Unakumbuka kufanya kituko gani during foolish age? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unakumbuka kufanya kituko gani during foolish age?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, Aug 3, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]Ilikuwa ni baada ya kumaliza paper ya mock (Form Four Mock Examination)miaka kadhaa iliyopita! Baada tu ya kumaliza paper, nikajiona kama mkataba wangu na mambo ya skonga ndo ushaisha! Wiki iliyofuata, nikapiga full ndela-sikuibuka school hata siku moja! Washikaji wakaniletea ujumbe kwamba Brother Masabo (Alikuwa ndie Headmaster-S.t. Anthony’s Sec. School) ananitafuta ile mbaya! Kwamba kila siku alikuwa anaibuka class kuulizia kama nimekuja shule! Taarifa hii nililetewa wakati nakusudia kuibuka skul wiki inayofuata! Hata hivyo, baada ya kuambiwa Bro. Masabo ananisaka, nikaanza kuogopa na kuachana na mpango wa kutaka kwenda skul wiki iliyofuata! Wakati nafikiria hivyo, nikajiuliza nitamweleza nini Bro. Masabo! Baada ya kutafakari sana, nikakumbuka mstari mmoja wa Bob Marley kwenye track iitwayo WAR! Kipande cha mstari huo kinasema “TOTAL DESTRUCTION, THE ONLY SOLUTION!” Nami nikaona suluhisho la kisanga nilichozusha ni kufanya total destruction!!![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Wiki iliyofuata, nikamwomba mshikaji mmoja aitwae Sweetbert aende mwa Mwalimu wa Darasa akatoe ripoti kwamba naumwa! Aliponiuliza endapo teacher angeamini; nikamjibu acha asiamini kv siku ya siku nitaenda kumthibitishia Bosi wake kwamba nilikuwa naumwa! Nikaendelea kumweleza kwamba “Sitamthibitishia kwa vyeti, bali kwa vitendo!”[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kama tulivyokubaliana, wiki iliyofuata mchizi akapanda gari hadi St. Anthony’s na kupeleka taarifa kwamba nipo hoi! Inavyoelekea, Ticha wa darasa hakuamini, lakini sikujali kv nilishapanga kwamba Bosi wake(Bro. Massabo) ataamini tu kwamba nilikuwa taabani.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Nikaongeza wiki zingine tatu(3) za utoro, nikatimiza mwezi mzima bila kwenda shule!Utoto bana! Siku niliyoamua kuibuka skul ni siku ambayo ilikuwa inaanza Pre-National Exams! Mchizi nikachukua masizi meupe nikadondoshea mafuta ya kula kidogo kisha nikajipaka kwenye lips! Mzee kujicheki kwenye kioo, lips zilikuwa nyeupeeee, kama mgonjwa ngoma au typhoid! Nikaona YES, success in first step! Nikaibuka skonga, huku nikiwa mnyonge maradufu!!!! Sikuongea na m2, kwa kuogopa yasije masizi yangu yakafutika!!! Nikaingia Class, na mara paper ya CIVICS ikagawanywa tayari kwa kuanza Pre-National Exams! Nikafanya swali la kwanza hadi la tano, mara nikaanza kutetemeka(KUJITETEMESHA)! Kuanzia swali la sita hadi la tisa, nikabadilisha mwandiko na kuwa kama ni wa mtoto wa darasa la kwanza!Hata hivyo, nilipofika swali la tisa, nikaongeza kasi ya kutetemeka hadi Msimamizi aliponiona! Jamaa ile kuniona tu, akaanza kutaharuki! Manake nilikuwa nimebadilika vibaya mno, mithili ya mtu aliyepandisha mashetani! Jamaa akaagiza nitolewe darasani hadi dispensary ya hapo skul! Pale dispensary waliponiona tu, wakaona ile issue ni mzito kwao! Kwani licha ya kutetemeka kupita kiasi, nilikuwa napiga makelele isivyo kawaida! SIO SIRI, ILITISHA! Sijui niliutoa wapi ule ujasiri![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Pamoja na yote hayo, bado akili yangu ilikuwa kwa Brother Massabo! Ni yeye peke yake ndie niliyetaka kumthibitishia kwamba nilikuwa naumwa taabani! Na kwakuwa issue yangu ilionekana ni mzito sana; ilibidi akaitwe Headmaster Brother Massabo!! Dakika mbili baadae, Bro Massabo akaja huku akionesha dalili zote za kutaharuki! [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]“NasDaz, nini! Umekumbwa na nini!” Nakumbuka Brother Massabo aliniuliza mara alipofika eneo la tukio! Akili yangu ikasema “nilikuwa nakusibiri wewe hapo Brother Massabo!” Badala ya kujibu, mzee nikaongeza kasi ya kujitetemesha na kupiga kelele hadi mwenyewe nikaanza kujiogopa! Kuona vile, Brother Massabo akaamuru atafutwe mtu anayekufahamu home! Sijui ni kwanini jamaa hakutoa wazo la kupelekwa hospital; inawezekana aliona haukuwa ugonjwa wa kawaida! Tena wana bahati, wakati ule nilikuwa sifahamu lolote kuhusu kupandisha mashetani; manake wangenikoma![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Baada ya Bro. Massabo kuamrisha atafutwe mtu anayekufahamu home, ikabidi nishushe mashetani kidogo ili nipate nafasi ya kumtaja mtu anayekufahamu home! “Habibu....!Habibuu...!Habibu Mabehewa!” Nakumbuka kumtaja mshikaji mmoja ambae wakati huo alikuwa ama Form I au Form II! Habibu akaenda kuitwa, na alipofika na kunikuta na hali niliyokuwa nayo; nae nikaona anaanza kulengwalengwa na machozi!Angekuwa demu, naamini angelia tu!NILITISHA BWANA!![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Ili nisiwafie mikononi, Brother Massabo akatoa gari yake binafsi ili nipelekwe home tukiambatana na Habibu, Dereva na Mwalimu Mtiro! Safari ikaanza, na tulipoenda mbali kidogo Mwalimu Mtiro akataka kuleta ukuda wake wa kiualimu!! Eti badala ya kupelekwa home, nipelekwe hospital!! Jamaa sijui alinishitukia kwamba nafanya sanaa, au ndo alikuwa ananihurumia nisije nikafia home! Kuona hivyo, nikashusha mashetani kidogo ili nipate nafasi ya kutetea uamuzi wa kurudishwa home badala ya kupelekwa hospital! [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Nikashinda, hivyo safari ikaendelea! Mbele kidogo, Mwalimu Mtiro akajibu nakaa wapi! Nikawahi kujibu kwamba nakaa Kurasini Kota za Bandari! Nikahisi habibu ni kama alishangaa ni kwanini nimesema nakaa huko! Hakufahamu na ndio maana niliwahi kujibu kv nilijua angejibu yeye angetaja mitaaa ya JKT! Huko kote ni kwetu, but JKT walikuwa wanaishi wazazi wangu ambao wangeshangaa sana kusikia eti naumwa karibu mwezi mmoja sasa(Kuna mida nilishusha mashetani na kuwapiga fix kwamba nilianza kuumwa soon after Mock Exams)! Na huko Bandari ndiko nilikokuwa naishi na uncle wangu lakini wakati huo nilikuwa alone kv uncle alikuwa safarini! Naamini Habibu angetaja JKT kv alijuwa pale bandari nilikuwa naishi peke yangu![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Safari ikaendelea! Mbele kidogo Mr. Mtiro akauliza naishi na nani! Nikamjibu nipo peke yangu. Akauliza endapo nina ndugu ili akafuatwe aje kukaa na mimi kwa wakati huo! Nikajibu ndio, ninao![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Safari ikaendelea, huku nikipiga mahesabu nitamweleza vipi Habibu kuhusu ni ndugu gani anayetakiwa kutaarifiwa juu ya ugonjwa wangu! Nilijua, taarifa hizo zikipelekwa home lazima wangeshangaa kv ni jana yake tu nilikuwa nimetoka kuuchapa wali maharage kwenye meza yao![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kama zali, Mr. Mtiro akajisahau kwa sekunde chache! Bila kupoteza muda, nikamnong’oneza Habibu “wapeleke kwa Sweetbert!” Mchizi akanielewa, ingawaje ni kama alizidi kukumbwa na mshangao kuhusu ugonjwa wangu! Huyu Sweet, ni mchizi wangu na ni Bro. wa huyu Habibu!![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Nikafikishwa gheto, kisha Habibu akaondoka tena na akina Mr. Mtiro ili afuatwe ndugu yangu! Kama nilivyokuwa nimemtonya, Habibu akawapeleka kwa Sweet ambae nae akaletwa kwa mgonjwa! [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Ninachokumbuka ni kwamba, hata Sweet alipokuja home aliiingia chumbani huku akiwa ametaharuki! Sielewi aliambiwa nini kuhusu ugonjwa wangu![/FONT]
  [FONT=&quot] “NasDaz, vipi kwani?” Sweetbert aliniuliza huku akiwa ametaaharuki mara baada ya kuingia chumbani kwangu![/FONT]
  [FONT=&quot] “Vipi, wameshaondoka?” Badala ya kumijibu nilikumbwa na maswahibu gani mimi nilimtupia swali katika namna ya kunong’ona! Hata hivyo, badala ya kujibu nae akaangua kicheko kwani akagundua sikuwa na mapepo wala nini; bali ni sanaa! Muda huo, Mr. Mtiro nae alikuwa keshaondoka baada ya kumfikisha mgonjwa home![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Brother Massabooooooo!!!! Wherever you are, forgive me man! That small play was all about saving myself from your punishment!! Mr. Mtiro, na wewe nichunie ticha wangu, si unajuwa tena mambo ya uanafunzi! Kwanza hata form zenu za kujiunga kuna kipengele kinasema “sometimes, use your common sense!” LOL![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kesi yangu na Brother Massabo ikaishia hapo! Wala hakuniuliza kwanini baada ya kumaliza Mock sikwenda shule! Angeniuliza nini wakati mwenyewe kashuhudia kwa macho yake kwamba nilikuwa mgonjwa mahututi?! Au kama ni wewe ungekuwa ndie Brother Massabo ungefanya nini?![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Hicho ni kisa kimojawapo tu nilichokifanya enzi zileeeee za uendawazimu, manake sio utoto! Bila shaka, hata wewe una visa kama hivi ulivyovifanya hususani enzi za primary school na sekondari! Tudadavulie bathiiii!![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  haya kaka jiunge na kina kanumba ufanye sinema za kibongo basi
   
 3. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Hahahaha!!Natengenezea movie!
   
 4. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Duh... Huo haukuwa ujanja lakini...

  will come back with mine kabla sijaanza kazi za huduma za kiroho
   
 5. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Ni zaidi ya usanii...
   
 6. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Duu, Mkuu u'r are great actor !! kama umeweza kuvuta mind za watu kadhaaa na wakaelewa kweli wewe ni mgonjwa!!!

  That's one of your lost talent - Incase kama umeitupa au huiendelezi !!

  Nimechakaa sana NasDas !!!
   
 7. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Walio soma Meta sekondari kule Mbeya wanamkumbuka sana bwana mmoja alikuwa anaitwa amfre Bujiku pamoja na rafiki zake Gerald Hongoli, san jako na gillbiz.
  Huyu jamaa amfre ndiye aliyekuwa kinara, akipiga walimu, kubomoa ukuta na vibweka vya kila namna.
  Alibandika bango kubwa kwenye geti la kuingilia shule kuwa shule imeuzwa.
  Akiingia shule anaruka ukuta na wakati wa kutoka alikuwa anaruka ukuta.
  Jamaa sema alikuwa jinias sana, nasikia kwa sasa yuko Dar ametulia sana na anafanya kazi ya maana sana kwenye benki moja kubwa.
  Dada yake naye alikuwa mtemi ile mbaya, mavazi yake ni jinsi na mabuti nilikutana naye Arusha ni meneja wa custumer servive pale standard chartered.
  Yaani hao ndugu ni full utata brooo
   
 8. k

  kisukari JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  Story ni ndefu lakini imenichekesha mno.you make my day.
   
 9. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Nahofia tu kupoteza madogo wa leo lakini jamaa ninge-meet nae tufanye ka-movie flan hivi
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Mimi nakumbuka nilikuwa na safari yakutoka kariakoo
  kwenda mwenge ,kufika kariakoo nikaona mwanamke mrembo...
  Nikaanza kumfata nyuma nyum,a ili nipate nafasi ya kumtongoza...
  Yule mwanamke akaingia kwenye basi,na mimi nikaingia bila kujua basi linaenda wapi

  kumbe basi linaenda mlandizi....

  Nikauchuna hivyo hivyo mpaka mlandizi....ile kushuka tu mwanamke akaingia kwenye gari ya mumewe na mimi tamaa ikaishia hapo hapo

  nikaanza utaratibu wa kurudi na hiyo ni kutoka saa sita mpaka karibu saa kumi.....

  Yaaani..............................
   
 11. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Mnhh...:lie:...:lie:...:lie:...:lie:
   
 12. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  SURE, haukuwa ujanja lakini it worked coz' nilishinda soo! Unafanya mchezo na Brother Massabo nini!!!
   
 13. Qulfayaqul

  Qulfayaqul JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2010
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 471
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Dah noma sana nilishawahi kumtandika mimba binamu yangu sintasahau.
   
 14. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Astaghfirullah! Lakini kwenu si rukhsa bana!!!?
   
 15. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Umeona enh?! Tena unajua nini, nachukua kisa hiki na vingine (kama cha mkuu Boss na vya mndava wa Meta) including vya kubuni then movie NOTORIOUS STUDENT inakuwa released! tittle kidhungu, ndani kiswahili-kwanza mi mwenyewe bonge la mtunzi!
   
 16. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ee bwana umenikumbusha mbali miaka ya 1998-2000 hapo shuleni hapo Meta palikuwa na mob moja lilikuwa linajuliana kama mob deep hawa jamaa walishindikana, kwanza walevi wakubwa, then kuna mmoja wao
  alikuwa mfupi jina sikumbuki huyo yeye daima daika 3 mbele, siku kulikuwa na disko ya kuwakaribisha kidato cha tano, kafika getini kalewa mbaya makamu mkuu wa shule aliyekuwa anaitwa Mageta,
  akamletea za kuleta acha amtandike mangumi
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,412
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana Boss, sijawahi kucheka hapa jukwaani tangu niingie kama nilivyocheka leo yaaani! lol! we mtundu sana hahahahahaha. Naona unapenda Warembo kweli. Nini hasa kilikuvutia na huyo mdada guu la kihaya, **** la kukata, sura ya kuvutia sana au shingo ya upanga?
   
 18. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Dah Milambo...2002..Kuna Jamaa alikuwa analetewa wa wali na nduguze wakati tuko hostel..sasa tunamuomba tumege nae kila wakati anatunyima anasema hautosho..utaratibu huo ukaendelea kwa mwezi mpaka tulipo pata solution.

  Yule mkuu alikuwa anaweka wali na mchuzi kwenye locker sasa tukamtegea kaondoka kwenda prepo...dah wacha tuchukue lile locker si alikuwa kaweka kufuri basi kulitikisia up and down side by side..mpaka tulipo amini kuwa sasa mchuzi,wali,nyama and nguo zake alipo hifadhi na wali vimepata mchachuko sawia na sie hao tukatembea mbali....baada ya masaa matatu kurudi...matokeo ya tukio lile hata hatukuamini...tulikuta mstali wa nyenyere(sisimizi) wakielekea na kurudi toka kwenye locker..yule bwana kufungua...kuanzia uniforn vingine vilikuwa vimekuwa wali na mchuzi..that was end of uchoyo wa wali hsa school za boarding..dah.

  Buswelu
   
 19. kaitlynne

  kaitlynne Member

  #19
  Aug 6, 2010
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uwwwiiiii mbavu zangu. sijawahi cheka hivi. watu mna vituko!!
   
 20. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  kituko nilichofanya ni nilikuwa nakula hela ya tution na naishia kucheza football. ikaundwa mbinu ya kunibana kila nikienda nikapewa daftari ambalo mwalimu wa tution awe ana weka sahihi narudisha nyumbani wanahakiki.baada ya mbinu hiyo nikajifunza kufoji sahihi.

  Katika siku tatu za tution nilikuwa nahudhuria siku 1ja tu. kama mobile zingekuwepo na zingekuwa ni nafuu kwafamilia za kikulima nadhani nisingekuwa sina ujanja.

  Sasa basi nilikuwa navizia wale walioenda tution nacheki daftari zao nakopi maswali na majibu na kujisahisha then najipa VIzuri sana then naliwakilisha kwa mom abaye ndiye alikuwa Auditor wa familia.teh teh teh lakini baada ya muda mrefu na kugundulika ilibdi walegeze kamba nikapewa ruhusa rasmi jumamosi na jumapili kujirusha na kucheza football kama nitakavyo.

  In between nakumbuka nilibadilisha matokeo kutoka kuwa wa 29 . Nikafanya usanii kufuta 2 ikabaki 9. Hi ni sababu nilihaidiwa zawadi ya baiskeli siku nikiingia kwenye kumi bora. So badala ya kuwa wa 29 nikawa wa 9.

  Teh teh teh. it was really foolish
   
Loading...