Ngoja niongeze la kwangu:
Kuna siku ilikuwa asubuhi ya saa tatu siku ya jumamosi ,nilikuwa naelekea school kwa ajili tuition ya form IV, basi njiani nilimwona mdada mrembo mzuri sana mweupe Mhehe, huyo dada aliniangalia sana kiasi kilichonifanya nimwangalie na kujiuliza kulikoni kuniangalia kiasi hicho?
basi sikutoa macho yangu kwake huku niliendelea kutembea.
Kwa bahati mbaya kwa mbele kulikuwa na mtaro na sikuliona mtaro wakati natembea huku namwangalia mdada,nikatumbukia mtaroni bahati ilikuwa ya udongo ingekuwa ya simenti ingekuwa balaa, wacha yule dada alinicheka saaana, nikanyanyuka taratibu na kusepa kimyakimya,tuition mambo hayakuingia akilini.
Niliporudi nilipita njia hiyohiyo,bahati nilimkuta mdada tena njiani,alinisimamisha na kuniongelesha
Mdada: Pole kwa mtaroo!!
Mimi: Ahsante!
Mdada: Viiipiii?
Mimi: Sijakuelewa!
Mdada: Hunielewi?
Mimi: Lipi ulinitaka nikuambie?
Mdada: Hujanielewa mpaka saa hizi?
Mimi: Shida yako ni nini?
Mdada: Si hii!!
Khaaa! Hapo nikagundua alichotaka...!!!!