Unajipaka mafuta gani mwilini?

Chukua nazi zako 3, 5, na kuendelea.
Kuna vizuri au kama huwezi kukuna waweza zibandua kisha ukakata vipande vidogo vidogo ukablend,
(me napendelea kukuna)

Ukishamaliza chuja upate tui zuri, waweza rudia tena kuchuja kama utaona tui lipo bado kwenye machicha,

Kisha tafuta mfuko wa nailon mweupe, (waweza tumia miwili au mitatu au hata mmoja, kutegemea na wingi wa tui lako)

Mimina tui kwenye mfuko huo, kisha ufunge kwa juu na uhifadhi sehem ambayo haitatikisika.

Acha kwa masaa kadhaa kuanzia ma 3,
Ukija kuangalia utakuta maji yapo chini na tui lipo juu, cha kufanya chukua mkasi kata kipande kidogo kwa chini kisha acha yale maji yamwagike (waweza kuelekezea kwenye sufuria au bakuli sio yamwagike chini.)

Mpaka ikikaribia na tui kutoka, bana lile tundu halafu elekezea kwenye sufuria unalotaka kuchemshia tui lako, achia lile tui lote, kisha tupia karafuu, au mdalasini au hiliki au vyote (kama utapenda kukata harufu kama mimi, kama hupendi acha usiweke hivyo viungo)

Chemsha tui lako huku unakoroga kwa mwiko usiache mpaka tui litakauka lote na kuonekana mafundo mafundo meupe na mafuta yatakuja juu. Endelea mpaka yale mafundo yaanze kua rangi ya kahawia (brown).

Shusha sufuria lako, acha kama dakika 10 yapoe kisha mimina kwenye chombo utakachotumia (chuja), tupia vile viungo kama uliweka.
Tayari kwa matumizi.

Asante kwa somo
 
Hebu wanaukumbi tushee hii kitu, hebu tuambizane. Je unatumia mafuta gani mwilini/lotion/cream? Unaogea sabuni gani?

Mimi kuanzia natumia lotion ya Ingram, naogea sabuni ya Pearl na mafuta ya nazi niliyotengeneza mwenyewe. Kila Jumapili natengeneza.
Matokeo nipo soft mpaka najitamani.

Wewe je?

NB: Natafuta foundation nzuri sijapata naombeni idea
ya nazi
 
WP_20161012_001.jpg
WP_20161012_001.jpg
WP_20161012_001.jpg
 
Napaka mafuta ya nazi minara naogea sabuni ya ozona vimenisaidia uso angalau kua vizuri. Nina wiki mbili toka nianze kuvitumia
 
Back
Top Bottom