITA waverify cheti changu till now sijarudishiwa majibu(Huenda nikamiliki na cheti cha kuzaliwa ambacho kipo verified na RITA kwa pesa niliyolipia mimi mwenyewe).

Ningependa kumiliki pesa nyingi,uhai usio na kikomo pamoja na mvuto katika kila aspect ya maisha haya


Note: Nahitaji kuomba mkopo pale Helsb ila sina 30k mwenye ako na franga kunisaidia akuje PM....Naishi maisha ya kipato cha chini ila sijasajiliwa kwenye mfuko wa TASAF
 
Nina miaka 30 namiliki Nyumba tatu...Magari ya mizigo 10 na Gari binafsi mbili moja ya wife vipi inatosha au nieongeze vingine kambuyaya mimi??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom