Unakumbuka nini wakati unafanya mtihani wa Kidato cha Nne

Wanajamvi.

Leo wanafunzi 572, 338 wa kidato cha nne kutoka shule 5,371 kote nchini wameanza mtihani wa taifa.

Hebu tukumbushane hapa nini hasa unakumbuka wakati unafanya mtihani wa kidato cha nne
Sintosahau paper limevuja, tukafanya solving usiku mzima, kuingia kwenye mtihani kitu chenyewe kabisa, ile imefika nusu saa tukaambiwa tusimame wakakusanya makaratasi yao wakatugawia mtihani mwingine, nusu ya darasa tuliangua vilio
 
Nilifanya mtian nikiwa mgonjwa nakumbuka kauli ya katekista aliekuja siku chache kabla ya kuanza kwa mitiani. Alisema "kuna watu watafanya vibaya mitiani yao na watasingizia ugonjwa/kuumwa" hii kauli ilikuwa inazunguka kichwani mwangu mpaka matokeo yalipotoka. Kipindi nasubiria matokeo nilikonda kikabaki kichwa tu, wiki baada ya matokeo niliongezeka mpaka mama akawa ananiambia kweli mwanangu ulikuwa na stress za matokeo.
 
Hhahhahahahahaha, matokeo yalikuwaje mdau?
Mkuu acha tu. Kuna watu wengi tu walikuwa na wasiwasi eti nitapata Div zero kumbe siku zote nilikuwa nawachora tu kwamba "masikini wanajipa hofu ya bure tu". Mhusika mwenyewe kumbe nilikuwa naishi nikijua nitapa Div I fulani ya kibabe sana. Yesu alijua kunifurahisha.

Imeandikwa

"Na kwa habari ya mambo yajayo (Roho wa Mungu)atawapasha habari zake". Hilo ni miongoni mwa mambo mengi yanayohusu future yangu ambayo Mungu kwa Roho wake amewahi kunipasha habari zake. Ndio maana nimekomaa nae hadi leo

Ninyang'anye vyote ila sio Yesu. Hiyo itakuwa ni hasara ya milele kwangu. Sitaona umuhimu wa kuwepo kwangu hapa duniani
 
Sintosahau paper limevuja, tukafanya solving usiku mzima, kuingia kwenye mtihani kitu chenyewe kabisa, ile imefika nusu saa tukaambiwa tusimame wakakusanya makaratasi yao wakatugawia mtihani mwingine, nusu ya darasa tuliangua vilio
Hahahahhahhaaha, pole sana, ni mwaka gani hiyo?
 
Nilifanya mtian nikiwa mgonjwa nakumbuka kauli ya katekista aliekuja siku chache kabla ya kuanza kwa mitiani. Alisema "kuna watu watafanya vibaya mitiani yao na watasingizia ugonjwa/kuumwa" hii kauli ilikuwa inazunguka kichwani mwangu mpaka matokeo yalipotoka. Kipindi nasubiria matokeo nilikonda kikabaki kichwa tu, wiki baada ya matokeo niliongezeka mpaka mama akawa ananiambia kweli mwanangu ulikuwa na stress za matokeo.
Pole sana, ndio maana tunaambiwa tuwe makini sana na maneno tunayowasemea wengine
 
Mkuu acha tu. Kuna watu wengi tu walikuwa na wasiwasi eti nitapata Div zero kumbe siku zote nilikuwa nawachora tu kwamba "masikini wanajipa hofu ya bure tu". Mhusika mwenyewe kumbe nilikuwa naishi nikijua nitapa Div I fulani ya kibabe sana. Yesu alijua kunifurahisha.

Imeandikwa

"Na kwa habari ya mambo yajayo (Roho wa Mungu)atawapasha habari zake". Hilo ni miongoni mwa mambo mengi yanayohusu future yangu ambayo Mungu kwa Roho wake amewahi kunipasha habari zake. Ndio maana nimekomaa nae hadi leo

Ninyang'anye vyote ila sio Yesu. Hiyo itakuwa ni hasara ya milele kwangu. Sitaona umuhimu wa kuwepo kwangu hapa duniani
AMen
 
Back
Top Bottom