Unajua unaweza kuwa chanzo cha kuharibu maisha ya baadaye ya mtoto wako kwa kuweka picha/video zake mtandoni?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wakuu,

Imekuwa ni kawaida au tuseme fashion kwa wazazi/walezi kupost picha au video za watoto mtandani.

Picha au video hizo zinaweza kuwa za vichekesho, matukio mbalimbali ya maisha au mtoto anaambiwa afanye tukio fulani huku akirekodiwa na kisha kupostiwa mtandaoni au hata vitendo vya aibu ambavyo watu wazima huona kama vichesho/utani na kuweka mtandaoni kwa lengo la kufurahi tu kutokana na maudhui hayo.

Umeshawahi kufikiria mtoto wako atajihisi vipi akikutana na picha/video zake unazoweka mtandaoni, umeshawahi kujiuliza itaathiri vipi uhusiano wake na majirani, watu wa rika lake, kwenye ajira nk?

Mfano, umeweka video ya mtoto wako kafanya tukio analia, kamasi zinamtoka, au tukio lolote lile la aibu, mtoto huyu anakuja kuwa mkubwa yuko ofisi fulani siku ya siku ameteleza watu wanakuja kuibuka na picha yake akiwa kwenye hali hiyo na kutumia kumdhalilisha, hata ingekuwa wewe ungejisikia vizuri?

Huo ni mfano mdogo tu, lakini kuna watu wanarekodi watoto wao au kupiga picha ambazo hazifai, za aibu, zinazoweza kusababisha msongo wa mawazo kwa mtoto wako baadae na kwa hatua mbaya zaidi mtu anaweza hata kujiua ili tu kuondokana na kadhia ya kuchekwa, kudharauliwa, kutukanwa kutokana na ulichopost mtandaoni akiwa mdogo.

Wewe unatakiwa kuwa wa kwanza kumlinda mtoto ambae hawezi kujitetea na sio kumdhalilisha.
 
Upo sahihi kabisa, kuna dada mmoja alikuwa akimpost sana mwanae.

Sasa ikatokea ajiitae mtaalam wa mambo ya afya na lishe mtandaoni akawa anaelezea matatizo ya lishe kwa watoto, mwisho wa siku akaweka picha ya huyo mtoto wa huyo dada kama mfano wa muonekano wa mtoto aliyekosa lishe bora.

Dada mwenye mtoto akaanza kung'aka na kulalama kwamba waache kumshobokea mwanae, kwani amewakosea nini hadi wamtolee mfano.

Basi tusio-mind visa kwa chinichini tukasema ohooo.
 
inategemea umeweka picha ya aina gani,Cha msingi isiwe picha ya kumdhalilisha mtoto ila Kama ni picha ya kawaida Mimi sioni shida
 
inategemea umeweka picha ya aina gani,Cha msingi isiwe picha ya kumdhalilisha mtoto ila Kama ni picha ya kawaida Mimi sioni shida
Inaweza ikawa sehemu ya traffickers kupata taarifa zote za mtoto wako,unapost mnapoishi, akiwa shuleni, mkienda kanisani, matukio mblimbali ya kifamilia,yaani kupitia mtandao mtu anapata taarifa zote za kumpata wako...unaweza usiweke cha kumdhalilisha lakini ukamu expose lwenye hatari nyingine

Sent from my Infinix X693 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom