Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,116
Ni kama fashion sasa hivi watu kuwarekodi watoto kwa video fupi au kuwapiga picha wakiwa katika harakati zao za maisha ya kitoto.
Kwa kuwa mtandao imekuwa mbadala wa albam kwenye kutunza kumbukumbu ni jambo jema kutunza kumbukumbu za makuzi ya mtoto iwapo unaona ni lazima ukatunze mitandaoni kwani bado zipo njia nyingine za kutunza bila kuwapost mitandaoni.
Ila naona hali inazidi kuwa mbaya sana kwa wazazi na walezi kutafuta watoto wao kutrend kwa kuwarekodi video mbaya ambazo natumai hazina wema kwa dunia inakokwenda kwa kuwa mtandao hausahau zitamrudia hata atakapokuwa mkubwa.
Wapo wazazi wanawapa script watoto wameze ili warekodiwe, wakati mwingine ukipima maudhui anayotoa mtoto na umri wake unaona kabisa mtoto anafanyishwa jambo ambalo linamkuza kiumri sana hakuoaswa kutamka au kufanya kitendo hicho katika umri huo, mfano wapo wanaowachezesha nyimbo zinazoimba mapenzi, ivyo huwaweka jinsia mbili tofauti na kuwafundisha kukumbatiqnq kushikana kukiss nk.
Lakini wapo wanaowaacha watoto wapande, waingie sehemu ambazo unaoana kabisa zilikuwa hatarishi kwa watoto ili tu wapate video za kuweka mitandaoni, ipo siku litawakuta jambo na hamtapata wa kumlilia.
Unakuta katoto kadogo kanaimba nyimbo ambazo hata mtu mzima napata ukakasi kuimba mbele ya watu mbaya zaidi kanaima kqnakata viuno na kulala chini kanabinua kalio na mzazi anarekodi na kushangilia wakati mwingine anamsisitiza akate zaidi, jamani mnawapeleka wapi watoto? Mnaanda jamii ya aina gani?
Kabla hujaweka maudhui yoyote yanayomuhusu mtoto, jiulize.
Mtoto akiyamwaga mauno na watu wazima wanamshangilia😭
Mtu anawaza kupiga picha bila kuangalia huenda ataumizwa na mashine ya kufulia anayoingia.

- Je, mtoto akikua atafurahia kuona alifanya/ au kufanyishwa kitendo hicho?
- Je, haitaharibu mtazamo wa watoto wenzake watakaoona video hiyo na kumuona hana maadili?
- Je, Video hiyo ikibaki mtandaoni haitatoa picha ya malezi au makuzi mabovu na kusababisha akaja kukosa fursa fulani ukubwani, maana kuna nyadhfa wanaangaoia hata malezi ya familia aliyokulia wanaotaka kumwajiri.
- Je, hautakuja kumtengenezea mtoto chanzo cha kupata dhihaka kutoka kwa jamii yake ya baadae?