Zijue aina mbalimbali za wake!

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
1. MKE SHEREHE (party wife)
Hawa muda wote wanawaza sherehe na starehe tu, utawasikia kesho sendoff, birthday, graduation, mara kitchen party. Wako tayari kutumia hela ya chakula kwa ajili ya kununua viwalo, vipodozi, kutengeneza nywele, kuchangia sherehe.

2. MKE KAMUSI (dictionary wife)
Hawa ni aina ya wanawake ambao huamini mawazo yao tu huwa hawapendi kushauriwa na ni wabishi sana, huwa hawajali hata mume wake anasema nini.

3. MKE PAMPAS (pampas wife)
Hawa ni wavivu sana na wameharibiwa na familia zao, hasa familia tajiri, hawawezi fanya kazi yoyote wanatuma hovyo hata waume zao utasikia baby nipe hicho, baby njoo unitolee hiki. Kama kuna house girl au boy ni zaid ya punda kwao.

4. MKE OFISI (The office wife)
Hawa husahau kabisa majukumu yao kwa kisingizio cha kazi, wanajifanya kuwa bize muda wote na majukumu ya kiofisi kuliko hata familia au waume zao mara nyingi hawa wanaibiwaga waume zao na ma'house girls.

5. MKE MGONJWA (Sick wife)
Hawa muda wote ni wachovu na wanyonge, utasikia akilalamika kuumwa mara hiki mara kile huku hawaendi hospitali. Na wana lawama kama nini usiombe ukutane naye utajuta.

6. MKE MWALIMU MKUU (Headmistress)
Hawa hugeuka viranja ndani ya familia hata mbele ya mume wake anajifanya muelekezi mkuu na huuliza maswali kwanini hii hivi mara hicho hivyo pasipo kujali kuna nani hata kama kuna mgeni.

7. MKE NGUMI (Fighting wife)
Hawa muda wote ni wavarangati, na akiamua kulianzisha huwa hawaangaliii mazingira na ataongea bila mipaka na kama unaishi uswahilini kila jirani lazma atajua kimenuka, yuko radhi kukunjana na mume wake.

8. MKE NDOO YA TAKA (Dustbin wife)
Hawa huwa wachafu kupita kiasi hawajali hiki cha thamani au laa, utamkuta mchafu muda wote ni mara chache kutokelezea labda kwenye sherehe. Mara nyingi waume zao wanawakinai mapema

9. MKE MLINZI (protective wife)
Hawa huwabana waume zao mpaka kero, hujifanya wana wivu, wanawaona wanawake wote kama maadui na hawataki hata kuona rafiki yake akiwa karibu na mumewe. Anahisi anaibiwa ukirudi nyumbani badala ya kupokea mzigo mkononi anakupokea simu ilioyoko mfukoni.

10. MKE MZURI (Agood wife)
Hawa ndo wale walioandikwa kwenye vitabu vya dini. Hawa ni wapole wanyenyekevu, wasikivu hata kama amekosewa anatumia busara kumaliza matatizo yao. Wana mapenzi ya dhati, ni walezi wazuri na wanajua maana ya upendo kwa waume na familia zao.

Swali langu kwako:
Je wewe ni namba ngapi?

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Mie namba 10 mie sio mjuaji wala nini?? I hope mume mtarajiwa kaona hilo ndio maana kasettle nakawa anaamani. Na furaha . Cc wakina haule cc: Leejay49
😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘
 
Back
Top Bottom