Unam-treat FAIRLY house girl wako? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unam-treat FAIRLY house girl wako?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mkeshaji, Mar 8, 2012.

 1. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hebu tujadili hili wana MMU,
  House girl ni mtu muhimu sana katika nyumba.

  Umuhimu wake ni pamoja na:
  -Kukusaidia/kukufanyia kazi za nyumbani.

  -Kukulindia nyumba pindi unapokuwa kazini.

  -Kuhudumia watoto/familia yako hata/hasa pale ambapo haupo nyumbani........na mengine mengi mengi yasiyo idadi.

  Kwa hiyo tunakubaliana kuwa huyu ni mtu muhimu sana kwako na kwa familia yako.

  Sasa swali linakuja:
  Hivi housegirl wako unampa treatment zinazostahili kweli?

  -Unakula naye meza moja na chakula kimoja kama unachokula wewe, au ndo vile tena wewe na familia yako mnakula mapochopocho hapo dining room wakati yeye mnamfutika huko stoo akila makombo?

  -Analala mahali panapostahili, au ndo kumweka sebuleni mbu wakimmaliza.

  Umempa mkataba wa uhakika kwa mujibu wa sheria za kazi?
  -Unamlipa mshahara unaostahili na kumwekea akiba ya uzeeni?
  -Unampa bima ya afya na matibabu ya kiutu?
  -Unampa likizo ya siku 28 kila mwaka?

  -Unampatia elimu stahiki? Kumbuka wengi wameingia kwenye kazi hiyo kwa sababu hawakupata fursa ya kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali nyingi zikiwa za kiuchumi, lakini si kwamba hawana uwezo kiakili. Au unamtumia tu kama toiletipepa?

  -Humpi manyanyaso ya kumfokeafokea bila sababu maalum?

  -Unampa mapumziko yanayostahili au ndo vile akiamka saa kumi analala saa saba.

  -Unaporudi kazini anakufurahia kama baba/mama au ndo anakereka kwa kujua muda wa kukaa kwa hofu umefika sasa.

  -Unamsaidia kazi pale panapostahili?

  -Mara moja moja unamnunulia japo mavazi na kumfanya kama mmoja wa familia yako? Au ndo vile tena gauni refu hadi linaburuza chini, kila siku hilo hilo....

  Hebu tujadili haya kwanza.
   
 2. zimwimtu

  zimwimtu JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 1,887
  Likes Received: 609
  Trophy Points: 280
  mmmmh... siredi nzuri, ngoja waje wenyewe.. mie bado single, and home alone.
   
 3. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mi namtreat fair sana aisee.
   
 4. Zabibu

  Zabibu JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  asante kwa kulileta hili hapa,nina ndugu yangu mmoja ivi ana tabia ya kumnyanyasa msaidizi wake wa kazi kila saa anamgombeza na kumpiga makwenzi na vibao bila hata sababu ya msingi,mara ampimie chakula,asiingie sebuleni yaan vitu vya ajabu ajabu tu na ukimuuliza kwanini anamfanyia ivo mtoto wa watu ana msemo wake "fuata yaliyo kuleta".afu anamlipa mshahara elfu kumi wakati anafanya kazi nyingi kweli.Jamani hii sio tabia nzuri kabisa sijui wanawake wengine wakoje?
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  namtreat fair sana, ila wengine ni makauzu ile mbaya................

  Akiumwa ni juu yangu...
  Kila jumamosi yupo free....
  Nimemfungulia akaunti bank napitisha mshahara wake huko......
  Likizo anapata........
  Nashirikiana nae kufanya kazi.....

  Malipo ya uzeeni...hapana
  shule?......... Angalau akae nami miaka 3.... Huku nikiangalia mwenendo wake, maana nimemuuliza anapenda kufanya nini baadae, pia inategemea na umri wa watoto.....
   
 6. k

  kisukari JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  kwa kweli huu ni unyanyasaji wa hali ya juu.dada wa watu kwa kukimbilia hana.inasikitisha mno
   
 7. k

  kisukari JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  house girl wetu,yupo tangu 2002,kwa kweli ni kama mmoja wa familia yetu.ndugu zake huwa wanakuja kutembea wanafikia nyumbani.alizaa,pale pale nyumbani yupo na mtoto wake.mshahara ninaompa,anamsomesha mdogo wake,baba yao alisema hasomeshi mtoto wa kike.na ni mtoto mwenye tabia nzuri mno.kuhusu zawadi namnunulia sana tu.na mshahara wake namlipa wa miezi minne kwa mkupuo,ili afanyie mambo yake.likizo yake kila dec,huwa anaenda kwao.na hela ninayomlipa,ni nyingi tu kwani ni mdada ambae anaishi vizuri sana na mama
   
 8. s

  sawabho JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Tuliye naye sasa ana mwezi mmoja tangu tuanze kuwa naye, lakini ni sehemu ya familia kuazia mezani, afya mpaka mavazi. Aliyeondoka kaondoka na mafunzo ya kushona na tumemnunulia cherehani ili aanzishe maisha yake. Alipokuwa akienda likizo tulikuwa tunampatia nauli ya kwenda na kurudi, tofauti na mshahara wake. Kuhusu akiba ya uzeeni hatuwawekei kwa sababu hatutajii kukaa nao mpaka wafikishe miaka 60 ya kustaafu. Ila wanaokaa na sisi vizuri, akimaliza kazi mchana anaenda shule, mwisho anaondoka na ujuzi aliouchagua wenyewe.
   
 9. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Hebu tujadili hili wana MMU,
  House girl ni mtu muhimu sana katika nyumba.

  Umuhimu wake ni pamoja na:
  -Kukusaidia/kukufanyia kazi za nyumbani.

  Agreed

  -Kukulindia nyumba pindi unapokuwa kazini.

  Agreed

  -Kuhudumia watoto/familia yako hata/hasa pale ambapo haupo nyumbani........na mengine mengi mengi yasiyo idadi.

  Agreed ingawa sikai na mtoto wala familia (ni mimi na yeye tu)

  Kwa hiyo tunakubaliana kuwa huyu ni mtu muhimu sana kwako na kwa familia yako.

  Agreed 100%
  Sasa swali linakuja:
  Hivi housegirl wako unampa treatment zinazostahili kweli?

  -Unakula naye meza moja na chakula kimoja kama unachokula wewe, au ndo vile tena wewe na familia yako mnakula mapochopocho hapo dining room wakati yeye mnamfutika huko stoo akila makombo?

  Anakula muda tofauti na wangu, na anakula (pika) chakula anachotaka yeye.

  -Analala mahali panapostahili, au ndo kumweka sebuleni mbu wakimmaliza.

  Analala chumba cha peke yake na kitanda size 6X6 cha mti wa mninga na godolo dodoma while l sleep on 5X6 bed


  Umempa mkataba wa uhakika kwa mujibu wa sheria za kazi?
  -Unamlipa mshahara unaostahili na kumwekea akiba ya uzeeni?

  Namlipa zaidi ya kiwango kilicho wekwa na serikali kwa msaidizi unayemlisha, mlaza, mtibu cha 23,700TZS; simuwekei akiba ya uzeeni

  -Unampa bima ya afya na matibabu ya kiutu?

  Anatibiwa ninapotibiwa mimi


  -Unampa likizo ya siku 28 kila mwaka?

  Ya siku 30

  -Unampatia elimu stahiki? Kumbuka wengi wameingia kwenye kazi hiyo kwa sababu hawakupata fursa ya kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali nyingi zikiwa za kiuchumi, lakini si kwamba hawana uwezo kiakili. Au unamtumia tu kama toiletipepa?

  Nimempa elimu ya kupika na kutunza nyumba, kushona kwa kutumia cherehani, ya dini (anatarajjiwa kubatizwa hivi karibuni)

  -Humpi manyanyaso ya kumfokeafokea bila sababu maalum?

  Mimi ni mvivu wa kuongea, so nikilazimika kusema ninasema naye

  -Unampa mapumziko yanayostahili au ndo vile akiamka saa kumi analala saa saba.

  Anajipangia kazi na muda wake mwenyewe, muda mwingi sipo

  -Unaporudi kazini anakufurahia kama baba/mama au ndo anakereka kwa kujua muda wa kukaa kwa hofu umefika sasa.

  Nikisafiri ananitumia sms za kunimiss

  -Unamsaidia kazi pale panapostahili?

  Ninapika mara chake kwa lengo la kutry new recipes na si kumsaidia

  -Mara moja moja unamnunulia japo mavazi na kumfanya kama mmoja wa familia yako? Au ndo vile tena gauni refu hadi linaburuza chini, kila siku hilo hilo....

  Kila siku kuu, na ocassionaly nikiona kitu kitakachompendeza

  Hebu tujadili haya kwanza.

  Roger that
   
 10. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Si vibaya ukashiriki japo kwa kusikiliza ili pindi na wewe utakapokuwa unaishi na hawa ndugu zetu basi ujue jinsi gani ya kuishi nao huku ukiwapa haki zao stahiki kama wasaidizi lakini zaidi kama binadamu sawa na wewe.
   
 11. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wengine wanapenda sana kunyanyasa binadamu wenzao.
  Wanasahau kuwa hata wao wanaweza kunyanyaswa na watu wengine katika maeneo tofauti. Kabla hujamfanyia mwezio baya, jaribu kujiweka kwenye nafasi yake...utajisikiaje?
   
 12. M

  MandawaNaManenge Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Asante kwa thread hii njema ambayo inatupa muda wa kujitathmini.
  Mie ( japo sio kama naji chest-thump) naamini ni mmoja kati ya waajiri fair.

  Namtreat vizuri kwa kweli , kutokana na feedback ninayopata toka kwake, ndugu zake na ndugu zangu.
  Mshahara namlipa vizuri mno maana natambua naye ana majukumu katika familia yao na pia kwa kujua kuwa hivyo alivyo ningeweza kuwa ni mimi kama tu si rehema za Mungu. Kwahiyo huwa ninaipokea hali niliyo nayo kwa shukrani na kumrudishia Mungu shukrani kwa kuwatendea wengine , akiwemo yeye mdada mema.

  Mshahara ni 100k+. Na pia kwao wazazi wake niliwanunulia simu ili waweze kuwa wanawasiliana na mwana wao bila kwenda kugonga kwa jirani na kila akienda likizo ( usually annually unless akatae mwenyewe - kama mfano mwaka jana alikataa) akienda nawafungashia vitu.
  Anapika atakacho, na ni fundi kweli kweli. Mavazi namnunulia kama mwanangu. Ukimkuta kwanza huwezi amini ni Hg.

  Kiukweli, tuwaenzi hawa madada maana wanaleta sanity katika maisha yetu na tukumbuke kuwa nchi zingine huduma kama hizi ni kama unaffordable, but hapa kwetu walau bado tunaweza wapata, japo si kama kwa urahisi uliokuwapo nyuma.
  N.B: Nimekaa naye miaka saba na nimemsomesha amesiti mtihani wa QT mwaka jana. Asanteni.
  Na cha kuchekesha ( mie hunichekesha sijui kama nanyi wajuvi mtaliona hilo la kuchekesha) wazazi wake walini'susia' sort of , ( positively though)
  wakasema huyu sasa ni mwanangu maana wao hawadhani kama wataweza tena kumlea kama nimleavyo. Kwahiyo hata akipata mchumba, nijue ni jukumu langu wao watakuja tu kama wageni waalikwa. Tehe
   
 13. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hii imetulia.
  Ni lazima tukumbuke kuwa hawa ni binadamu wenzetu, na wana haki kama tunavyodhani tuna haki sisi. Hivyo tusiwanyanyapae, tuwape haki zao stahiki na kuwa-treat kama vile ambavyo tungependa sisi tuwe treated.
   
 14. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nzuri sana hii.
  Hongera!
   
 15. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ok, endeleeni hivyo hivyo na Mwenyezi Mungu atawabariki. Mnafanya kazi nzuri sana.
   
 16. S

  Shekispia JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Salute to thoze who doent mistreat their housekeeperz..
   
 17. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  alizalia kwako bado useme anatabia njema anyway
  hongera kwa kulelea mtoto wa dume mwingine
  nakupongeza kwa moyo huo
   
 18. K

  Konya JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hawa watu(mahg) wanakutana na changamoto au matatizo mengi,kuna case moja niliishuhudia miezi kadhaa iliyopita..nilikuwa kwenye hotel moja ivi maeneo flani,nilikuwa napata lunch,pembeni yangu kulikuwa na familia moja yenye asili ya kiasia walikuwa wanapata lunch na wenyewe,walikuwa na mdada ambaye ana asili ya kibantu,alikuwa kampakata mtoto wa kama miaka 2-4 ivi mtoto mwenyewe naye alikuwa na asili ya kiasia,kilicho nikera ni wale member wa ile familia kuconcentrate na kula,kunywa na stori huku waki muignore yule binti kabisa kama hawakuwa naye vile na mbaya zaidi alikuwa anasumbuliwa mno na yule mtoto aliyekuwa amemshika na hakupata msaada wowote kutoka kwa member wa ile familia kumbembeleza na yale mamisosi yote walikuwa wamejirundikia wao tu yule binti akawa na bite2 tu anatafuna na ukiangalia nguo zake alizovaa mmh ilikuwa ni aibu kwa mazingira yale,ilinikera mno nikareflect enzi zile za utumwa ndo nikachoka kabisa kuendelea kuwepo maeneo yale iliniuma sana kiukweli walichokuwa wanamfanyia yule mdada.
   
 19. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Mi wangu siku moja moja nampa upendeleo wa kulala kitanda kimoja na mimi.
  MP.
   
 20. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Mimi nilkuwa naye nikawa namlipa 50,000 kwa mwezi kula kulala na mengine yote kasoro sex kwangu, lakini wapi bwana. Ndege wengine hawafugiki kwa kweli.
   
Loading...