Mimi nakumbuka enzi hizo nipo shule ya msingi mengeni pr school marangu namkumbuka sana mwalimu wangu kiwoli msimu wa mahindi ya kukaanga ukifika unakuta jamaa kakaanga karibu nusu rambo lol ikifika kipindi cha mapumziko ukijichanganya tu kutoka nje unakuta mahindi yote yameliwa nakumbuka kipindi cha kufunga shule inabidi ukae vizuri usigombane na mtu manake lzm utasikia kuna ngumi sehemu bas wakati wa kutoka wanafunzi karibia woote siku hiyo watabadilisha njia kwenda kushuhudia ngumi ama kweli utoto raha wewe unakumbuka nini?
Nakumbuka wakati nipo darasa la sita kuna mwalimu alikuwa ametukusanya waschana wote kuanzia darasa la tano hadi la saba kwaajili ya kutufundisha masuala ya kuvunja ungo na akaja na pakti kibao za always.
Kwa kipindi hicho nilikuwa bado sijapasua masinia so always zilikuwa ngeni machoni pangu, kabla ya yote mwalimu akatuuliza swali, "mnaijua always?" tukaitikia "ndiyooooooo"
mwalimu... "anaejua anyoshe kidole atueleze"
mimi nilikuaga na kiherehere sana darasani cha kunyosha kidole, basi nikanyoosha huku nikisema "mimi mwalimu najua"
mwalimu nae bila hiyana akanipoint "haya tujibie"
mimi kwa sauti kubwa ya ujasiri kabisa huku nikivuta maneno nikajibu "mwaaalimuuuu alwayyyyyyys koookaaakkkooolaaaaa"
mwalimu akasema "nini?"
nikamwambia bila aibu ni cocacola mwalimu.
Yaani nilichekwa darasa zima hadi nikalia maana nilijiona niko sahihi kutoka na kibwagizo cha tangazo la cocacola "always cocacola"
ladydoctor upo dada? olweisi koka ....
hahahaaaaaaaaa mayo weeee,nahisi kiherehere kilishia hapo hapo.
Nimemkumbuka demu wangu , Betrece niliyeanza nae darasa la 3! Alikua binti wa class teacher wetu.
ugomvi ndo kitu nilichokuwa nakipenda
blaza huyo demu yuko wappi tukamsalimu sasa...?Nimemkumbuka demu wangu , Betrece niliyeanza nae darasa la 3! Alikua binti wa class teacher wetu.
blaza huyo demu yuko wappi tukamsalimu sasa...?
Currently she's Chairperson of one of Parastatal firm within the country .
nakumbuka tulisoma kitabu hichi darasa la tatu
sikumuelewa mwalimu alimaanisha nini mpaka
sayansi kimu akaingia na kitabu hichi na
kuanza kutufundisha wakati hatuelewi chochote kipindi hicho
labda nyakati hizi za sasa hebu kione na wewe utaelewa hapa
View attachment 123270