- Thread starter
- #41
Kongosho,Duh, hii ni nyanja nyingine ambayo ni pasua kichwa sana.
Ili umsaidie mtu, lazima na yeye ajitambue ndipo mtu mwingine waweza msaidia.
Unakuta mwingine hataki kabisa kujiendeleza na hayuko tayari, inakuwa ngumu sana kumsaidia.
Suala la kumwekea akiba ya uzeeni, kinadharia linawezekana ila kiuhalisia ni gumu. Mshahara wa wewe mwenyewe uliyemwajiri kukufikisha mwisho wa mwezi ni kwa mawazo, sasa utakumbuka NSSF ya msaidizi wa home? Achia mbali mshahara?
Kwa sabau huduma nyingi anapata hapo hapo nyumbani si mbaya ukakata sehemu ya mshahara kila mwezi ambayo utamwekea akiba ili mkataba wake unapokatika awe na kiasi cha kufikia kwao. Ni vema kumfungulia akaunti ili kiasi hicho kiwe kinaingia benki moja kwa moja. Katika hili ni vema umshirikishe yeye japo unatakiwa kukaa na kadi yake ya benki ili ku-control matumizi yake.