Unajua athari ya tabasamu lako kwa mke wako?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Mwanamke! Kiumbe wa kipekee ambaye wanaume wengi hawajamfahamu kiusahihi!

Mwanamke, kiumbe "dhaifu" lakini mwenye nguvu ajabu!

Mwanamke ni kiwanda kinachoishi!

Mpe mchele, atakurudishia ukiwa umegeuzwa na kupewa jina jingine, wali!

Mhuzunishe, naye atakufanya "ulie" bila kupigwa!

Mwanamke! Mpe tabasamu...

Sitaki kukuambia athari ya tabasamu lako kwa mke wako, kama hujui! Itapendeza ukigundua mwenyewe. Na ukigundua, utaendelea kugundua na zaidi, na zaidi!! Ugunduzi mmoja utakupeleka kwenye ugunduzi mwingine. Itakuwa ni furaha baada ya Furaha!!!

Nakushauri kitu gani? Kugundua athari ya tabasamu lako kwa mke wako? Kwa jinsi gani? Fuata maelekezo hapa chini.

Kwa siku thelathini mfululizo, hakikisha Unafanya haya kila siku:
1. Kila umwonapo, tabasamu bila kujali kama anakuona au hakuoni

2. Uamkapo Asubuhi na hata urejeapo Jioni toka "kazini", n.k., msalimie kwa tabasamu!

3. Umalizapo kula chakula alichokupikia au kukutengea, mshukuru kwa maneno yanayosindikizwa na tabasamu!

4. Akiwa anapika, fanya kupita jikoni umwongeleshe neno lo lote zuri, likisindikizwa na tabasamu.

Na ukiona, labda umekaa sebuleni na yeye yupo, labda jikoni, halafu ukaona kama anapita uliko mara kwa mara, inawezekana akawa anahitaji umwongezee "dozi", tabasamu. Ukiweza, umfuate huko huko aliko ukapige naye stori kwa muda, au "full time", lakini hakikisha stori zinasindikizwa na tabasamu!

Fanya hivyo, na kabla ya mwezi kuisha, utaanza kugundua ambayo hukuwa ukiyafahamu kuhusu mwanamke. Hata kama ulidanganywa "jandoni" kuhusu mwanamke, ugunduzi wako utakuwa mwanzo wa kuanza kuujua ukweli halisi, wa "nguvu" ya mwanamke.

Katika kipindi hicho cha zoezi la kutabasamu, epuka kumwongelesha maneno ya kumvunja moyo au kumhuzunisha! Usimkosoe, na ikibidi kukosoa, ufanye hivyo kwa hekima na upendo mkubwa sana.

Ukiweza, uwe na diary ya kuandika kila siku kuhusu mke wako. Kila siku, uhakikishe unaandika jambo lo lote zuri linalomhusu, iwe ni sura yake, tabia yake, matendo yake, cho chote kile.

Kwa maneno mengine, uwe unayawinda mazuri yake kwa ajili ya kuripoti kitabuni, kwenye diary yako maalum kuhusu mke wako.

Fanya hivyo, na ndani ya mwezi mmoja unaweza ukagundua ugunduzi mzuri kumhusu mke wako, na mwanamke kwa ujumla, ugunduzi utakaokuacha kinywa wazi kwa furaha!

Unaweza kufanya hivyo?

Ni zoezi la siku thelathini tu lakini linaweza kukuletea manufaa makubwa sana!
 
Shauri yako
 

Attachments

  • FB_IMG_1684563130645.jpg
    FB_IMG_1684563130645.jpg
    15.4 KB · Views: 6
Acha ushamba utakunishwa nazi na tabasamu lako while wanaume wenzako wanapata deals out🤐 na HSE boy anakugongea
No reference no right to argue! Umeshawahi kulifanya hilo zoezi?

Nakudokezea tu! Ukimfanya mkeo ajisikie "malkia" wa nyumbani
kwako atakufanya mfalme hata kama wengine walikuwa wanakuona "kapuku".

Wanawake ni viumbe wa ajabu sana, I tell you!
 
We humjui Prisca we he he heeee

Umgonge mitabasamu yote hiyo atakwambia umeanza kuwa choko

Huwajui wanawake wewe
Mkuu, kuna kitu hujajua kuhusu wanawake. Simaanishi kila mwanamke, bali mke "wako" tu. Ukijua kumpenda "kiusahihi", utaupata moyo wake.

Kama hujui kuwa mwanamke anaweza akafikia hatua ya kuhakikisha kuwa anaishi kwa ajili ya "kumpendeza" mume wake, niulize mimi.

Lakini namna pekee ya kufikia hiyo hatua ni kwa njia ya upendo.

Ukimshibisha upendo, atakufaidisha kwa unyenyekevu.
 
Huwajui wanawake mkuu Ukimchekea Chekea Atakuchekea chekea Ukitaka Akupe Heshima na Nidhamu kama Kuruta na Kwata Atakupatia Pia
Nafikiri watu wengine huwa hawatofautishi hofu na heshima.

Mkuu, ulichomaanisha hapo ni hofu na nidhamu ya woga.

Mkeo akikuogopa, atakupa nidhamu ya woga. Lakini akikupenda, atakupa unyenyekevu unaosukumwa na upendo na siyo nidhamu ya woga.

Mke anayekuheshimu kwa heshima ya upendo, atakuwa upande wako wakati wote, hata ukiwa mbali. Atakuwa kama "mlinzi" wako.
 
Bora ukamchekea mamba kuliko uyoo mdudu.......
Unakosea sana kuwa na mtazamo huo mkuu.

Ujue tu kuwa "mwanamke" yupo vile alivyo kwa sababu ya mwanaume.

Katika uongozi, inaaminika kuwa "everything rises and falls under the leadership". Mwanaume ni kiongozi. Ukiona "mwanamke" kawa "mdudu" ni kwa sababu "mwanaume" hajasimama vyema kwenye nafasi yake.
 
Mm hakuna mwanamke na mdate asinipende na tabia yangu ni niko serious mda mwingi na nawaza sana hela .sijawah kuwa nampigia simu mwanamke sijui uko wap sijui nakumiss big NO .
 
Back
Top Bottom